Uchumi wa fremu, Framenomics

Akilindogosana

JF-Expert Member
Jan 12, 2020
2,876
8,697
Uchumi wa fremu (Framenomics, Frame + Economics=Framenomics), ndio uchumi halisi wa nchi hii. Uchumi wa kuagiza vitu na kuviuza. Kuimport na kuuza. Hakuna uzalishaji wa bidhaa au huduma wala hakuna exports.

Changamoto ni nyingi sana, mipango, ardhi, mtaji, sheria za nchi, na umeme halafu Umeme wenyewe magumashi, unakatikakatika. Nchi za asia huko nchi ina megawatt 50,000 mpaka megawatt laki mbili na zaidi.

Huu uchumi wa fremu, zikichukuliwa taarifa inaonyesha kiuchumi tuko vizuri na tunapaaaaaaa, ILA KIUHALISIA HALI NI NGUMU.

Huu uchumi wa fremu, hauwezi kuongeza ajira, ila unaua ajira kabisa, maana unapoagiza na kuagiza ni sawa na kuexport ajira nje. Unafaidisha sekta nzima ya nchi nyingine na viwanda vya nchi nyingine.

Huu uchumi wa fremu, wa kuagiza agiza ushindani ukizidi unaleta migogoro kati ya mtu na mtu, mfano umeagiza bidhaa A unaiuza unaongeza mzigo wa bidhaa A, baadae unaona majirani woote wa hiyohiyo bidhaa A, baadae mji mzima una bidhaa A. Baada ya hapo mzigo utadoda, unaona watu wabaya 🤣🤣 kama unaroho nyepesi unaenda kwa mganga 🤣

Huu uchumi wa fremu hakuna sehemu tutafika, tutaishia kuagiza na kuagiza na kuagiza na kuagiza zaidi.

Wataalam wa uchumi na wataalam wengine mbalimbali mtaongezea nyama.
 
Back
Top Bottom