Uchumba wangu umevunjwa

Tuliza akili, huyo mchumba wako kama yuko serious atakuelewa, na ukitumia nguvu kubwa kumuelewesha mchumba wako anaweza kukukubalia ila ataishi kwa mashaka sana. Sasa wewe huyo mchumba wake muache achambue mwenyewe asiporudi atakuwa kakuepusha na janga kwani hata yeye atakuwa ni tatizo.


pia inawezekana yey ndo kaunda picha hilo kutaka kujua reaction yako kwa matukio kama hayo, kwa hiyo utulivu unahitajika sana katika hilo.
 
Wadau, Mimi ni mwanaume....kuna tatizo limenikumba na kuharibu uchumba wangu. Nilikuwa na mchumba wangu nyumbani kwangu,mida ya saa 5 usiku. Kabla hatujalala tukiwa wote,wakati huo nilikuwa niki-set alarm huku mchumba wangu akiiangalia simu yangu,ghafla iliingia sms ya mahaba mazito kutoka kwa mtu nisiyemfahamu.....kulingana na sms hiyo alidai kuwa amemisi penzi langu sana na angetamani tuonane,hivyo nimfuate au kama nipo bize aje yeye..Kiukweli nilichanganyikiwa na mwanamke wangu alishindwa kunielewa. Nkampigia simu hakupokea, akadai yupo kwenye makelele akitoka atanipigia. Nkamuuliza wewe ni nani ....akadai yeye ni Vero mpenzi wangu. Wakati mimi sijawahi kuwa na mpenzi wala mtu wa karibu au ambae nina mazoea nae tu,anaeitwa Vero. Nilipoendelea kupiga simu yake hakupokea akadai atanipigia soon..... Mwanamke wangu alishindwa kunielewa na akaondoka usiku ule. Alipoondoka nilimtafuta huyo muhuni lakin hakupokea simu,akidai yupo kwenye sherehe ....akitoka atanitafuta,lakini mpaka napaandika uzi huu sijapokea simu yake na mara nyingi hapatikani.

Wadau naomba mnisaidie nitamfahamu vipi huyu mtu ambae lengo lake ni kuniharibia mambo yangu.
Naambatisha na "conversation" tulofanya na huyo muhuni.View attachment 1002396

Sent using Jamii Forums mobile app

umeshajiuliza swali, Je kama huyo mchumba wako amecheza huo mchezo na rafiki yake kwa nia ya kuvunja uchumba na wewe?
 
Hivi mlitegemea ndo amkumbatie vizuri after kuona hiyo text; asipanick arelax tu? Jamani kila mtu ana njia yake ya kureact, mimi ningekuwa huyo binti ningefanya tu hivyo hivyo, tungeongea siku nyingine after hasira zangu kuisha.

Let's not judge her, yeye akamtafute physically waongee, akigoma kuelewa ndo tutajuaga sasa. Lakini hapa tutahukumu tu bure, hapa ingekuwa text ndo imeingia kwa mdada ehehehee na makofi angeshakula na simu kuvunjwa kabla hata ya utetezi
You have a point. Kila mtu ana react kivyake. Ushauri wangu ni kuwa asijarib kumlazimisha bibie amwelewe bali aendelee kimya kimya kumtafuta mbaya wake. Atakapomjua basi amalizie kesi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu hivi.....
Kwani ulikua na wachumba wangapi...!!??
Maana kwa uzowefu wangu kwenye hii sector ya viwanda, kabla hauja oa unapaswa walau ukuwe na wachumba watatu...tehteehh
 
Mkuu, kabla sijakushauri chochote naomba kujua kwamba je hilo ni kosa lako la ngapi kwake kukuta sms kama hiyo kwenye simu yako??? Au kuna siku umewahi pigiwa simu za utata ukiwa nae huyo mchumba wako???
 
kwanini ulimruhusu kuangalia simu yako huyo mwanamke? njia rahsi ya kutafuta sababu ya kumuacha mke/mme wako ni kudukua simu yake
 
Mpaka nimpe mwanamke simu hata ashike tu nimeficha kila kitu sms zinaingia kimya kimya hamna notification iwe ya whatsapp au call simu inakuwa kama ipo kwenye airplane mode
Na sijawahi feli coz yalionikutaga hayatajirudia tena nilijifunza
Pole mkuu najua inavyouma duh
 
Hahahah huyo ni manzi anaekujua na ameamua kukuharibia style makusudi tu. Tuliza kichwa taratibu utamgundua otherwise wataalamu watakuja na ngonjera za jini mahaba. Sasa sijui majini wanatumia smartphone sikuhizi!
ndio majini yanatumia smat siku hizi kuna mdau alipost juzi kati jini limemtumia hela na linachat nae

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila mkuu usimwamini mwanamke % zote kushikashika simu yako wengine wanapenda ugonvi tu hata akikuta picha ya famila mko mama, baba, dada na mabro ataulizia hao wanawake nikina nani wako haamin mpaka hawaone aamin
 
Kaka asante. Uelewa wangu ni mdogo ndo maana nkaomba msaada. Ila kwa uelewa wangu mdogo nmefanya yafuatayo. Nmeangalia tigo pesa, jina kweli ni Veronica lakini sijawahi kuwa familiar na hilo jina. Nme-search hilo jina na number Facebook lakini hakuna details.... Nmeangalia whatsap...hayupo whatsap...nmewapa watu wangu wa karibu hiyo no wachunguze,lakini hajibu calls wala sms. Naomba msaada wako, nmesema uelewa wangu ni mdogo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hivi huo ulimwengu wa mchumba wako unaujua wote? Unafikiri atatoa namba ys demu wa karibu ili umjue! Yeye anaweza kuwa dar huyo vero yupo Arusha kapewa mchongo huo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa mimi mwenye uzowefu kwenye hii sekta ya mahusiano, naomba nihitimishe kwa kusema kwamba.....Huyo mwanamke alikua hakupendi, na alikua ana target umkosee ili apate strong reason ya kukuacha.
Kimsingi ipo hivi...... Mwanamke kama anakupenda, hata ikitokea amekufumania ukiwa kifuani mwa mwanamke mwingine huyo hawezi akakuacha ama lahh, atakupa nafasi ya kukusikiliza basi hata umdanganye na kisha maisha yaendelee.

Naomba kuwasilisha
View attachment 1002401
Unajua nakusikiliza na kwa kuwa Umekiria kuwa Umebobea kwenye hiyo sekta sina Shaka na kweli wote bado wanakupigania, Confirmatory test done . Big up brother
 
Mkuu huyoalaikuwa mpenzi wako wa Muda mrefu au Mchumba wako? Level ya Uchumba wako ikoje? Ulishato mahali na kutambulishana pande zote za Familia? Ukinijibu nitakuja na Majibu ya kilichotokea.

Ila tofautisha Mahusiano ya Kingono ambayo wengi mnayaita ( Mapenzi, Upenzi) na mahusiano yaliyoruhusishwa na familia za pane=de zote mbili ambazo ndizo zinazaa neno (Mchumba/Uchumba) baada ya kutoa Posa au kitu chochote ambacho mila husika zinakiheshimu...

Nawasilisha
 
Unajua nakusikiliza na kwa kuwa Umekiria kuwa Umebobea kwenye hiyo sekta sina Shaka na kweli wote bado wanakupigania, Confirmatory test done . Big up brother
Kupiganiwa sio sifa, na katika safari ya mahusiano naamini kuna watu wengi hasa wanaume (wanafiq) ambao hupendelea kujionyesha kwamba wao ni wasafi na hawakuwahi kukisea ama kuwa na wachumba zaidi ya mmoja wakati wa ujana wao.
Hapa nadhani ni wakati muafaka wa kumuelekeza kijana ili ajifunze kupitia mimi/sisi, na asije akafanya makosa kama nilio ama tulio kwisha kuyafanya.
Haya wewe ambae ni msafi and perfect, ebu tupe maekelezo sisi wazinifu na wachafu (kwa kauliyako tunao gombaniwa) ebu natamani nijifunze ama tujifunze kutoka kwako wewe Mr perfect.
 
Mkuu huyoalaikuwa mpenzi wako wa Muda mrefu au Mchumba wako? Level ya Uchumba wako ikoje? Ulishato mahali na kutambulishana pande zote za Familia? Ukinijibu nitakuja na Majibu ya kilichotokea.

Ila tofautisha Mahusiano ya Kingono ambayo wengi mnayaita ( Mapenzi, Upenzi) na mahusiano yaliyoruhusishwa na familia za pane=de zote mbili ambazo ndizo zinazaa neno (Mchumba/Uchumba) baada ya kutoa Posa au kitu chochote ambacho mila husika zinakiheshimu...

Nawasilisha
Mkuu, sioni sababu ya kumuuliza maswali mengi mleta mada.
Hapa kwa jinsi alivyo elekeza, hai hitaji hata shule kubwa ili kubaini kinacho jiri kwenye mawazo ya mchumba wa mleta mada.
Naaa...... jf tujifunze kuheshimu mawazo ya yeyote mleta mada, hii hutokana na wakati mwingine mwenye threads hajisikii kuanika baadhi ya mambo zake kwa undani.
Nivyema tumshauri kwa kiwango cha maelekezo alio yatoa mleta mada, na kwaku mchimba nadhani ni kutaka kuingilia yale ambayo mleta mada hakupendi tuyafahamu.
 
Pole Sana kwa mchezo aliokuchezea huyo mchumba wako it's a game ili akae mbali na wewe na hakupendi kabisa na hayuko tayari kuwa mke wako. Kama huamini jaribu kumuita Kisha mweleze Kila kitu alafu mpe jukumu na yeye la kumtafuta huyo Malaya wake aliye mtuma Kama atakubali. Kama kweli anakupenda atakubaliana na wewe ili mtatue Hilo tatizo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom