Bukoba Finest
JF-Expert Member
- Jul 13, 2023
- 250
- 314
Jinsi mama wa msichana alivyovuruga mahusiano yangu.
Hii ni true story
Mwaka 2019 nilimpata Binti wa kichaga akanipa condition moja tu kwamba kama nahitaji mahusiano naye basi natakiwa kujitambulisha kwa mama yake (Preliminary stage) hapo ndo tunaweza kuanzisha mahusiano na baadae tukaanza Mipango ya ndoa.
Nilifanya hivyo nikampigia mama yake simu nikajitambulisha, lakini muitikio haukuwa mzuri kwanza hakunipenda kwa sababu natokea ukanda wa akina "Nshomile".
Mimi baada ya kufanya hivyo kazi nikamuachia binti yake ndio aamue sasa nini cha kufanya of course mahusiano yaliendelea japo upinzani mwingi kwa mama yake, siku zikaenda mara ghafla ya katokea ya kutokea akafanikiwa kupata ujauzito. Tulifurahi sana.
Lakini kwa upande wa mama yeye hakufurahishwa pamoja kuwa taratibu zote za kujitambulisha na kupeleka kishika uchumba zilishafanyika basi mama yake akawa anajiweka karibu yangu sana kumbe anang'ata na kupuliza.
Kamwe hakupenda nishike simu ya mtoto wake akidai simu ni mali ya mtu binafsi na yaliyomo ni siri yake, basi baada ya muda mpenzi wangu alifanikiwa kujifungua salama lakini baada ya siku tatu Mungu alimchukua mtoto baada ya kupaliwa na maziwa akiwa ananyonya.
Hapo sasa ndo kisanga kilianza kwetu kwa akina kyoma huwa kuna dawa za kienyeji ambazo huwa zinatumiwa na mama kipindi akiwa mjamzito sasa kipindi mchumba wangu ni mjamzito alikataa kutumia hizo dawa akidai yeye hajawahi kutumia dawa za asili jambo ambalo mimi halikunipa wasiwasi kwani alikuwa anaudhuria clinic kama kawaida.
Basi mama yangu akasema huenda mtoto amekufa kwasababu mpenzi wako hakutumia dawa za kienyeji" ( Mtoto aligoma kunyonya siku mbili akanyonya ya tatu na akapaliwa hapo hapo). Bada ya mama kusema hivyo basi mama mkwe akawa anamwabia mtoto wake kuwa hizo dawa ni za mizimu, ni za kishirikina na ndo maana mtoto wako amefariki, story zilikuwa nyingi za kumkatisha tamaa mpenzi wangu japo mimi nilisimama kiume kwa sababu kuna rafiki yangu aliniambia kipindi hiki usipokuwa imara utaambiwa maneno mengi ya kukugombanisha na mwenzako"
Baada ya muda mpenzi wangu alibadilika sana ugomvi ukazidi ndani tukawa hatusikilizani kabisa, mpenzi wangu aliamua kumsikiliza mama yake na kuniacha na mimi niliona baadhi ya sms alizokuwa anamtumia. Mimi nilisimama kiume na baada ya miezi sita nikaanzisha mahusiano mapya (nilikata mawasiliano naye miezi miwili nyuma) Sijui ni bahati nzuri sijui mbaya niliyeanzisha naye mahusiano naye ni mchaga pia😤.
Tukawa tunaendelea na mahusiano yetu lakini mimi moyo wangu haukuwa real kwake kwasababu nilimpenda yule wa kwanza na tulikuwa na memories nyingi ngumu sana kuzisahau na kama ingetokea akanitext nilikuwa nafurahi sana. Baada ya mwaka mmoja na miezi kama miwili hivi mama mkwe wa kwanza akawa ananitumia ujumbe wa kwenye biblia unaonionya kwanini nilimfanya mwanae mke wangu wakati wa ujana wangu na nikamtenda roho iliniuma sana, na baadae mtoto wake alinitafuta akaniomba msamaha akasema yeye alishinikizwa na anaomba nimuoe ameshindwa kabisa kuwa na mahusiano mapya. Mpaka sasa hivi nimemsamehe na tunaishi pamoja niliamua kuvunja mahusiano yangu ya pili na tunaishi kwa furaha.
Je ungekuwa wewe ungeitikiaje kwenye hili, na pia nipe maoni yako kuhusu uamuzi wangu. Nawasilisha.