bmbalamwezi
JF-Expert Member
- Mar 12, 2015
- 788
- 195
Ni hali ya kusikitisha sana kwa mtu amnayefahamu fika siasa za Tanzania kufanya maamuzi anayoendelea kuyafanya. Urais wa Tanzania hauji kirahisi hivi kwa kudhani unapendwa au unaungwa mkonona watu wengi. Mzee huyu mimi namshauri hata fomu ya kugombea urais kupitia CDM-UKAWA asichukue kwani atajiongezea frustrations za bure. Huyu mzee angetulia na kula pesa yake na kumalizia muda wake kwa amani. Kama alivyosema kuwa CCM si Baba yake wala Mamam yake,na urais si Baba yake wala mama yake aachane nao. Sasa akishindwa atasemaje. Atasema ameonewa kama anavyodai sasa. Yeye ni nani wagombea walikuwa 42 aliyetakiwa ni mmoja. Kama yeye anadai ameonewa je wale wengine 40 watasemaje.Je angechaguliwa yeye angesimama jukwaani na kusema kuwa wenzake wameonewa! Mzee mwenzangu nakushauri uwekama akina Membe,Mwandosya na wengine wengi ambao wametulia na kuachana na siasa. Huko ulikohamia sio kwamba wanakutaka ikla wanataka mpunga wako tuu. Mzee nakushauri usome alama za nyakati ili umalizie uzee wako vizuri.Ni kweli wewe ni ulikuwa kiongozi mzuri lakini wakati wako ulishaisha au ulishaexpire. Kma unamwamini Mungu ambaye umekuwa ukimtaja na kusema kuwa wewe ni mkristo huna visasi muulize kama utapata urais. Atakwambia wazi wazi. Mwechie aliyechaguliwa kihalali aongoze jahazi hili. Huko ulikokimbilia tayari wameishafarakana kwa ujio wako. Je unadhani hiyo ni ishara nzuri Mzee mwenzangu. Nakutakia uamzimwema kama ulivyosema huwezi kuihama CCM na muda mfupi ukahama,sasa achana na kugombea ili uzidi kuheshimika. Kila la kheri Mzee.