Uchungu wa uwaziri ni mkubwa kuliko uvamizi wa vyombo vya habari | Page 2 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uchungu wa uwaziri ni mkubwa kuliko uvamizi wa vyombo vya habari

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sammosses, Apr 21, 2017.

 1. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #1
  Apr 21, 2017
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,242
  Likes Received: 172
  Trophy Points: 160
  Nilitaka kushangaa Mwakyembe kusemea sakata la uvamizi wa kituo cha radio clouds kwa kufuata taarifa ya mtangulizi wake ilihali jambo hilo hilo ndilo lililomchomoa mtangulizi wake. Uwaziri kwake ni zaidi ya usalama wa vyombo vya habari,kuleta hoja kuhusu Lowasa ni kukimbia kutolea ufafanuzi wa jambo lililoko mezani kwake na hii ndiyo double standard tunayoizungumzia.

  Ukosefu wa weredi katika kushughulikia masuala ya kitaifa utaendelea kupungua siku hadi siku iwapo tutataka kufunika kombe kwa lengo la kuleta mjadala uliokwisha pita,kamati yake Mwakiyembe ilipaswa kulibana bunge kushindwa kumfikisha Lowasa mahakamani kutokana na taarifa ya kamati,haileti mantinki kutuambia leo wabunge wa chadema kuleta jambo hilo wakati tunataka kujua kwa nini taarifa kuhusiana na Makonda umeikalia hutaki kuiweka wazi?

  Huoni ukimya huo ndiyo chachu ya uvamizi wa studio ya Tong we recording kwa kuwa tukio la clouds lilikosa ufuatiliaji. Tunataka kujua lini tukio hili taarifa zake zitawekwa wazi.

  Kuibua suala lililokwishapita na kinyume cha kanuni ya 64 ya bunge kujadili suala lililokwisha kwa lengo la kufunikwa kwa hoja ya uvamizi wa clouds si tu kunaonyesha utendaji mbovu kwa serikali bali kunadhalilisha taaluma ya waziri na mwalimu wa sheria kushindwa kuitumia elimu yake kwa faida ya umma.

  Utamaduni huu wa kukwepa hoja kwa kuibua hoja kunajenga udhaifu mkubwa wa ujenzi wa hoja hususani tunapokutana na wenzetu mbalimbali ndani ya shirikisho na kuonekana wasindikizaji.

  Pia kunaibua jamii ya watu wasioguswa(untouchable) ndani ya taifa linaloamini katika usawa. Makonda amekuwa nani mpaka waziri atumie nguvu kubwa kumlinda kwa hoja dhaifu,ikiwa Nape alithubutu na kumkabidhi taarifa ile alishindwa nini kuifanyia kazi ilhali taarifa zinasonyesha Makonda kuikimbia kamati ya wizara yenye dhamana.

  Tuna safari ndefu kufikia utawala bora ikiwa serikali ndiye mtetezi wa maovu,hapo ndipo udhaifu unapokuwa mkubwa wa kudhibiti uhalifu wakati upande mwingine inatetea uhalifu huo huo,tuache maigizo kama tuna nia ya dhati na Tanzania yetu.
   
 2. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #21
  Apr 21, 2017
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,242
  Likes Received: 172
  Trophy Points: 160
  Tusihamishe mada,tujikite kwenye hoja
   
 3. habari ya hapa

  habari ya hapa JF-Expert Member

  #22
  Apr 21, 2017
  Joined: Dec 20, 2012
  Messages: 12,032
  Likes Received: 7,241
  Trophy Points: 280
  Kwani wewe unafikiria nini

  Akili zangu hazina akili

  Waweza niita kilaza
   
 4. Mwene chungu

  Mwene chungu JF-Expert Member

  #23
  Apr 21, 2017
  Joined: Nov 12, 2016
  Messages: 922
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 180
  Umejiita Dr akili lakini huna Akili hata kidogo.

  Eti kutaka kubisha kuwa Makonda hakuvamia clouds.Mahakamani clouds walishaenda lakin kwa sbab ya urasimu na kulinagana na mazoea ya watanzania hakuna hakimu anaeweza kuhukumu kesi kw kufuata sheria kwa mteule wa rais ambae rais ameshaonesha mahaba ya kipekee kwake.

  Na ni bunge pekee ambalo linaweza kuhoj na kuja na msimamo wa kipekee ukizingatia kuwa jukumu la bunge ni pamoja na kuisimami serkali..
   
 5. kmbwembwe

  kmbwembwe JF-Expert Member

  #24
  Apr 21, 2017
  Joined: Aug 16, 2012
  Messages: 6,458
  Likes Received: 1,415
  Trophy Points: 280
  kwani clouds kulikua na uvamizi au usanii tu uliyopangwa na wauza ngada kwa madhumuni ya kumdhalilisha makonda. nape mwenyewe huenda alihusika na mpango huo mchafu. wanaita uvamizi wakati hizo clip zao zenyewe hakuna hata moja inaonyesha kutumika nguvu au intimidation of any type. nyie nyumbu na wauza ngada ogopeni mungu.
   
 6. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #25
  Apr 21, 2017
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,242
  Likes Received: 172
  Trophy Points: 160
  Clip inaonyesha makonda na askari,kama ni maigizo kumdhoofisha makonda basi naye anahusika,footage ya CCTV inamuonyesha akiwa na kikosi chake
   
 7. S

  Sexless JF-Expert Member

  #26
  Apr 21, 2017
  Joined: Mar 11, 2017
  Messages: 3,537
  Likes Received: 5,439
  Trophy Points: 280
  Mkuu usijaribu kutuaminisha kuwa upupu ni poda. Bashite alivamia kituo cha clouds na kwa kufanya hivyo alitenda kosa la jinai. Na hakuna namna nyingine bali kuwajibishwa. Kumbuka pia hana vyeti, anatumia vyeti vya Makonda.
   
 8. D

  Dr Akili JF-Expert Member

  #27
  Apr 21, 2017
  Joined: Aug 21, 2011
  Messages: 2,606
  Likes Received: 1,808
  Trophy Points: 280
  Na unaamini kuwa bunge hilo ambalo 75% ya wabunge wake wanatoka CCM litafanya hicho unachotaka?
   
 9. gollocko

  gollocko JF-Expert Member

  #28
  Apr 21, 2017
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 2,886
  Likes Received: 1,654
  Trophy Points: 280
  Dr. Ulisharudishwa internship?
   
 10. sblandes

  sblandes JF-Expert Member

  #29
  Apr 21, 2017
  Joined: Apr 25, 2010
  Messages: 2,714
  Likes Received: 988
  Trophy Points: 280
  Mbona unatoka nje ya msitari,the cardinal rule of engagement is to call a spade is a spade and not a big spoon.
  Haitaki kuota meno kujua there was something very fishy between Clouds and Makonda in the beginning,na wala hamkujiuliza,misifa aliopewa Clouds na Makonda,hadi Raisi wa Jamhuri.
  Wakati baadhi vyombo vya habari vinazungumzia utata wa elimu ya Makonda,Clouds alikuwa kimya kabisa.
  Ni ukweli usiopindika kuwa Clouds aliibuka ghafla kwa mambo may be personal,may be alirushwa biashara au alitaka ku Blackmail the state ndio akapata mkongoto!
  Sasa ninyi mna judge outcone bila kujua the content?
  Hivi huo ndio mtaji wa kusogelea QC?
   
 11. S

  Sexless JF-Expert Member

  #30
  Apr 21, 2017
  Joined: Mar 11, 2017
  Messages: 3,537
  Likes Received: 5,439
  Trophy Points: 280
  Mmh! Hapa mkuu unafanya ubashiri tu ya kwamba huenda kulikuwa na jambo baya (something fishy) nyuma ya pazia. Nilitegemea utuwekee hadharani hilo jambo baya. Kwa bahati mbaya hata wewe hulijui hilo jambo baya.

  Kwa watanzania tulio wengi tunamhukumu makonda kwa yale yalioonekana kwa macho ya nyama. Wewe unataka tuichukue dhana ya nyuma ya pazia ndiyo itumike kuhalalisha uvamizi wa makonda pale clouds. Hapana mkuuu. Kwani serikali inaogopa nn kulitaja jambo lenyewe? Ikiwa iliwataja wauza ngada hadharani inashindwa nn kuelezea alichokifuata makonda clouds?
   
 12. sblandes

  sblandes JF-Expert Member

  #31
  Apr 21, 2017
  Joined: Apr 25, 2010
  Messages: 2,714
  Likes Received: 988
  Trophy Points: 280
  Kitu usichojua ni sawa na giza nene.
  Acha kupoteza manhour tufanya kazi zenye tija.Mambo mengine tuwachie wenye madaraka wayafanyie kazi.Every point counts
   
 13. mwanamichakato

  mwanamichakato JF-Expert Member

  #32
  Apr 21, 2017
  Joined: Mar 20, 2015
  Messages: 700
  Likes Received: 407
  Trophy Points: 80
  Inawezekana kweli sakata la IPTL/PAP Escrow kurudi tena bungeni?
  Thats would be best of the best Bunge session ever..
  RIP Deo F.
   
 14. k

  kabombe JF-Expert Member

  #33
  Apr 21, 2017
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 16,962
  Likes Received: 9,774
  Trophy Points: 280
  Huna jipya
   
 15. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #34
  Apr 21, 2017
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,242
  Likes Received: 172
  Trophy Points: 160
  Tuna tumia haki yetu ya kikatiba kuhoji,huwezi kaa pembeni kuwaachia wenye madaraka,tukisoma katiba ya JM ya 1977 utaona kuwa madaraka na mamlaka ya serikali yatatoka kwa wananchi na msingi mkuu wa serikali ni ustawi kwa wananchi wake,tukikaa kimya hatuoni hata huo ustawi uliozungumzwa kwenye katiba utafanywa kwa utashi wa mtu,ndiyo maana tumewaweka wawakilishi wetu bungeni kutusemea na kuisimamia serikali.
   
 16. K

  Kohelethi JF-Expert Member

  #35
  Apr 21, 2017
  Joined: Mar 8, 2013
  Messages: 1,111
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  sasa mbona ya fisadi lowasa zezeta mwezio kasema iletwe hoja bungeni na si kumpeleka mahakamani. fisadi kashasema mwenye ushahidi ampeleke mahakamani mwambie zezeta aliyesema ushahidi upo usio na shaka ampeleke lowasa mahakamani. badala ya kumpeleka fisadi mahakamani mnatuletea UMALAYA WA KISIASA TU.
   
 17. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #36
  Apr 21, 2017
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,242
  Likes Received: 172
  Trophy Points: 160
  Ukisikiliza contents za Mwaki utaona kuna personal inferiority,ndiyo maana hata wakati ana wasalimisha report yake alisema"kuna mambo mengine hatujayaweka humu,tukiyaweka serikali itaanguka"kwa hoja kama hiyo unategemea nini, kamati ilishauri Lowasa ajipime aone,alichokifanya Lowasa ni political responsibility.
   
 18. Saju b

  Saju b JF-Expert Member

  #37
  Apr 21, 2017
  Joined: Jul 10, 2011
  Messages: 2,505
  Likes Received: 2,015
  Trophy Points: 280
  Ni kweli kabisa kwanza Makonda hana kinga ya kutoshtakiwa kama aliyonayo rais sasa iweje malalamiko yasipelekwe mahakaman bali bungeni? Wanatafuta sympath
   
 19. commonmwananchi

  commonmwananchi JF-Expert Member

  #38
  Apr 21, 2017
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 2,331
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Mtahangaika sana maana chadema mlipomkaribisha ngamia kwenye hema hamkujua madhara yake bali mlifikiri ni short cut to magogoni.

  Mkalewa na mafuriko bandia,misaada ya kujenga misikiti na makanisa.

  Ugeni rasmi kila aina ya fund raising na misa za TB joshua.

  Hadi mkamuona mpiganaji wa kweli mzee Dk wilbroad slaa kama si lolote na kumtupilia mbali.

  Sasa mnalazimishwa kumsafisha kwa nguvu zile zile mlizotumia kumchafua.

  Hadi kina Yericko Nyerere nao wanalamba matapishi yao.

  Mnadai demokrasia gani wakati ndani ya chagadema kwenyewe hakuna hiyo demokrasia bali muamuzi ni mwenyekiti mbowe tu na ukibusha wewe ni out......

  Kweli JPM kawashika pabaya,wakati mnahangaika kusafishana humu mitandaoni yeye anazidi kutimiza ahadi zake za ilani ya uchaguzi kwa wananchi.
   
 20. commonmwananchi

  commonmwananchi JF-Expert Member

  #39
  Apr 21, 2017
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 2,331
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Nendeni chagadema mumwambie mbowe airudishe ile katiba iliyokuwa na ukomo wa kipindi cha uenyekiti,pia atimize demokrasia kwa kuwaachia wanachama kufanya maamuzi ndani ya chama chenu na sio zidumu fikra za mwenyekiti mbowe.

  Kuteua viti maalumu yeye!
  Kuteua mgombea urais yeye!
  Kuteua wabunge EALA yeye!
  Kuteua wagombea uenyekiti kanda za chama yeye!

  Nk n.k n.k.........loh nyinyi sera imebaki clouds,makonda,na kumsafisha Lowassa baasi haya bhana
   
 21. D

  Dr Akili JF-Expert Member

  #40
  Apr 21, 2017
  Joined: Aug 21, 2011
  Messages: 2,606
  Likes Received: 1,808
  Trophy Points: 280
  Ndiyo, si kila mtu ameona jinsi serikali ya Kenya na ya Tanzania zilivyonywea katika suala la Tanzania kupeleka madaktari Kenya baada ya madaktari wa Kenya kulifikisha suala hilo mahakamani? Wangelilipeleka bungeni nothing would have changed. Suala la Makonda kuwadhalilisha watu kwa kuwatuhumu kufanya biashara za madawa ya kulevya bila kuwa na ushahidi, kuteka Clouds TV na kuwa na vyeti feki lingekuwa limepelekwa mahakamani sasa hivi lingalikuwa limeshaisha.
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...