Uchumba wa muda mrefu umenichosha

Kimsingi wewe ndo una hasara hapo.
Umri wa mwanamke kuzaa una ukomo, mwenzio hata by 50+anatungisha mimba.

Endelea kushirikiana nae kwenye huo mpango wenu!
 
Una umri gani ww na huyo mwenzako ana umri gani?Tuanzie hapa
 
Kimsingi wewe ndo una hasara hapo.
Umri wa mwanamke kuzaa una ukomo, mwenzio hata by 50+anatungisha mimba.

Endelea kushirikiana nae kwenye huo mpango wenu!
Usihangaike sana hata kaburi lishafukuliwa hii ni chai kama chai zingine tafuta maandazi tu hapa.

Btw miss u
 
Usiwe na hofu.Mbona Baba wa imani nabii Ibrahim aliishi miaka mia tisa (900)na hakupiga kelele?
 
kwani huwezi mshawishi akaenda kwenu kujitambulisha na kutoa mahari then mkaanza kuishi pamoja? au mpaka ndoa? maana hiyo ndoa ndo inaweza isitokee kwa miaka mingine 11 lakini suala la kuamua kuishi pamoja ni issue ya miezi 6 tu
 
11 years? Na wewe unaendelea kumpa kyuma tu?....poor girl unatumika na bado hujagundua unatumika.
Miaka 11 kwa mtoto wa kike umepoteza parefu imagine ungekuwa kwenye ndoa ndani ya muda huo ungekuwa na watoto wangapi?
 
"Kama kilivyo kipini cha dhahabu kwenye pua ya nguruwe.....basi hivyo ndivyo hivyo alivyo mwanamke mzuri asiyekuwa na akili'
 
Ukishahitaji kufanya mbinu ili mtu akuoe hapo ushakosea kitu.

Maana yake hapo hatakuoa wewe ataoa hizo mbinu, ambazo kuendelea kuzifanya miaka yote itakuwa shida, kwa sababu huo si uhalisi wako ni hadaa umefanya ili uolewe tu.

Kama unaona hana nia ya kukuoa, na wewe unataka kuolewa, achana naye tafuta anayetaka kukuoa.

Kwani wewe mbaya hivyo ukiachana naye hutapata mwingine wa kukuoa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…