mwana wa Tanzania
Member
- Nov 27, 2019
- 35
- 145
Anaandika John Sm Mgejwa
Kuna kipindi nchini Kenya hasa mwaka 2009/10 kwenye mapato yaliyokuwa yanakusanywa kwa mwaka, 47.3% ya Fedha zilizokusanywa zilikuwa zinatumika kulipa mishahara ya watumishi, kiwango hiki lilikuwa juu ya kile Cha kimataifa ambacho ni 35% ya makusanyo yote. Hii ina maana kuwa 52.7% ya makusanyo yote ndo ilikwenda kwenye Maendeleo na matumizi mengine ya serikali ya Kenya.https://www.ieakenya.or.ke/downloads.php…
Katika mwaka wa fedha 2011/12 kiwango hicho kiliongezeka na kufikia 48.1% na kufikia mwaka 2012/2013 kiwango hicho kiliongezeka hadi 55% ya makusanyo yote ya mwaka huo yaani 45% zikisalia kwa ajili ya maendeleo na matumizi mengine mengine ya serikali.
Kenya ilikuwa na watumishi wa umma 700,000 kwa 2014 wakati taifa hilo lina watu zaidi ya Milioni 40. Hii Ina maana kwamba asilimia 55% ya mapato yaliyokusanywa kwa mwaka yalikuwa yanakwenda kwa watumishi ambao hawafiki hata 1% ya watu milioni 40 Kutokana na mishahara mikubwa na marupurupu ya kufa mtu😃😃. Hapo ina maana kuwa 45% ndo ilikuwa inakwenda kwenye Maendeleo ya watu wanaofikia 99.51% ukiondoa watumishi ambao ni 0.48%. Maendeleo ya watu wengi zaidi ambao siyo watumishi yanakuwa chini kwa sababu lazima tu kiasi kinachoweza kwenda katika miradi ya Maendeleo kama hospital, shule nk ni kidogo.
Suluhisho la tatizo hili ambalo kwa Tanzania nitafuatilia pia kujua hali ikoje, ni kutambua kuwa kupandisha mishahara ni kuwapa moyo watumishi kwa muda mfupi tu, baada ya hapo wataendelea na maisha ya kuhangaika tu kwa sababu inflation au mfumko wa bei bado unakuwa pale pale na watumishi watakutana nao wakiwa na mishahara mikubwa, wataitumia hiyo mishahara na kujikuta ikiisha kwa haraka sababu ya mfumko wa bei.
Nimegusia kidogo Kenya ila point yangu kuu ni kumsapoti Magufuli 😋👇👇
Ukifuatilia utakuta kwamba bidhaa huwa zinapanda bei kwa SABABU mbili ambazo ni muhimu zaidi.
1. Gharama za uzalishaji na usafirishaji
2. Mzunguko mkubwa wa pesa mitaani.
Kwa kiongozi makini katika serikali yoyote duniani, anapaswa kuwa na mikakati ya kupunguza mfumko wa bei ili thamani ya pesa za watumishi hata kama ni kiasi kidogo ziwe na thamani kubwa katika ununuaji wa bidhaa.
Unawezaje kupunguza inflation katika nchi ili kuwabeba watumishi?
Unahakikisha unakuwa na Mipango ya kupunguza gharama za uzalishaji viwandani.
Unachopaswa kukifanya ni kutambua chanzo kikuu cha kupanda kwa gharama za uzalishaji nchini.
Chanzo kikuu cha kupanda kwa gharama za uzalishaji huwa ni nishati ya umeme, kisha malighafi na nguvu kazi. Wafanyakazi Tanzania na kwingineko duniani wanatumia sana bidhaa za viwandani iwe ni kutoka ndani au nje. Sisi tuongelee ndani.
Viwanda vingi Tanzania vinatumia gharama kubwa ya nishati ya umeme kwa sababu umeme uliopo haukidhi mahitaji ya viwanda, hali ambayo inaleta competition katika kile kiasi kilichopo cha umeme nchini.
Mataifa yaliyoendelea gharama za umeme ziko chini sana, kwa hiyo kwao gharama za uzalishaji ziko chini kwa kuwa wamewekeza zaidi kwenye umeme wa uhakika unaosaidia nishati katika viwanda. Gharama za usafirishaji kwa maana ya miundombinu zimeboreshwa hivyo kusafirisha bidhaa mbalimbali haihitaji kuhangaika kama katika mataifa yanayoendelea. Ndiyo maana mitumba inaweza kuwa na bei nafuu kuliko nguo mpya inayotoka kwenye kiwanda Cha Tanzania na kuuzwa Tanzania.
Kutokana na hilo kiongozi makini badala ya kuongeza mishahara atahakikisha kuwa anawekeza katika umeme ili baadaye afanikiwe kushusha bei za umeme kwenye viwanda vya bidhaa ambapo itapelekea kupunguza gharama za uzalishaji katika viwanda na tayari mnunuzi ambaye ni mfanyakazi, mkulima atanunua bidhaa kwa bei inayombeba, bei inayomfanya mshahara wake utosheleze nahitaji yake na kuweka akiba kidogo kidogo. Hii ndiyo maana John Magufuli anawekeza kwenye umeme, reli ya Kisasa, usafirishaji wa majini na anga na kupromote ujenzi wa viwanda.
Stieglers ni mwanzo mzuri!
