Tanzania ya Viwanda ilikuwa ya Magufuli binafsi au Sera ya CCM?

Mzee wa Twitter

JF-Expert Member
Nov 5, 2023
1,272
2,027
Wadau ni bora kuuliza kuliko kukaa Kimya.

Awamu ya Tano ya Dikteta Magufuli wakati inaingia Madarakani kwa mbwembwe zote ilitutangazia kuwa Tanzania ni ya Viwanda na Waziri TAMISEMI Mh. Jaffo alizunguka nchi zima kuagiza kutenga viwanja 100 kila Mkoa kwa ajili ya Ujenzi wa Viwanda na kuifanya Tanzania ya Viwanda kuwa na Jumla ya Viwanda 100x26=2600.

Jambo la kushangaza hatukuwa kupewa mwendelezo wa nini kinaendelea licha ya Mikoa kutenga Viwanja vikubwa 100 kila Mkoa mpaka Magufuli alipofariki na ndio ukawa mwisho wa kusikia Tanzania ya Viwanda licha ya 3/4 ya Viongozi waliokuwepo kwenye Serikali ya Magufuli mpaka leo bado wapo.

Je, Tanzania ya Viwanda ilikuwa ni takwa Binafsi la Magufuli?

Je, Tanzania ya Viwanda ilikuwa Sera ya CCM? Kama ni Sera mbona hatuisikii tena? CCM imekwama wapi? Mbona Viwanja 100 vipo kila Mkoa?

Naamini viwanda 2600 vikijengwa vitapunguza Tatizo la Ajira kwa Vijana kila mkoa.
 
Back
Top Bottom