Vipi Watanzania tutaweza kuboresha uchumi wetu?

Gabriel Shewio

New Member
Apr 28, 2021
1
0
(Maoni yangu binafsi)
Maboresho ya uchumi ni wimbo wa kila awamu ya kiuongozi, aidha kila awamu huja na vipaumbele vyake. Mfano, katika kuboresha elimu, awamu ya 5 chini ya JPM ilikuja na mkakati wa kutoa elimu bure na hivyo kutoa ruzuku mashuleni zinazokaribia shilingi bilioni 18 kila mwezi, pamoja na maboresho hayo katika elimu bado wastani wa ufaulu umezidi kudidimia, tatizo la ukosefu wa ajira limeongezeka maradufu na utegemezi wa kiuchumi bado ni mkubwa sana.

Serikali itambue kwamba mfumo wa elimu wa Tanzania haumsaidii Mtanzania wa kawaida kuweza kukabiliana na changamoto za kimaisha, aidha mfumo huu haumuwezeshi Mtanzania wa kawaida kuweza kupata utaalamu stahiki wa kuweza kuajiriwa ama kujiajiri.

Mlolongo mrefu wa ngazi za kimasomo uliowekwa unafanya elimu kuwa ngumu mno na kukosa ubora unaostahiki, mathalani wastani wa wanafunzi wanaopata madaraja ya chini (div IV na div 0) kwa mtihani wa kidato cha nne ni zaidi ya asilimia 60% ya wanafunzi wote hivyo wanafunzi hao kwa kukosa utaalamu stahiki na pia kwa kukosa sifa za kujiendeleza kielimu wanaingia kwenye ajira zisizo rasmi ama kuishia mtaani, rasilimali hii kubwa ya taifa hupotea bila kutumika.

Maboresho ya elimu ya Tanzania yazingatie kupunguza muda wa kukaa darasani, kuingiza masomo ya ufundi kuwa ni lazima kwa kila shule za sekondari, kuanzisha viwanda vidogo vidogo vitakavyo toa ajira kwa wahitimu wa vyuo, kuboresha miundo mbinu ya wazalishaji wa malighafi ili zitumike kwenye viwanda hivyo, kulinda soko la ndani na kutoa ruzuku kwa makampuni madogo madogo ya wazawa.

Kuimarisha mfumo wa elimu, kuubadili kabisa kulete tija kwa maendeleo ya taifa letu, kupunguza udahili wa wanafunzi wa vyuo vikuu ili kuongeza udahili kwenye vyuo vya kati vya ufundi. Mfano mwanafunzi anayemaliza kidato cha nne apelekwe chuo cha ufundi badala ya kupelekwa tena A level ambako ni kumpotezea muda tu.

Serikali iweke mpango mahususi kwa wanafunzi wanaofeli kidato cha nne, kigezo cha Living certificate na tabia njema yaweza kuchukuliwa kama ndio kigezo kikuu kwa ajili ya kujiunga na jeshi la JKT, mashamba makubwa ya kilimo na vifaa bora vya kisasa kwa ajili ya kuzalisha mazao ya chakula na biashara, kupunguza kuagiza vyakula kutoka nje na kupunguza bei ya vyakula, kwani nchi yetu inaeneo kubwa lenye rutuba na ambalo bado halijatumika.

Idadi ya watu inavyozidi kuongezeka ndipo matatizo ya ajira yanavyozidi kuongezeka, kwakuwa mtaji ni watu na idadi ya Watanzania inafikia milioni 60 na ushee, serikali ione fursa hii, kwa kupata soko la ndani la uhakika hivyo kuto agiza bidhaa kutoka nje mfano mavazi, vyakula, vifaa vya electroniki, n.k. kutaboresha viwanda vya ndani na bidhaa za ndani kwa kuzihakikishia soko la uhakika.

Kwenye swala la ubinafsishaji wa rasilimali za Taifa, wazawa wawezeshwe na wapewe kipaumbele kwenye kushikilia uchumi wa nchi yao. Mfano, kwenye makampundi ya serikali ambayo serikali inania ya kuyabinafsisha basi kampuni iliyosajiliwa nchini ndio ipewe kipaumbele. Vivyo hivyo kwenye utoaji wa tenda kubwa kubwa, napendekeza kujali wataalamu wa ndani na makampuni ya ndani.

Tanzania tunayoitaka tutaijenga sisi wenyewe, hakuna mgeni anayeweza kuwa na uchungu na nchi yetu, hivyo viongozi waondokane na kasumba hiyo. Kutegemea mikopo na misaada kutoka kwa wafadhili wa kigeni kusitufanye kubweteka bali iwe chachu ya kupambana na kujitafutia uhuru wa kiuchumi.

Ndimi

gshewio@gmail.com
 
Elimu bora siyo kigezo cha maendeleo. Hata asilimi 10 tu wakipata elimu bora wanatosha kufanya nchi iende vyema kabisa. Kuendelea kunahitaji sera za kujitoa mhanga na usimamizi wa kibabe. Hilo haliwezekani mpaka nchi iwe inaongozwa na dikteta.
 
Vile Watanzania tunaboresha uchumi wetu😁😁😁
 
Elimu bora siyo kigezo cha maendeleo. Hata asilimi 10 tu wakipata elimu bora wanatosha kufanya nchi iende vyema kabisa. Kuendelea kunahitaji sera za kujitoa mhanga na usimamizi wa kibabe. Hilo haliwezekani mpaka nchi iwe inaongozwa na dikteta.
Ok
 
Ni kubadili mtazamo (attitude) kiongozi awe mzalendo. Chagua kiongozi mzalendo mwenye maono. Mfano DRC, nchi ni tajiri, kinachotakiwa ni kiongozi mzalendo na mwenye maono, anaethubutu. Mtu akiharibu usiangale usoni. Kuna usemi kuwa ukimchekea nyani anamaliza mahindi shambani.

Sent from my SM-A042F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom