Vipindi hatari katika Uchumba/Mahusiano ya Vijana

willpower

JF-Expert Member
Dec 3, 2019
404
2,271
Kwa wadogo zangu:

Leo nina muda kidogo wa kuandika, nikakumbuka maisha yangu binafsi na misukosuko ya kimahusiano; nikaona nije na huu uzi; vipindi hatari kwa uchumba/mahusiano ya vijana wengi.
Hivi ndio vipindi ambavyo mahusiano mengi hufikia tamati na kuacha aidha uchungu ama fadhaa kwenye mioyo ya vijana wengi.

Hapa nitazungumzia vijana ambao walau wamefika kiwang cha elimu ya juu. Maana huu ndio muda ambao wengi huanzisha mahusiano serious....

1. Kipindi binti/mwanamke anapopata kazi
Hii ilinitokea, miaka hiyo na mpenzi wangu, hapa mwite Sara, dada na taaluma yake ya masuala ya Benki; nikamuunganisha na jamaa yangu mmoja kwenye benki fulani hapa City Centre; Binti na familia yake walinishukuru na alianza kazi vyema kabisa huku tukiendelea na mahuasiano yetu kwa furaha na amani.

Baada ya muda akahama kwao; tukaenda kupanga mitaa ya Kijitonyama, nilikuwa naishi kwenye nyumba ya mjomba . Ikawa sasa sikai tena kwangu; tukawa kama mke na mume. Hii ina raha yake, asikwambie mtu huwa ina raha yake sana; mnatoka kazini unampitia binti anakusubirisha kidogo ili aweke hesabu zake sawa. Mnarudi zenu nyumbani; mnakumbatiana na mnapanga mipango ya kimaisha mpaka mnapata na majina ya watoto.

Baada ya muda wajanja wa mjini wakamuona; si unajua tena Posta ya wakati ule; kama hujaenda kula Break point basi utakuwa pale Petrol Station ya Oryx au Meals Restaurant mtaa wa Pamba. Mwanzoni alikuwa anapambana sana kulinda penzi lakini mwishoni watu wakapanda dau, na kama ujuavyo kila mtu ananunulika; mtu mzima mmoja wa pale mnapohifadhi fedha za hii nchi hatimaye akamchukua.

Dalili za kwanza ikawa ananiambia nisimpitie maana atachelewa kutoka, sasa nikawa nawaza huyu mimi nina usafiri kwa nini ghafla tu hataki kuongozana na mimi(mume mtarajiwa). Kumbe mzee wa minara miwili ameshamuagizia gari kutoka Japan. Baada ya muda ikawa wazi kuwa ana mahusiano; nikabeba vitu vyangu; nikarudi kwenye nyumba ya urithi kwa mjomba. Iliniathiri kwa yale mazoea; ila kama ujuavyo sisi wengine huwa yakiisha yameisha; hakuna muda wa kujilizaliza.

Sikuwa na ubavu kwa huyu mzee. Uhusiano ukaishia hivyo😅

2. Unapokuwa mbali naye kikazi
Baadaye kaka yenu nikajitafuta nikapata binti fulani mweupe, sura nzuri, mwili wa kike na vijiakili kichwani; nikasema sasa hapa nitulie ili nioe hatimaye nipeleke wajukuu nyumbani; huyu sikuwa na hofu naye kuhusu hela maana alikuwa anajiweza haswa tofauti na yule wa kwanza ambaye nyumbani kwao hali ilikuwa mbaya. Tukiwa katika penzi motomoto, nikapata mchongo wa kazi za UN nchi fulani hapa Afrika ya Magharibi; nikaangalia malipo nikaona huu ndio muda wa mimi kutoka kimaisha.

Mkataba ni wa mwaka na unapata likizo baada ya miezi nane. Mtoto wa kiume nikaona miezi nane sio kesi; nikaongea na bibie; akasikitika lakini mwisho tukakubaliana kuwa acha mimi niende kuchukua dola za kimarekani; miezi 8 sio mingi.

Safari ikawadia kweli; nikafika Afrika ya Magharibi; mazingira ya kazi hayakuwa magumu sana maana kazi nyingi zilikuwa ni paperwork; hivyo nilikuwa na muda wa kutosha kuwasiliana na huyu binti. Miaka ile tulikuwa tunatumia Yahoo Mesenger na MSN Mesenger.

Baada ya muda tukaombwa na ofisi kuwa kutokana na hali ilivyo, inabidi tumalize mwaka kabisa japokuwa hela ya likizo tutapewa pamoja na gharama za usafiri; lakini tubaki kwa miezi 12.

Wakati huo huku Bongo ninajenga lakini msimamizi ni kaka yangu, huku mchumba wangu akiwa anashauri namna ya ujenzi na vitu vingine maana hii ndio ingekuwa nyumba yetu baada ya ndoa. Kwa wakati huo hata majina ya watoto tulikuwa nayo 😄Mapenzi ufala sana.

Muda wote huu mapenzi ya kwenye simu na mesenger, kumbe upweke umeshamchosha mtoto wa watu, akaanza kutoka na jamaa mwingine; kwa siri. Ikiwa imebaki miezi minne kurudi; nikapewa taarifa kuwa shemeji ana mahusiano na mtu; ilinisikitisha sana kwa sababu ikanikumbusha namna mahusiano ya kwanza yalivyoisha.

Niliporudi yakawa yameisha; nilipata muda wa kuonana naye; tukaongea na kwa ustaarabu wake akaniomba msamaha; lakini kwangu hii habari ikawa imeisha. Haikuisha bila maumivu na uchungu lakini nilijifunza mapema sana kuwa mapenzi yakiisha, yaache yaishe.

Unataka kujua hawa wanawake wana hali gani sasa hivi?

Wana hali nzuri tu za kimaisha na wamebaki kuwa marafiki ambao tunakutana mara chache katika matukio ya kijamii.

Mahusiano ya kimapenzi hufikia mwisho; usibebe chuki, hasira na uchungu moyoni. Ni vipindi tu katika safari ndefu ya maisha.
 
Naona hujaweka unapokua umeyumba kiuchumi biashara haziendi au hauna kazi....


Ila ww ulikua una pesa na bado yakakukuta kweli haya mambo hayana fomula na usitafute pesa kumridhisha mwanamke
Hilo ni somo; kila mwisho wa mahusiano una sababu zake; unaweza kuwa na fedha ikaja sababu nyingine. Jmbo la msingi ni hilo ; HAYA MAMBO HAYANA FORMULA
 
Pole sana mkuu
Asante sana; nikiangalia nyuma na ninapoangalia maisha yangu ya sasa naona kabisa ilikuwa ni safari tu katika kujifunza. Kwa sasa nashangaa vijana wanapochanganyikiwa kwa kuachwa na kuachana.
 
b77a991d-0d79-4c1b-9d40-983c51233e8a.jpg
 
Kwa wadogo zangu:
Leo nina muda kidogo wa kuandika, nikakumbuka maisha yangu binafsi na misukosuko ya kimahusiano; nikaona nije na huu uzi; vipindi hatari kwa uchumba/mahusiano ya vijana wengi.
Kosa lako ni moja uchumba wa mda mrefu chenga tupu , muoe mpe mimba mambo mengine mbele kwa mbele , ni 2% ya wanaume hukubali kupokonya mwanamke mwenye mtoto , wengi ni eat and run.... Sasa wewe uchumbaa tuu unawaacha wananawiri holaaaa...lazima wahuni wapite nao
 
Tumeishi mzee; miaka ile sehemu ya kukutana mjini ni pale ofisi za Posta.
Wewe kweli mkongwe...

Tumeishi mzee; miaka ile kukutana pale ofisi za Posta.

Wakati wa mgahawa maarufu wa Food World

Maduka ya simu maarufu ni SAPNA

Supermarket ni IMALASEKO

Pizza tunakula pale Steers mtaa wa Ohio/Samora naona siku hizi kuna Petrol Station

Tunachat kupitia Yahoo Mesenger na MSN Mesenger

Wenye email address walikuwa yahoo.com au hotmail.com

VISA za Marekani tulikuwa tunajaza internet cafe, unapamba na muda ili kupata pdf yenye barcode....

ATM ukiikosa Millenium Towers lazima uje Posta.

Kona ya Mlimani City kulikuwa na Petrol station ya BONJOUR

Barabara ya Sam Nujoma ikiwa mbovu hatari.





Maisha ni safari.
 
Kweli....kumbe na zamani wanawake walikuwa wababaishaji ee.
Asikwambie wadada/wanawake ni wababaishaji na pasua kichwa enzi na enzi; ukiwa na mtoto wa kiume jambo la muhimu ni kumfundisha kuwa mapenzi huisha; awekeze akili na maarifa kwenye mambo ya msingi maana kwenye mapenzi asipotuliza akili anaweza kuchanganyikiwa.
 
Asikwambie wadada/wanawake ni wababaishaji na pasua kichwa enzi na enzi; ukiwa na mtoto wa kiume jambo la muhimu ni kumfundisha kuwa mapenzi huisha; awekeze akili na maarifa kwenye mambo ya msingi maana kwenye mapenzi asipotuliza akili anaweza kuchanganyikiwa.
Umesema ukweli mkuu, Ashraf Hakim ametuonyesha Mwanga km reference na wewe pia umeonyesha Mwanga mwingine kua hawa pasua kichwa wakipasua move on usiwaze mara 3
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom