Uchungu wa uwaziri ni mkubwa kuliko uvamizi wa vyombo vya habari

Hoja nyembamba sana hiyo kaka,Mwakyembe ndiye aliyesema report ya Nape ina mapungu ataishughulikia hiyo saga,kwa kuwa mvamizi ni mtumishi wa umma aliyeteuliwa na rais na kwa kuwa waziri mwenye dhamana na vyombo hivyo vya habari anawajibu wa kujua kadhia hiyo ni sahihi bunge kuhoji kwa kuwa ndicho chombo pekee chenye dhamana ya kuisimamia na kuishauri serikali.
Tufanye mwakyembe ameshindwa kushughulikia hilo la uvamizi sasa pelekeni mahakamani.
 
Keny="Dr Akili, post: 20787966, member: 52338"]Ndiyo, si kila mtu ameona jinsi serikali ya Kenya na ya Tanzania zilivyonywea katika suala la Tanzania kupeleka madaktari Kenya baada ya madaktari wa Kenya kulifikisha suala hilo mahakamani? Wangelilipeleka bungeni nothing would have changed. Suala la Makonda kuwadhalilisha watu kwa kuwatuhumu kufanya biashara za madawa ya kulevya bila kuwa na ushahidi, kuteka Clouds TV na kuwa na vyeti feki lingekuwa limepelekwa mahakamani sasa hivi lingalikuwa limeshaisha.[/QUOTE]
Kenya wa
Ndiyo, si kila mtu ameona jinsi serikali ya Kenya na ya Tanzania zilivyonywea katika suala la Tanzania kupeleka madaktari Kenya baada ya madaktari wa Kenya kulifikisha suala hilo mahakamani? Wangelilipeleka bungeni nothing would have changed. Suala la Makonda kuwadhalilisha watu kwa kuwatuhumu kufanya biashara za madawa ya kulevya bila kuwa na ushahidi, kuteka Clouds TV na kuwa na vyeti feki lingekuwa limepelekwa mahakamani sasa hivi lingalikuwa limeshaisha.
Kenya ni waumini wa utawala wa sheria,lakini pamoja na hayo mbona mbunge lina haki ya kujuwa,ilikishajuwa litapendekeza hatua stahiki,clouds wao ni utashi wao kuamua kwenda au kutokwenda mahakamani.
 
Kwa kuwa Mwakyembe ana ushahidi kuhusu ufisadi uliofanywa Lowasa na kwa kuwa serikali ya awamu ya tano ilishaunda mahakama ya mafisadi ni kwa nini basi chini ya wizara ya sheria iliyokuwa inaongozwa na Mwaki ilishindwa kumfikisha Lowasa mahakamani,tuache siasa kwenye mambo ya msingi, tunataka kwanza taarifa ya Bashite
 
Why are you one sided like a panga?
Kwanini Mkuu wa Mkoa alienda pale in the first place?
Kwanini alifanya Clouds kama kijiwe?
Mambo yapi Clouds walizungumza na Makonda ambayo sisi hatujui?
Kwanini Makonda aliogozana na Vyombo vya Usalma tena wenye Siraha kwenye Studio ya Clouds.
Kitu gani halisi kilimsukuma Nape kuunda tume ?Bila kuwauliza wakubwa wake kwanza?
Open your eyes and stay focused on big picture.

It is a shame that i am being asked to open my eyes by you Mkuu....Who are you asking all the questions below??
 
Nilitaka kushangaa Mwakyembe kusemea sakata la uvamizi wa kituo cha radio clouds kwa kufuata taarifa ya mtangulizi wake ilihali jambo hilo hilo ndilo lililomchomoa mtangulizi wake. Uwaziri kwake ni zaidi ya usalama wa vyombo vya habari,kuleta hoja kuhusu Lowasa ni kukimbia kutolea ufafanuzi wa jambo lililoko mezani kwake na hii ndiyo double standard tunayoizungumzia.

Ukosefu wa weredi katika kushughulikia masuala ya kitaifa utaendelea kupungua siku hadi siku iwapo tutataka kufunika kombe kwa lengo la kuleta mjadala uliokwisha pita,kamati yake Mwakiyembe ilipaswa kulibana bunge kushindwa kumfikisha Lowasa mahakamani kutokana na taarifa ya kamati,haileti mantinki kutuambia leo wabunge wa chadema kuleta jambo hilo wakati tunataka kujua kwa nini taarifa kuhusiana na Makonda umeikalia hutaki kuiweka wazi?

Huoni ukimya huo ndiyo chachu ya uvamizi wa studio ya Tong we recording kwa kuwa tukio la clouds lilikosa ufuatiliaji. Tunataka kujua lini tukio hili taarifa zake zitawekwa wazi.

Kuibua suala lililokwishapita na kinyume cha kanuni ya 64 ya bunge kujadili suala lililokwisha kwa lengo la kufunikwa kwa hoja ya uvamizi wa clouds si tu kunaonyesha utendaji mbovu kwa serikali bali kunadhalilisha taaluma ya waziri na mwalimu wa sheria kushindwa kuitumia elimu yake kwa faida ya umma.

Utamaduni huu wa kukwepa hoja kwa kuibua hoja kunajenga udhaifu mkubwa wa ujenzi wa hoja hususani tunapokutana na wenzetu mbalimbali ndani ya shirikisho na kuonekana wasindikizaji.

Pia kunaibua jamii ya watu wasioguswa(untouchable) ndani ya taifa linaloamini katika usawa. Makonda amekuwa nani mpaka waziri atumie nguvu kubwa kumlinda kwa hoja dhaifu,ikiwa Nape alithubutu na kumkabidhi taarifa ile alishindwa nini kuifanyia kazi ilhali taarifa zinasonyesha Makonda kuikimbia kamati ya wizara yenye dhamana.

Tuna safari ndefu kufikia utawala bora ikiwa serikali ndiye mtetezi wa maovu,hapo ndipo udhaifu unapokuwa mkubwa wa kudhibiti uhalifu wakati upande mwingine inatetea uhalifu huo huo,tuache maigizo kama tuna nia ya dhati na Tanzania yetu.
Hoja mubashara. Kuibua hoja kwa ajili ya kufunika hoja.
Ndiyo maana Makonda kaibua hoja ya madawa ya kulevya, haijafika popote ikaibuliwa hoja ya vyeti na Clouds kuizima hoja ya madawa.
Kwa watu wenye weledi wanaowaza kama wewe wanaona hoja ya vyeti na Clouds iliyoibuka kufunika hoja ya madawa ni kekele za kutengeneza ili kupoza hoja iliyokuwa mezani.
 
Back
Top Bottom