DOKEZO Uchunguzi: 'Makanisa ya Kiroho' na shuhuda FEKI kuwahadaa watanzania

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Wakati ongezeko la nyumba za ibada maarufu 'Makanisa ya Kisasa' likizidi kushika kasi Nchini Tanzania, kuna baadhi ya makanisa hayo yanatumia shuhuda za uongo (feki/za mchongo), kujizolea maelfu ya waumini kisha kujipatia fedha kwa mgongo wa sadaka.

Uchunguzi ulioufanywa na kikundi cha wazalendo kwa siku 180 (kuanzia Februari hadi Julai 2023) katika makanisa tofauti ndani ya Dar es Salaam na mikoa mingine kadhaa umebaini mambo kadhaa ambayo yanaweza kutumika kama mfano wa kinachoendelea katika taasisi kadhaa za dini.

Code name ni "Shaba" (jina la ufunguo)
Ndani ya uchunguzi wetu, kuna msamiati wenye maana tofauti na ilivyozoeleka wa neno “Shaba” ambao utambulisha watu maalum wanaodaiwa kukodishwa ama kulipwa ili watoe shuhuda za uongo, kwa lengo la kuvutia waumini na kujizolea fedha zao kupitia sadaka.

Watu maarufu wakiwemo wasanii (wa maigizo) wanapewa fedha ili kutoa shuhuda feki kwa lengo la kuongeza ushawishi kwa waumini kutoka madhehebu mbalimbali.

Ananukuliwa muumini mmoja akisema "Mimi nilikuwa Kanisa la...(jina tunahifadhi kwa sasa), lakini nilihama kwa kuwa matatizo yangu hayakutatuliwa licha ya kufuata maelekezo yote aliyokuwa anatoa Nabii.

“Hivyo baada ya kusikiliza redio na kuona TV katika kipindi cha Nabii...(jina tunalihifadhi kwa sasa), nimeona kila siku watu wanatoa shuhuda za kufanikiwa nami nikavutiwa kuja hapa."

Akaelekea katika “Kanisa jipya kwake” Jumapili moja ya Juni 2023, akaomba msaada kwa watumishi wakampa ushuhuda ingawa kuna baadhi ya vipengele walikuwa wanasitasita kuvitolea maelezo.

Akafuata vile wanavyotaka wao, ndipo aliposhtuka baada ya kusikia kwamba ni kweli kuna baadhi ya watu wanatafutwa na viongozi wao kwa ajili ya kutoa shuhuda feki.

Aliyabaini hayo kwa kufanya uchunguzi wa kimyakimya, ndipo Muumini mmoja ndani ya kanisa hilo lililojizolea umaarufu siku za hivi karibuni akamweleza:

"Kuna kitu kinaitwa shaba; huu ni utaratibu wa kuigiza miujiza, watu wanacheza Shaba kila wakati kwenye makanisa, mimi nilipata dili baada ya kuunganishwa na mwenzangu ambaye amefanya hivyo kipindi kirefu.

"Alikuwa akiigiza kutokewa na miujiza mbele ya madhabahu, kuna dili alilipata lakini ikawa wanatakiwa watu watatu aliniunganisha na mimi, nilianza kwa kushtuka lakini aliponieleza nikazoea mpaka sasa nazunguka nyumba za Ibada tofauti," alidai mwananchi huyo.

'Muumini' huyo ambaye hapa tunampa jina la XXX anasimulia; "Mara ya kwanza nilitakiwa kufanya shaba mbele ya madhabahu kujifanya napandwa na mapepo, nilifanya hivyo nikavuta changu nikaondoka, baada ya hapo nimekuwa nizunguka na bosi kwenye maeneo tofauti ikiwemo mikoani."

XXX anaeleza kuna hatua inafika kiongozi wa kanisa hilo anakodisha mali za thamani ikiwemo magari kisha kuwapa wacheza Shaba ili wakaoneshe madhabahuni kuwa wamezipata baada ya kuombewa kanisani hapo, ilihali wakijua ni uongo.

"Wakati mwingine nafanya shaba nikionesha Maisha yangu yamekuwa ya mafanikio baada ya kuanza kusali kanisani kwa 'Mtume', naweza kutafutiwa mpaka gari ili nikaigize kuwa nimenunua gari baada ya biashara zangu kuanza kwenda vizuri.

