Uchumba wangu upo mashakani

Uchumba wangu upo mashakani

sumia

Member
Joined
Feb 12, 2015
Posts
35
Reaction score
8
Habari zenu wanajamvi.

Wazazi wangu wanataka kurudisha mahari kwa mchumba wangu kisa imani tofauti za kidini, kinachonipa wakati mgumu ni kwamba mwanzoni walikubali kupokea kisa nilikuwa mjamzito.

Sasa nimepata miscarage wazazi na ndugu wamekaa kikao na wanakomaa mahari irudishwe kwa mchumba wangu wakati hadi engagement ring nimeshavalishwa.

Mchumba wangu bado hajapata taarifa nafikiria reaction yake sababu ameshapoteza muda sana kwa ajili yangu na pia naona ni kama mkosi vile kurudisha mahari.

Mawazo yenu jamani na ushauri nifanye nini.
 
Ao wazazi ni wakuwapeleka polisi tu huwezi kumfanya kijana wa watu kama mdoli
 
Usipopata shida hujui kama wengine huwa wana shida!
Utapokea kwa kadri ya ukitoacho!
Nadhani hayo ni maneno sahihi kwa wazazi hao
 
Wasikilize wazazi na ndugu zako wanajua lipi ni jema kwako Dada japokuwa walichokifanya sio cha kiungwana,kwani mwanzoni hawakujua izo tofauti?
 
Mie nawashangaa wazazi wako. Ina maana walikubali kupokea mahari kwa sababu ulikuwa mja mzito na si kwa sababu mmependana kiasi cha kuamua kuishi pamoja kama mke na mume? Mume mtarajiwa anafahamu kama ujauzito umetoka? Ana maoni gani kuhusu hiyo miscarriage?

Mie naona wazazi wako wamekuwa vigeugeu kwanza walikubali ndoa sasa hawaitaki tena. Kaeni na mwenzio muamue mnataka nini kama bado mnapendana na kutaka kuendelea kuwa pamoja kama mume na mke basi akili mkichwa ila muwe tayari na repercussion za kuamua kuwa pamoja kama wapenzi na hatimaye kufunga pingu za maisha. Kila la heri na baraka katika kufanya maamuzi yenu
.
 
Kiukweli Suala la Udini linataka kuota mizizi. Tatizo letu WATZ tunakariri masuala ya dini badala ya kuyaelewa.
 
Kurudisha mahari haina utofauti na kuvunja ndoa...
 
BAK

Mchumba anajua kama imeharibika na alikuwa pamoja na sisi bega kwa bega.
Ndio maana najiona mwenye hatia sana kwa sababu tunapendana kwa dhati.
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: BAK
BAK

Mchumba anajua kama imeharibika na alikuwa pamoja na sisi bega kwa bega.
Ndio maana najiona mwenye hatia sana kwa sababu tunapendana kwa dhati.
Ingefaa mchumba wako ukamwambia ili mjue mtafanya nini juu ya hili. Ila uamuzi wowote utakaochukua hakikisha unatoka moyoni mwako ili baadae usije ukajilaumu au kulaumu watu wengine. Kwa mfano ikiwa utawasikiliza wazazi na ukaamua kuachana na mchumba wako sasa ikitokea huko mbele mambo yasiwe mazuri upande wako basi pasiwe na nafasi ya kulaumu wazazi. Ikiwa utaamua kuambatana na mchumba wako na huko mbele akakuumiza basi hakikisha isiwepo room ya kulaumu na kujutia uamuzi wako. Simama ktk kile unachoona kinakufaa
 
Kama munapendana vizuri wazaz wapuuze coz kisheria na kibible mtu yeyote akifikisha miaka 18 anamamuzi yake binafisi.
 
Dada sumia , Pole na M/C na mawazo... Lakini mtu hafanyi makosa mara mbili !! Kosa la kwanza unalijuwa wewe na la pili linaelekea ( asiye sikia la mkuu huvunjika guu ) !! Wazee wanaheshima na uzito zao!!!
 
Last edited by a moderator:
Hii hata mie imenikuta,
tulipeleka posa mahali, tukajibiwa vizuri, wakati tunajipanga kupeleka mahari sasa.
Ni jana tu mambo yameibuka,
Pamoja na kuwa kijana wangu alikuwa tayari kubadili dini,
Lakini wazazi wa binti wamemjia juu hadi kumpiga msichana kwa mikanda.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Wasikutishe, beba mizigo amia kwa mumeo.
 
wasikutishe, beba mizigo amia kwa mumeo....

Wazazi hawamtishi ila lazima achunguze wazazi wameshtuka nini hadi kutaka kurudisha hiyo posa????
Kwa kweli awasikilize wazazi wake, mimi naamini ni mzazi pekee ndio mwenye huruma kwa mwanae ivo hawezi kumuongoza mwanae kwenye njia isiyo sahihi.
 
Waache warudishe baadaa ya ck mbl ww hamia kwa msela wako
 
Ninavyofahamu mimi, kama kutoa mahari ndio BARAKA zenyewe na ndoa huanzia pale wazazi wa pande zote mbili kukubaliana kutoa na kupokea mahari.

Mpaka sasa kimila unahesabika kuwa mke wa mtu make mahari na baraka zotr zimeshatolewa pande zote mbili.

Ina maana wazazi hawakuridhia wewe kuolewa? Walipokea mahari bila kutoa Baraka? Dah, inasikitisha sana.

Rejea comment ya Watu8 "Kurudisha mahari ni sawa na kuvunja ndoa" Ngoja wenye busara zao waendelee kukushauri
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom