Uchawi upo, usidanganywe

Uchawi upo, usidanganywe

Kuna jamaa m1 mid 90 alikuwa kamaliza chuo sasa kila akipata kazi anaacha baada ya kuifanya kwa muda mfupi. Baada ya kuangaika sana bila mafanikio mzee m1 wa makoamo akasema huyu atakuwa kalogwa. Basi wakaenda kwa wataalam walichoambiwa na dawa yake ni vigumu kuamini.

Aliambiwa kalogwa na dawa yake ni lazima aende kwenye msitu maeneo ya huko upareni. Alitajiwa eneo na aliambiwa atakuta nyuki wametulia juu ya mti. Basi awafukuze kwa aidha kuwapiga kwa mawe au kupanda na kuwaondoa kwa mkono. Vyovyote vile ilimradi watoke pale.

Watu wakatili. Jamaa akaongozana na yule mzee na ndugu yake m1. Walipofika maeneo hayo wakakuta nyuki kweli, walishahakikishiwa kuwa kutakuwa hamna hatari yoyote yaani nyuki watakuwa wapole kama inzi. Ila atagongwa na wawili au watatu. Wakaingia mzigoni wakafurumusha nyuki ambao waliondoka eneo lile. Kweli kuna nyuki kadhaa waliwagonga.

Waliporejea nyumbani wakakuta wale nyuki wapo kwenye moja ya banda la kuku pale home kwao. Wakarudi kwa bingwa na kumweleza. Akawaambia kuwa wale watakaa pale kwa muda wa siku sita na siku ya saba awafukuze tena kama alivyofanya kule msituni. Siku zikaenda muda ukawadia. Akawafukuza kama mwanzo ingawa siku hiyo alitolewa manundu ya kutosha. Baada ya kupita kama mwezi hivi jamaa akachukua ajira na sasa ni moja ya mabosi huko mkoani tabora. Hakuwahi kuacha kazi tena.
Kwa hiyo alikuwa amerogwa, na yeye ni wa huko huko upareni?
 
Mkuu nilichogundua hapo in kuwa una miaka 30 hayo mengine niyakawaida tuu
Baada ya kugundua ilitosha ukakaa kimya, na wajuaje kama ameandika taarifa za kweli. Mambo kama haya usitegemee mtu akaweka ukweli wake wote humu.
 
Ah wapi...huyo jamaa atakuwa aliuwawa na wasaidizi wa huyo Mzee....hakuna kitu kama hicho

Huyo tembo kuna alomshuhudia kwa macho?
 
Japo umeandika bila vituo wala nukta ila sijaelewa point yako. Mchawi/mganga wa Nigeria anamzidi vipi mganga/mchawi wa Tanzania kama hakuna uchawi... Umetoa namba tubadilishane uzoefu wa kitu ambacho hakipo?
Dunia ni pana sitaki uniamini mimi lakini ukiweza tunaweza badilishana uzofu bila shaka mimi nitajifunza kwako na we2 utajifunza kwangu.elimu haina mwisho ndio maana dunia haikuwahi kusimamama
 
Mkuu nilikua sijsoma story yako nikiamini, kama story zingine zote za uchawi, huwa zinaacha loopholes and surely enough yako pia was no exception to this. Kwanza ni kawaida kwa waganga wa jadi kusema mbaya wako ni jirani yako au ndugu yako kama hujui hili hadi leo basi siwezi kushangaa kwanini unaamini uchawi upo.

Pili, kuuwawa na tembo au wanyama maeneo ya karibu na mbugani ni jambo la kawaida, sawa na mtu wa mjini kugongwa na gari. Nadiriki kusema ilikua coincidence tu na pengine huyo mtu asingekufa mganga angekuja na sababu zingine kama kawaida yao.

Nitakupa kisa kidogo, Juma alimwambia Obedi leo usiku utanikoma baada ya kukorofishana, Obedi usiku ule aligongwa na gari na kufariki pale pale unadhani Juma ni mchawi? Kwanini isiwe conicidence? Unaweza muongelea mtu mabaya bila kumaanisha na jambo baya likampata ila hiyo sio ithibati ya kuonyesha wewe ni mchawi.

Hizi ndo kasoro za story za uchawi, ni story za hearsay na mara nyingi zina loopholes ambazo watu hukimbilia kusema ni uchawi wakati zinaweza kujibika kwa njia zingine.