“Ikiwa ni baada ya kutumia 'mafuta ya upako au maji ya baraka', kwa kuwa wanakuwepo watu wengi ambao biashara zao zinasuasua kwahiyo Shaba ya aina hiyo inakuwa rahisi kuamini," alidai muumini.

Malipo ni 'mazuri', si rahisi kushtukiwa
"Malipo ni makubaliano, binafsi nalipwa Sh. 150,000 hadi 300,000 kama nasafirishwa kwenda mkoani. Kuna shaba unazifanya zinaweza kuhatarisha usalama wako hapo lazima akuongezee dau.

"Ni vigumu shaba kugundulika maana inafanywa kwa uhalisia kiasi kwamba unakuwa unabaki bila mashaka hata ukiwa msomi shaba inavyofanywa lazima uamini."

Mlinzi wa Kanisa afichua
Mlinzi wa kanisa hilo maarufu lenye makao yake Kawe Jijini Dar es Salaam anafunguka kuwa wacheza Shaba wa kanisa hilo hutafutwa kwa siri sana.

Anasema "Binafsi niligundua baada ya muda mrefu kupita nikiwa hapa (Kanisani), tulikuwa tunawashikilia kwa nguvu wanapofanya maigizo ya kuzimia, baadaye unawaona wapo fiti wanachukua mzigo wao.

“Siku hizi nimewazoea, wapo wanaoigiza kukosa Watoto, mwingine anakuja na Watoto wasio wake pia wapo wanaoigiza kupata mali na utajiri.

"Walinzi wengi tumeshashtukia mchezo huo, sema ndio hivyo utafanyaje unalinda kibarua hata wenzako ukiwaona husemi.”

Watumishi waandamizi hula kiapo
Watumishi waandamizi ndani ya kanisa hilo (la Kawe), hulishwa kiapo cha kutunza siri za kiongozi wao, hivyo huwa ni vigumu kukupa ushirikiano pindi mtu anapotaka kufahamu upande wake wa pili. Aidha, Makanisa mengi yamewaajiri ndugu na jamaa zao wa karibu katika kuhakikisha kuna kutunza siri miongoni mwao.

Kanisa lilipo Kivule jijini Dar
Binti aliyejitambulisha kwetu kuwa anaishi Sinza lakini ni muumini Kanisa lililopo Kivule anaeleza alipewa fedha ili atoe shuhuda ya uongo kwamba amepata kazi baada ya kuhitimu chuo kikuu, wakati si kweli.

"Nimehitimu Chuo cha IFM kwa sasa najihusisha na biashara ya nguo za watoto na wadada. Mara ya kwanza nilifika kanisani kwa 'Mtume' anisaidie kuniombea nipate kazi na Mwanaume wa kufunga naye ndoa.

“Nilienda siku ambayo sio ya Ibada nikakutana na Mchungaji akanielekeza niende Jumapili hiyo siku nikaombewa lakini baada ya hapo yule mchungaji alinifuata akaniambia kuna dili la hela, ndiyo akanieleza wiki mbili mbele niigize kuwa nimepata kazi na Mume wa kunioa."

"Aliniambia nitapewa sh 200,000/= nikiweza kufanya hivyo lakini akinisisitiza niwe msiri. Ilipofika hiyo siku nilikuwa nimeshapewa maelekezo namna ya kuzungumza nikafika pale kwenye madhabau nikatoa ushuhuda wakanipa changu jioni ndio ikawa mwanzo wa kufanya 'Shaba', ndivyo wengi wanaita.

"Nimeenda mpaka mikoani kwa nyakati tofauti kwa ajili ya Shaba. Napangiwa sehemu ya kukaa kwenye siku tunazokuwa mikoani pesa ya kula na posho inakuwepo ukimaliza kazi. Kiukweli, shaba imenisukuma kimaisha."

Kanisa jingine lililopo Kimara, Dar
Mhudumu mmoja kwa siri atatufahamisha kuwa kanisa hilo huwapanga watu kwa ajili ya kutoa shuhuda za uongo kwenye vyombo vya habari, hususani kwenye runinga na redio.

