Wadau, Mimi ni mwanaume....kuna tatizo limenikumba na kuharibu uchumba wangu. Nilikuwa na mchumba wangu nyumbani kwangu,mida ya saa 5 usiku. Kabla hatujalala tukiwa wote,wakati huo nilikuwa niki-set alarm huku mchumba wangu akiiangalia simu yangu,ghafla iliingia sms ya mahaba mazito kutoka kwa mtu nisiyemfahamu.....kulingana na sms hiyo alidai kuwa amemisi penzi langu sana na angetamani tuonane,hivyo nimfuate au kama nipo bize aje yeye..Kiukweli nilichanganyikiwa na mwanamke wangu alishindwa kunielewa. Nkampigia simu hakupokea, akadai yupo kwenye makelele akitoka atanipigia. Nkamuuliza wewe ni nani ....akadai yeye ni Vero mpenzi wangu. Wakati mimi sijawahi kuwa na mpenzi wala mtu wa karibu au ambae nina mazoea nae tu,anaeitwa Vero. Nilipoendelea kupiga simu yake hakupokea akadai atanipigia soon..... Mwanamke wangu alishindwa kunielewa na akaondoka usiku ule. Alipoondoka nilimtafuta huyo muhuni lakin hakupokea simu,akidai yupo kwenye sherehe ....akitoka atanitafuta,lakini mpaka napaandika uzi huu sijapokea simu yake na mara nyingi hapatikani.
Wadau naomba mnisaidie nitamfahamu vipi huyu mtu ambae lengo lake ni kuniharibia mambo yangu.
Naambatisha na "conversation" tulofanya na huyo muhuni.
View attachment 1002396
Sent using
Jamii Forums mobile app