Hapo inawezekana ni dili amecheza huyo mchumba wako alitaka akuache akakosa njia sahihi basi akampanga rafiki yake ili atume hiyo meseji ukiwa na mchumba wako
Sent using
Jamii Forums mobile app
Nimewaza the same, usijiumize sana inawezekana mtu wako alishapanga kukuacha ila hana ground ya kufanya hivyo akaamua kufanya umafya aidha na rafiki yake wa kike,, au hata mwanaume wake mpya anayependa kuendeleza naye urafiki..
Inauma sana maana lijamaa litakuwa kishaanza kumtafuna...
Kama kweli angekuwa anakupenda kutoka moyoni hawezi kukuacha kirahisi hivyo lazima angekuhoji, angechukua namba ya huyo mdada amtafute ajue ukweli,, asingekurupuka na kuondoka.
Hilo dili mwana acha kuumiza sana akili. Najua inauma ukiachwa bila kutarajia,, kisaikolojia inaumiza sana,,
Fanya yafuatayo
1. Kwanza jiulize kabla yake mbona ulikuwa unaishi vizuri tu,, hata sasa utaishi vizuri tu kwanza kakuondolea mikosi
2. Piga maombi kwa sana,, mshukuru Mungu kakuondolea huyo yumkini huko mbele angekuja kukuletea madhara.
3. Kama unamtafuta na haangaiki na wewe mwandikie mesage ya kumuaga kabisa ajue umetoa moyoni mwako maana hakuwa na mapenzi ya dhati kwako..
4. Mwana tafuta hela..., piga maombi kwa sana
5. Tafuta hela mwana..., usimwache Mungu piga maombi,
6. Nasema hivii piga hela ndefu....usisahau sala
7. Tafuta hela..., ibada kwa sana
8. Achana na mademu uchwara tafuta hela, maombi kwa sana
9. Tafuta helaaaa, mtafute Mungu
10.Utaishi kwa raha sana.