HAKUNA UCHAWI.
Haujaweza kueleza ni vp hakuna uchawi bali umeonesha tu kuwa tukio linalohusishwa kuwa ni uchawi linaweza lisiwe tukio la uchawi na kulitafsiri tofauti.

Tatizo hamuelezi ni vp hakuna uchawi,na kibaya hata yale matukio ambayo mmeshindwa kuyaelezea pia mnapinga si uchawi na kung'ang'ana kusema kwamba kutakuwa maelezo yake ila hamyajui.
 
Haujaweza kueleza ni vp hakuna uchawi bali umeonesha tu kuwa tukio linalohusishwa kuwa ni uchawi linaweza lisiwe tukio la uchawi la kulitafsiri tofauti.

Tatizo hamuelezi ni vp hakuna uchawi mnabaki kujaribu,na kibaya hata yale matukio ambayo mmendishwa kuyaelezea pia mnapinga si uchawi na kung'ang'ana kusema kwamba kutakuwa maelezo yake ila hamuyajui.
Sio kazi yangu kueleza hakuna kitu fulani wakati hakipo, wewe unayeamini kipo ndo inabidi uthibitishe pasi na shaka kwamba kipo.

Nikisema hakuna bahari Moro sihitaji kueleza zaidi ila Kama unaamini Moro kuna bahari basi wewe ndo inabidi uthibitishe.

Tumeomba humu mara kadhaa mturoge tuamini huo uchawi mnashindwa, mnakuja na sababu kibao za kukwepa.

Story za uchawi zinaaminiwa na wavivu wa kufikiri.
 
Wewe ndio mvivu wa kufikiri na ndiyo maana unasema sio kazi yako kutoa maelezo,ungekuwa unaweza kuelezea usingesema hivi.

Kiujumla wewe unadai hakuna uchawi kabisa bila hata kueleza ni kwa vp,halafu hapo hapo yanatokea matukio yenye kuhusishwa na uchawi wewe unapinga kuwa sio uchawi hata kama hauwezi kutolea maelezo ya hayo matukio kwa kuonesha kuwa sio uchawi.

Kwa hali hiyo hata hivyo unavyosema urogwe ili ndio ujiridhishe kuwa uchawi upo,hata mtu akikuroga ndiyo kipi kitakufanya ujue kuwa ni athari za uchawi ama sio uchawi?
Mfano mie niseme nataka kumroga mwanao awe chizi,mara baada ya siku chache mwanao akapata malaria ikampanda kichwani na kuwa chizi.

Utawezaje kujua ni athari ya uchawi ndiyo chanzo cha yote hayo?
 
Mbona sasa unachanganya ndugu usha sema mwanangu alipatwa na mararia yakapanda kichwani lakini mungu si asumani tukajitahidi kumpeleka hospitali madaktari akapona.ooooo kumbe ilikia mararia kwa hiyo we2 ulilogelezea kwenye mararia uwiiiiiiiiiiiiiii
 
Hapa hatugombani hapa tunaelimishana na pia tunapeana uzoefu.uchawi hata we2 huujui niamini mi2 na pengine kwa bahati mbaya unaamini unajua kitu ambacho hujui,angalia nguvu hii unayo ita we2 uchawi inavyo fanya kazi.uchawi hauna ushahidi uchawi hauonekani uchawi haushikiki uchawi ni vitu vya kufikirika zaidi au kuhisi kama unavyo hisi.watu wote wanao dhulika na nguvu hii ni watu masikini zaidi kuliko wenye uwezo uwezo ninao zungumuzia hapa si fedha tu bali uwezo wa kufiri uwezo kupambanua mambo uwezo angalau hata kudadisi vitu vidogovidogo,lakini pia we ni shahidi wangu ni watu wa aina gani?hudhurika na huo unao ita uchawi?kama hujui fanya hivi fanya uchunguzi nitu wenye uwezo mdogo wa kufikiri ni watu masikini hata kipato ni wavivu hata kwa kufanya kazi.mtu yeyote anae tafta pesa kweli kweke huo ni upuuzi tu tafti zangu zinaonyesha watu wengi wanao dhulika na nguvu hiyo ni watu wenye roho mbaya ni watu walawama kwenye jamii zetu.kinacho wadhuru si uchawi bali ni nguvu waliyo jipandikizia wenyewe kwenye imani zao.ndio maana sisi tusio amini hilo huishi huru na tuko huru na wengi tutawatoa huko
 
Niulize cho2te nitakujibu
 
Back
Top Bottom