stakehigh
JF-Expert Member
- Aug 9, 2019
- 6,385
- 3,494
- Uchumi ni nini?
- Uchumi ni jumla ya shughuli zote za binadamu zinazolenga kutosheleza mahitaji yao. Ni hasa uzalishaji, usambazaji na utumiaji wa bidhaa pamoja na kutolewa kwa huduma kwa njia mbalimbali.
- Uchumi mara nyingi hutazamwa kwenye ngazi za kijiji, eneo, taifa au dunia.
- Sayansi ya Uchumi (kwa Kiingereza economics) ni tawi la elimu inayochunguza masharti ya uchumi kufaulu au kushindwa.
- Uchumi unaendeshwa na kitu kinaitwa (TRANSACTION) au kwa lugha rahisi mwamala, kwa kawaida hakunaga kitu kama uchumi upo vibaya ama uchumi vizuri, ukiona pesa zmepotea kwenye mfuko wako basi kwa haraka unatakiwa kujua kuna mtu/watu ameacha kufanya spending kwenye budget yake ya kila sku, na wewe ukiona kuna hela haikufikii basi na wewe kuna huduma unazikata haraka haraka na anaekutegemea kwa namna moja nae anapata joto la uchumi
- Unapoenda kununua kitu chochote unabadilishana pesa na huduma ama bidhaa , kila dakika nchi nzima hiki ndo kinachofanyika, sasa kila mtu akiwa anafanya transaction pesa inakua kwenye mzunguko na unaweza tumia end point yoyote kujipatia pesa, tatizo la mfumo huu ni kwamba unapopata pesa lazima na wewe upitishe kwa mtu mwingine, ni tafauti kwenye uchumi mdogo! Nchi zenye uchumi mkubwa duniani pesa zinatembea sana , (with bonus ya high value currency), mfano nchi kama marekani $100 znatembea sana lakini hio noti bado ina thamani kubwa! Anyway ni nje ya topic, Basi kila mtu akiwa anafanya transactions serikali inauwezo wa kutap pesa kwa kuzidumbukiza kwenye miradi mipya ambayo ikasababisha pesa pia kusogea na kuzunguka zaidi, hio ndo maaana ya transaction kwako! Ili kuweza kufika hatua hii inabidi nchi iwe productive(uzalishaji), endapo wananchi watakua productive wengi basi economy inakua kwenye mstari wa kupanda always bila shuka, kwa lugha nyepesi ni hivi
-
- Nchi ikiweza kupata ukuaji huu basi serikali itafanya kazi kwa ufanisi mkubwa katika makusanyo ya kodi, lakini kibaya ni kwamba hakuna nchi yoyote yenye productivity kama hio, basi serikali inashindwa kua na constant supply of cash kwa sababu kuna watu wanaofanya kazi sana, na kuna wengine ambao ni wavivu, upatikanaji wa mapato pia unakua mdogo na huduma mpya znaanzishwa kwa taratibu sana! Lakini kwa kua pesa za dunia ni karatasi plain, ili kufidia watu ambao hawana spidi hio serikali inaweza kukopa kufidia ukuaji mdogo wa uchumi kwa wananchi.
- Lakini kuna tatizo kwenye hili jambo, ukikopa ina maaana lazima ulipe na kwa riba, ina maaana kipindi serikali inapokea hio hela, na kudumbukiza kwenye huduma za kijamii kunakua na pesa nyingi zilizojazwa kwenye mzunguko bila uwiano wa uzalishaji, lakini pia kuna kitengo kinaitwa (BENKI KUU) wao wakiona uchumi unazidi kua dim and slower wanapunguza interest rate kwenye mabenki na watu wengi zaidi wanaenda kukopa, ukijumlisha serikali + mikopo ya mashirika na watu binafasi kwenye mabenki basi watu wanaona uchumi unaenda sawa kwa sababu kila kitu wanachotaka wanakipata! Hakuna wa kuuliza kwa sababu serikali na mabenki wamemwaga pesa nyingi kwa wananchi, hii inaitwa (BOOM) everyone feels rich, u can buy anything and spend anywhere, hata zile huduma ulikua unasita kwenda kwa sababu ulikua unaona znatumia mapato yako na hazina umuhimu unaanza kurudi sehem kama hizi, kwa lugha rahisi kila mtu anakua tajiri mpaka yule mwenye huduma ya kawaida,
- Hiki ndicho wananchi hua wanalilia kila sku uchumi uwe ivi, lakni hii ni hatari, kuna kundi la watu wanaitwa wafanya biashara endapo wataona wateja wana uwezo sana basi wao hupandisha bei ya bidhaa na huduma, ili kuhakikisha hatufiki uku BOT lazima wapandishe interest rate (RIBA): Lakini pia unatakiwa kujua inapofika kipindi pesa zpo nyingi kuliko huduma unazotaka kitalaamu tunaiita (INFLATION), situation hii husababisha pesa nyingi kutokua na thamani, sasa BOT kuona hili hua wanaongeza interest rates, sasa hapa ndo tatizo linapotokea
- Kwanini natakiwa kujua haya yote?
= mimi sio mwandishi mzuri ila elimu hii ni muhimu kwa wote kuijua