Mume wangu hataki msamaha wangu

happy amos

JF-Expert Member
Feb 23, 2012
251
434
Naogopa Sana

Iko hivi jana tulikua namaongezi na mzee sebulen mpaka saa 6 usiku sababu toka nimetoka nyumban kujifungua ni kama ananikwepa hivi.

Akitoka kazini anipita uwanjan kwenye mazoez mpaka saa 3 usiku akirudi anakaa seblen anaangalia mpira mpaka saa 7 ndio anakuja kulala na gafla ukija seblen unamkuta anachat na simu sasa Jana nikaamua kumuuliza.

Tukiwa katika maongezi akapigiwa simu hakupokea ikarudia tena akaikata simu ikiwa vibration, Nikamwambia mbona hiyo simu unaikata? Nani anapiga akadai achana na simu bahati mbaya nikampokonya simu akaja juu achana na simu yangu akaninyonga mkono nikamng'ata mkono.

Uwiiii hapo ndio nilipoamsha mashetani sababu alinikimbiza anipige na rungu nikamtoroka nikajifungia chumbani namuomba msamaha hataki kunisikiliza.

Leo nimeamka namuomba msamaha hataki nifanyeje jamani. Wasiwasi wangu anaweza niua maana ana hasira Sana alafu chumban Kuna rungu na sime
 
Kuna njia nyingi :

1.Kama unampenda : Tuma ujumbe wa kuomba msamaha akirudi nyumbani ujifanye kama hamna tatizo anaweza akakaa kimya iko siku atajishitukia.

2.Kama umeshachoka hutaki vita: inategemea na hali ilivyo, unaweza kuamua kuondoka, uanze mchakato wa kutengana.

3. Kama vita ni vita: mvizie siku ataingia kwenye anga zako unambinya nani hii kisawa sawa hata apige kelele vipi akiendelea kufurukuta unampa onyo "ukiendelea utazipoteza" kuna mdau humu aliadabishwa kwa siku mbili alikuwa hata hawezi kutembea vizuri.

Ukweli ni kwamba mara nyingi ndoa hudumu kwasababu ya uvumilivu wa mwanamke !
 
Naogopa Sana

Iko hivi Jana tulikua namaongezi na mzee sebulen mpaka saa 6 usiku sababu toka nimetoka nyumban kujifungua ni kama ananikwepa hivi.

Akitoka kazini anipita uwanjan kwenye mazoez mpaka saa 3 usiku akirudi anakaa seblen anaangalia mpira mpaka saa 7 ndio anakuja kulala na gafla ukija seblen unamkuta anachat na simu Sasa Jana nikaamua kumuuliza.

Tukiwa katika maongezi akapigiwa simu hakupokea ikarudia tena akaikata simu ikiwa vibration, Nikamwambia mbona hiyo simu unaikata? Nani anapiga akadai achana na simu bahati mbaya nikampokonya simu akaja juu achana na simu yangu akaninyonga mkono nikamng'ata mkono.

Uwiiii hapo ndio nilipoamsha mashetani sababu alinikimbiza anipige na rungu nikamtoroka nikajifungia chumbani namuomba msamaha hataki kunisikiliza.

Leo nimeamka namuomba msamaha hataki nifanyeje jamani.
Wasiwas wangu anaweza niua maana ana hasira Sana alafu chumban Kuna rungu na sime
Yaani wewe ndo umeyapatia umeolwa na security kabisa Rungu na Sime
usihofu hana mpango hata wa kukupiga mkwala tu usiguse simu yake siku nyingine hatakufanya kitu ila fanya imeisha hiyo endelea naye kwa matukio mengine atarudi usihofu
 
Pole sana kwa hilo.
Kwanza ondoa hizo silaha rungu na sime chumbani.

Kisha mtumie sms ya kumuomba msamaha kuwa hutorudia kosa lako tena.pia andika ujumbe wa mahaba na heshima.

Kisha mpikie mumeo chakula anachokipenda zaidi.

Akirudi nyumbani hakikisha umekuwa smart mithili ya kuvutiwa na ww.

Mpokee mumeo, muandalie maji yakuoga, mpe chakula anachopenda na mfariji mumeo hakika hasira zitaisha na atakusamehe. Tumia lugha ya upole, sura ya kimahaba na sio uoga.

Siku zote mwanaume anahitaji vitendo vinavyompa yeye heshima kwa mke wake, na mwanamke anahitaji maneno yenye kuakisi mahaba na upendo. Hii ndiyo kanuni.

Kila raheli utanipa mrejesho
 
Kuna njia nyingi :

1.Kama unampenda : Tuma ujumbe wa kuomba msamaha akirudi nyumbani ujifanye kama hamna tatizo anaweza akakaa kimya iko siku atajishitukia.

2.Kama umeshachoka hutaki vita: inategemea na hali ilivyo, unaweza kuamua kuondoka, uanze mchakato wa kutengana.

3. Kama vita ni vita: mvizie siku ataingia kwenye anga zako unambinya nani hii kisawa sawa hata apige kelele vipi akiendelea kufurukuta unampa onyo "ukiendelea utazipoteza" kuna mdau humu aliadabishwa kwa siku mbili alikuwa hata hawezi kutembea vizuri.

Ukweli ni kwamba mara nyingi ndoa hudumu kwasababu ya uvumilivu wa mwanamke !
Kuwa na utu tafadhali, kwa hali hii ndio maana sihitaji kuwa verified.
 
Back
Top Bottom