Anasimulia "Wanakuja watu wengi sana lakini miujiza wala sio ya kweli. Kuna watu wanapangwa na watu wa habari ambao wamepewa jukumu hilo kwa kushirikiana na mhudumu maalum. Siku za ibada wanakuwa na watu wao, wakishawaandaa ndio wanakuja kuhojiwa ‘live’ wanatoa ushuhuda ambao unavutia wasikilizaji wengi.”

Uchunguzi wetu unaonesha kupitia baadhi ya vyombo vya habari vinavyomilikiwa na wakuu wa makanisa hayo vimekuwa vikitumika katika propaganda za kuvuta ‘wateja’.

Uchunguzi huu pia umefanywa katika kipindi ambapo makanisa kongwe (Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) na Kanisa Katoliki), yamekuwa yakiwasihi waumini wao kuacha 'kutangatanga' katika makanisa yanayowavuta kwa kigezo cha kusaka miujiza.

Michezo ya vipindi vya redio
Chanzo kingine kinaeleza “Kwenye vipindi vya redio napo tumefanya maigizo sana. Sisi ndio tunapiga simu redioni Mchungaji au mtumishi anapokuwa studio, tunaigiza kutoa shida zenu na kuchangia fedha, tunabadili sauti na kushikilia ‘line’ ili wale wenye shida za ukweli wasipate mawasiliano.

“Tunachokifanya hapo mtu akiwa anasikiliza ni rahisi kushawishika kuwa kiongozi huyo wa Kanisa anafanya maombi ya kweli na watu wanachangia kweli sadaka kubwa. Michezo hiyo ipo sana kwenye redio za makanisa haya ya kiroho na mpaka sasa bado inaendelea.”

Itaendelea sehemu ya pili...

Habari zinazofanana: Wawili akiwemo mchungaji washikiliwa na polisi kwa kulaghai mchawi kadondoka na ungo kanisani kwenye mkesha
Dini zimevamiwa na matapeli...
 
Kuna Jamaa kaanzisha...kanisa la mbogamboga...alianza na kupata sadaka laki 2...3....Sasa hivi kila jpili anakusanya si chini ya m10......
Ameanza na kubadili namna ya kuongea...maringo..madoido....kwa kifupi...kiburi..
Anataka watu wamtukuzee🙄🙄🙄
 
Kule kwa Papa, waamini wameambiwa wapeleke shuhuda zao kwa kulipa zaka, halafu eti hizo shuhuda zinapitiwa/ hakikiwa kwanza na kamati ya zaka!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
mleta hoja huko hapaoni, kakazana na makanisa ya kiroho. Nimuombe akayajue kwanza makanisa ya kiroho yakoje na mafundisho ni nini ndio alete utafiti wake tuuchambue tumpe ukweli wa mambo, naona kama anachanganya matango pori , magugu na ngano. Hawa watunga shuhuda za uongo ni wale waganga wa kienyeji walio advance kufuata wateja wao wanakokimbilia kwenye dini baada ya kuwagundua uongo wao. Wanawafuatilia wateja wao kulekule wanakoamini watatuliwa shida zao. Wateja wanapenda dini na waganga wao ikabidi wajibadili kuwa wa dini, matokeo yake ndio hayo maji na mafuta ya upako, keki ya upako na upuuzi mwingine mwingi ukishadidiwa na shuhuda za uongo. Watu wanabebwa na upepo wa kila aina mradi tu watatuliwe shida zao. Wakubwa kwa wadogo walinyweshwa kikombe cha dawa feki za mitishamba kwa ujinga
 
Nyie ambao mnajiona mko sahihi katika dini na madhehebu yenu kaeni na waumini vizuri, wafundisheni kweli ya Mungu wenu. Kama nanyi ni wapuuzi ni lazima mkimbiwe na waumini wenu, wanaenda kwa wapuuzi wengine zaidi yenu halafu mnakuja kulialia humu kuwa mnanyang'anywa waumini kwa shuhuda za uongo wakati nanyi ni wapuuzi walewale tu ila mmezidiana upuuzi wenu. Mnawafanya binadamu wenzenu kuwa watumwa wa fikra zenu kwa kuwabebesha mizigo mizito ya ujinga, maradhi na umasikini. Hubirini kweli iwaweke huru waumini wenu. Tokeni gizani mje kwenye nuru muone mwanga wa matumaini ya kweli
 
Hawa jamaa wanakera sana. Pamoja na hayo yote, bado Bwana Yesu anatenda miujiza ya kweli kupitia watumishi wake wa kweli wanaomtafuta Bwana na nguvu zake. LAKINI muujiza mkuu kwa mwanadamu ni ile hali ya kutubu na kuokoka. Yaani kuishi maisha matakatifu mbali na dhambi huo ndio muujiza mkuu kuacha dhambi. Mithali 28:13. Afichaye dhambi zake hatafanikiwa. Bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema.
 
Nyie ambao mnajiona mko sahihi katika dini na madhehebu yenu kaeni na waumini vizuri, wafundisheni kweli ya Mungu wenu. Kama nanyi ni wapuuzi ni lazima mkimbiwe na waumini wenu, wanaenda kwa wapuuzi wengine zaidi yenu halafu mnakuja kulialia humu kuwa mnanyang'anywa waumini kwa shuhuda za uongo wakati nanyi ni wapuuzi walewale tu ila mmezidiana upuuzi wenu. Mnawafanya binadamu wenzenu kuwa watumwa wa fikra zenu kwa kuwabebesha mizigo mizito ya ujinga, maradhi na umasikini. Hubirini kweli iwaweke huru waumini wenu. Tokeni gizani mje kwenye nuru muone mwanga wa matumaini ya kweli
Kibaya zaidi kajianika ye ni wa wapi
 
Wakati ongezeko la nyumba za ibada maarufu 'Makanisa ya Kisasa' likizidi kushika kasi Nchini Tanzania, kuna baadhi ya makanisa hayo yanatumia shuhuda za uongo (feki/za mchongo), kujizolea maelfu ya waumini kisha kujipatia fedha kwa mgongo wa sadaka.

Uchunguzi ulioufanywa na kikundi cha wazalendo kwa siku 180 (kuanzia Februari hadi Julai 2023) katika makanisa tofauti ndani ya Dar es Salaam na mikoa mingine kadhaa umebaini mambo kadhaa ambayo yanaweza kutumika kama mfano wa kinachoendelea katika taasisi kadhaa za dini.

Code name ni "Shaba" (jina la ufunguo)
Ndani ya uchunguzi wetu, kuna msamiati wenye maana tofauti na ilivyozoeleka wa neno “Shaba” ambao utambulisha watu maalum wanaodaiwa kukodishwa ama kulipwa ili watoe shuhuda za uongo, kwa lengo la kuvutia waumini na kujizolea fedha zao kupitia sadaka.

Watu maarufu wakiwemo wasanii (wa maigizo) wanapewa fedha ili kutoa shuhuda feki kwa lengo la kuongeza ushawishi kwa waumini kutoka madhehebu mbalimbali.

Ananukuliwa muumini mmoja akisema "Mimi nilikuwa Kanisa la...(jina tunahifadhi kwa sasa), lakini nilihama kwa kuwa matatizo yangu hayakutatuliwa licha ya kufuata maelekezo yote aliyokuwa anatoa Nabii.

“Hivyo baada ya kusikiliza redio na kuona TV katika kipindi cha Nabii...(jina tunalihifadhi kwa sasa), nimeona kila siku watu wanatoa shuhuda za kufanikiwa nami nikavutiwa kuja hapa."

Akaelekea katika “Kanisa jipya kwake” Jumapili moja ya Juni 2023, akaomba msaada kwa watumishi wakampa ushuhuda ingawa kuna baadhi ya vipengele walikuwa wanasitasita kuvitolea maelezo.

Akafuata vile wanavyotaka wao, ndipo aliposhtuka baada ya kusikia kwamba ni kweli kuna baadhi ya watu wanatafutwa na viongozi wao kwa ajili ya kutoa shuhuda feki.

Aliyabaini hayo kwa kufanya uchunguzi wa kimyakimya, ndipo Muumini mmoja ndani ya kanisa hilo lililojizolea umaarufu siku za hivi karibuni akamweleza:

"Kuna kitu kinaitwa shaba; huu ni utaratibu wa kuigiza miujiza, watu wanacheza Shaba kila wakati kwenye makanisa, mimi nilipata dili baada ya kuunganishwa na mwenzangu ambaye amefanya hivyo kipindi kirefu.

"Alikuwa akiigiza kutokewa na miujiza mbele ya madhabahu, kuna dili alilipata lakini ikawa wanatakiwa watu watatu aliniunganisha na mimi, nilianza kwa kushtuka lakini aliponieleza nikazoea mpaka sasa nazunguka nyumba za Ibada tofauti," alidai mwananchi huyo.

'Muumini' huyo ambaye hapa tunampa jina la XXX anasimulia; "Mara ya kwanza nilitakiwa kufanya shaba mbele ya madhabahu kujifanya napandwa na mapepo, nilifanya hivyo nikavuta changu nikaondoka, baada ya hapo nimekuwa nizunguka na bosi kwenye maeneo tofauti ikiwemo mikoani."

XXX anaeleza kuna hatua inafika kiongozi wa kanisa hilo anakodisha mali za thamani ikiwemo magari kisha kuwapa wacheza Shaba ili wakaoneshe madhabahuni kuwa wamezipata baada ya kuombewa kanisani hapo, ilihali wakijua ni uongo.

"Wakati mwingine nafanya shaba nikionesha Maisha yangu yamekuwa ya mafanikio baada ya kuanza kusali kanisani kwa 'Mtume', naweza kutafutiwa mpaka gari ili nikaigize kuwa nimenunua gari baada ya biashara zangu kuanza kwenda vizuri.

“Ikiwa ni baada ya kutumia 'mafuta ya upako au maji ya baraka', kwa kuwa wanakuwepo watu wengi ambao biashara zao zinasuasua kwahiyo Shaba ya aina hiyo inakuwa rahisi kuamini," alidai muumini.

Malipo ni 'mazuri', si rahisi kushtukiwa
"Malipo ni makubaliano, binafsi nalipwa Sh. 150,000 hadi 300,000 kama nasafirishwa kwenda mkoani. Kuna shaba unazifanya zinaweza kuhatarisha usalama wako hapo lazima akuongezee dau.

"Ni vigumu shaba kugundulika maana inafanywa kwa uhalisia kiasi kwamba unakuwa unabaki bila mashaka hata ukiwa msomi shaba inavyofanywa lazima uamini."

Mlinzi wa Kanisa afichua
Mlinzi wa kanisa hilo maarufu lenye makao yake Kawe Jijini Dar es Salaam anafunguka kuwa wacheza Shaba wa kanisa hilo hutafutwa kwa siri sana.

Anasema "Binafsi niligundua baada ya muda mrefu kupita nikiwa hapa (Kanisani), tulikuwa tunawashikilia kwa nguvu wanapofanya maigizo ya kuzimia, baadaye unawaona wapo fiti wanachukua mzigo wao.

“Siku hizi nimewazoea, wapo wanaoigiza kukosa Watoto, mwingine anakuja na Watoto wasio wake pia wapo wanaoigiza kupata mali na utajiri.

"Walinzi wengi tumeshashtukia mchezo huo, sema ndio hivyo utafanyaje unalinda kibarua hata wenzako ukiwaona husemi.”

Watumishi waandamizi hula kiapo
Watumishi waandamizi ndani ya kanisa hilo (la Kawe), hulishwa kiapo cha kutunza siri za kiongozi wao, hivyo huwa ni vigumu kukupa ushirikiano pindi mtu anapotaka kufahamu upande wake wa pili. Aidha, Makanisa mengi yamewaajiri ndugu na jamaa zao wa karibu katika kuhakikisha kuna kutunza siri miongoni mwao.

Kanisa lilipo Kivule jijini Dar
Binti aliyejitambulisha kwetu kuwa anaishi Sinza lakini ni muumini Kanisa lililopo Kivule anaeleza alipewa fedha ili atoe shuhuda ya uongo kwamba amepata kazi baada ya kuhitimu chuo kikuu, wakati si kweli.

"Nimehitimu Chuo cha IFM kwa sasa najihusisha na biashara ya nguo za watoto na wadada. Mara ya kwanza nilifika kanisani kwa 'Mtume' anisaidie kuniombea nipate kazi na Mwanaume wa kufunga naye ndoa.

“Nilienda siku ambayo sio ya Ibada nikakutana na Mchungaji akanielekeza niende Jumapili hiyo siku nikaombewa lakini baada ya hapo yule mchungaji alinifuata akaniambia kuna dili la hela, ndiyo akanieleza wiki mbili mbele niigize kuwa nimepata kazi na Mume wa kunioa."

"Aliniambia nitapewa sh 200,000/= nikiweza kufanya hivyo lakini akinisisitiza niwe msiri. Ilipofika hiyo siku nilikuwa nimeshapewa maelekezo namna ya kuzungumza nikafika pale kwenye madhabau nikatoa ushuhuda wakanipa changu jioni ndio ikawa mwanzo wa kufanya 'Shaba', ndivyo wengi wanaita.

"Nimeenda mpaka mikoani kwa nyakati tofauti kwa ajili ya Shaba. Napangiwa sehemu ya kukaa kwenye siku tunazokuwa mikoani pesa ya kula na posho inakuwepo ukimaliza kazi. Kiukweli, shaba imenisukuma kimaisha."

Kanisa jingine lililopo Kimara, Dar
Mhudumu mmoja kwa siri atatufahamisha kuwa kanisa hilo huwapanga watu kwa ajili ya kutoa shuhuda za uongo kwenye vyombo vya habari, hususani kwenye runinga na redio.

Anasimulia "Wanakuja watu wengi sana lakini miujiza wala sio ya kweli. Kuna watu wanapangwa na watu wa habari ambao wamepewa jukumu hilo kwa kushirikiana na mhudumu maalum. Siku za ibada wanakuwa na watu wao, wakishawaandaa ndio wanakuja kuhojiwa ‘live’ wanatoa ushuhuda ambao unavutia wasikilizaji wengi.”

Uchunguzi wetu unaonesha kupitia baadhi ya vyombo vya habari vinavyomilikiwa na wakuu wa makanisa hayo vimekuwa vikitumika katika propaganda za kuvuta ‘wateja’.

Uchunguzi huu pia umefanywa katika kipindi ambapo makanisa kongwe (Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) na Kanisa Katoliki), yamekuwa yakiwasihi waumini wao kuacha 'kutangatanga' katika makanisa yanayowavuta kwa kigezo cha kusaka miujiza.

Michezo ya vipindi vya redio
Chanzo kingine kinaeleza “Kwenye vipindi vya redio napo tumefanya maigizo sana. Sisi ndio tunapiga simu redioni Mchungaji au mtumishi anapokuwa studio, tunaigiza kutoa shida zenu na kuchangia fedha, tunabadili sauti na kushikilia ‘line’ ili wale wenye shida za ukweli wasipate mawasiliano.

“Tunachokifanya hapo mtu akiwa anasikiliza ni rahisi kushawishika kuwa kiongozi huyo wa Kanisa anafanya maombi ya kweli na watu wanachangia kweli sadaka kubwa. Michezo hiyo ipo sana kwenye redio za makanisa haya ya kiroho na mpaka sasa bado inaendelea.”

Itaendelea sehemu ya pili...

Habari zinazofanana: Wawili akiwemo mchungaji washikiliwa na polisi kwa kulaghai mchawi kadondoka na ungo kanisani kwenye mkesha
Hizi dini hizi zikiendelea mpaka 2030 tutakuwa maskini sana
 
Yesu Kristo ( Masihi ), katika enzi zake alipingwa pia, ikiwamo yeye kama yeye na hata miujiza aliyokuwa anafanya wakamuambia anafanya kwa nguvu za belzababu.. Hata manabii walio kuwa kabla yake walipigwa sana pia na wengine hata kuuwawa... Ije kwa nyakati hizi ? ambapo Paul Apostle anasema .....

Neno la msalaba kwao wanaopotea ni upuzi, bali kwetu sisi tunaookolewa ni nguvu ya Mungu. Mungu alipenda kuwaokoa waaminio kwa upuzi wa lile neno linalohubiriwa. Kwa sababu upumbavu wa Mungu una hekima zaidi ya wanadamu, na udhaifu wa Mungu una nguvu zaidi ya wanadamu.
 
Back
Top Bottom