Kuhusu ajira, tangu John P. Magufuli aingie kwenye Urais, ameajiri watanzania wengi, fuatilia National Bureau of Statistics utaona. Lakini Kutokana na uwekezaji unaofanyika ni kwa faida ya taifa kwa miaka 10 hadi 15 ijayo. Mafanikio ya uwekezaji huo kwenye ajira yataonwa na Rais wa Sasa, lakini zaidi Rais wa awamu ya sita ataona zaidi mafanikio ya uwekezaji huu kwa sababu mafanikio yake ni ya muda mrefu na hii ndiyo tabia halisi ya Maendeleo makubwa. Huwezi kuyaona kwa wakati huu ambapo yako katika process nzima lakini jipe muda wa miaka Kama 5 hadi 10 hivi.
Kumekuwa na Walimu wengi ambao hawajaajiriwa, lakini hili Mimi ninalionaje?
Ni kweli ajira za ualimu ni adimu, hasa masomo ya sanaa, Lakini tunafahamu kuwa watu hawa wanaweza kuajiriwa katika kazi zingine pia tofauti na ualimu, swali ni je, tunazo nafasi hizo za kuwaajiri hawa wahitimu wa digrii na shahada za elimu katika kazi ambazo siyo za ualimu?
Bado ni ngumu, kwa sababu idadi iliyopo ya waliohitimu ni kubwa kiasi kwamba watanzania wanaomiliki kampuni zenye uwezo wa kuajiri ni wachache sana, hawawezi ku manage hilo, Kwa upande wa serikali ni kwamba wanaweza wote kuajiriwa kuanzia mwaka 2015 hadi 2019 lakini watalipwa nini?
Bado vyanzo vya mapato ( tax base) ni ndogo kwa Tanzania Kutokana na ajira rasmi kuwa kidogo, kila mtanzania anaruhusiwa kuanzisha biashara za kuajiri wengine, tunapopata wafanyabiashara wengi hapo ndipo tunakuwa na nguvu ya kutatua changamoto za jamii Kama vile ukosefu wa ajira. Lakini sasa hawapo, kila mtu Yuko mtaani anasaka ajira au mwingine ameajiriwa!!
Suala la ajira ni mtambuka. Suala la ajira linaweza kutatuliwa endapo hizi juhudi zinazofanywa na Rais Magufuli za uwekezaji zitaungwa mkono na watanzania wote bila kujali vyama vyetu vya siasa. Kwa sababu uwekezaji huu ukikamilika utaleta mapato mengi zaidi na yatatumika kuwaajiri Vijana wa kitanzania katika nchi yao.
Employment opportunities hupatikana Kutokana na uwekezaji katika viwanda nk, hata hivyo huwezi kuwa na viwanda vingi bila kuwa na nishati ya umeme. Ndiyo maana unaona viongozi makini huwekeza katika Mambo hayo. Hapa Magufuli ni mfano hai, huku ndiko anakoelekea.
Suala la ajira za walimu, katika uongozi wa Kikwete ndani ya miaka 10 ya Kikwete, walimu wengi sana walizalishwa kwani katika kipindi hicho Serikali ililegeza masharti ya kwenda chuo kikuu, udahili ukaongezeka kwa kasi, wanafunzi wengi wakamaliza vyuo, Rais Kikwete aliajiri sana kuanzia miaka ya 2012+ kwani walimu wengi sana walikuwa wanazalishwa kutoka vyuoni.
Serikali katika awamu ya nne ilitoa kipaumbele kutoa Mikopo kwa watu wanaosoma degree ya elimu. Kadri siku zilivyokwenda walimu walikuwa wengi mno hasa masomo ya Sanaa hadi Rais Kikwete mwenywe akasema mwaka 2015 mwanzoni kwamba, tunakoelekea sasa walimu wa degree watapangwa kwenye vituo vya elimu ya msingi kwa sababu wamekuwa wengi sana na ndo dunia inakoelekea.
Utaratibu huo uliendelea watu wakawa wengi, Rais Kikwete kidogo sana alitaka kuahirisha kuajiri mwaka 2015 kwani ilikuwa kawaida waliomaliza vyuo mwaka mmoja nyuma kuajiriwa mwaka unaofuata tena mwezi wa March, lakini mwaka huo alitoa ajira mwezi wa May 2015, watu walisubiri ajira hadi kiwewe kikawajaa.
Sera kuhusu utoaji wa Mikopo iliyoanzishwa na serikali ya awamu ya nne haikuchungwa sana na wala hawakujua kuwa kungekuwa na mafuriko ya walimu nchini kiasi hiki hasa wa Sanaa.
Hivi sasa Shule za Sekondari zina ziada ya walimu zaidi ya maelfu ambao wapo mashuleni wanagawana vipindi kwenye SoMo moja tena darasa moja na wengine wamehamishiwa shule ya msingi!
Hata Kama ni wewe huwezi kuajiri wakati walimu unao wengi wa ziada mashuleni, haya ni matokeo ya sera mbovu za bodi ya mikopo ya miaka hiyo, ya kutoa Mikopo zaidi kwa walimu kitu ambacho wengi walivutwa na kujikuta wanaingia mtegoni.
Kwa Sasa tuwe tolerant tu ili serikali iwawekee mazingira ya walimu kuajiriwa kwenye shule za serikali.
Ni wakati Sasa wa kuamka kifikra, don't wait for employment, the government is preparing a conducive environment for you to survive in employment industry but this should not make you idle waiting for employment