sammosses
JF-Expert Member
- Jan 24, 2011
- 1,685
- 1,111
Nilitaka kushangaa Mwakyembe kusemea sakata la uvamizi wa kituo cha radio clouds kwa kufuata taarifa ya mtangulizi wake ilihali jambo hilo hilo ndilo lililomchomoa mtangulizi wake. Uwaziri kwake ni zaidi ya usalama wa vyombo vya habari,kuleta hoja kuhusu Lowasa ni kukimbia kutolea ufafanuzi wa jambo lililoko mezani kwake na hii ndiyo double standard tunayoizungumzia.
Ukosefu wa weredi katika kushughulikia masuala ya kitaifa utaendelea kupungua siku hadi siku iwapo tutataka kufunika kombe kwa lengo la kuleta mjadala uliokwisha pita,kamati yake Mwakiyembe ilipaswa kulibana bunge kushindwa kumfikisha Lowasa mahakamani kutokana na taarifa ya kamati,haileti mantinki kutuambia leo wabunge wa chadema kuleta jambo hilo wakati tunataka kujua kwa nini taarifa kuhusiana na Makonda umeikalia hutaki kuiweka wazi?
Huoni ukimya huo ndiyo chachu ya uvamizi wa studio ya Tong we recording kwa kuwa tukio la clouds lilikosa ufuatiliaji. Tunataka kujua lini tukio hili taarifa zake zitawekwa wazi.
Kuibua suala lililokwishapita na kinyume cha kanuni ya 64 ya bunge kujadili suala lililokwisha kwa lengo la kufunikwa kwa hoja ya uvamizi wa clouds si tu kunaonyesha utendaji mbovu kwa serikali bali kunadhalilisha taaluma ya waziri na mwalimu wa sheria kushindwa kuitumia elimu yake kwa faida ya umma.
Utamaduni huu wa kukwepa hoja kwa kuibua hoja kunajenga udhaifu mkubwa wa ujenzi wa hoja hususani tunapokutana na wenzetu mbalimbali ndani ya shirikisho na kuonekana wasindikizaji.
Pia kunaibua jamii ya watu wasioguswa(untouchable) ndani ya taifa linaloamini katika usawa. Makonda amekuwa nani mpaka waziri atumie nguvu kubwa kumlinda kwa hoja dhaifu,ikiwa Nape alithubutu na kumkabidhi taarifa ile alishindwa nini kuifanyia kazi ilhali taarifa zinasonyesha Makonda kuikimbia kamati ya wizara yenye dhamana.
Tuna safari ndefu kufikia utawala bora ikiwa serikali ndiye mtetezi wa maovu,hapo ndipo udhaifu unapokuwa mkubwa wa kudhibiti uhalifu wakati upande mwingine inatetea uhalifu huo huo,tuache maigizo kama tuna nia ya dhati na Tanzania yetu.