Uchawi upo, usidanganywe

Uchawi upo, usidanganywe

wachawi ni mawakala wa shetani na wanajidai wana nguvu nyingi kuliko zile kweli wanazo na ukianza kujihusisha nao ni ngumu kuacha...Mimi binafsi nikulia na kuishi na wachawi, wameua watoto wao kabisa na vijukuu vyao nikiona dawa ya wachawi ni moja tu ni kuwa na imani thabiti katika Chanzo Nguvu ulimwenguni pote Mungu wa Kweli na inategemea ujuzi sahihi na si hadithi zinafundishwa nyumba nyingi za ibada na makelele yasiyo ya msingi

................................
sasa kaeni makofi yametosha!
 
wachawi ni mawakala wa shetani na wanajidai wana nguvu nyingi kuliko zile kweli wanazo na ukianza kujihusisha nao ni ngumu kuacha...Mimi binafsi nikulia na kuishi na wachawi, wameua watoto wao kabisa na vijukuu vyao nikiona dawa ya wachawi ni moja tu ni kuwa na imani thabiti katika Chanzo Nguvu ulimwenguni pote Mungu wa Kweli na inategemea ujuzi sahihi na si hadithi zinafundishwa nyumba nyingi za ibada na makelele yasiyo ya msingi

................................
sasa kaeni makofi yametosha!
Umenena
 
Uchawi ni african chemistry naupenda sana MTU unaenda kwa babu
 
Kingine nilichogundua ni kuwa familia ile iliyo jirani yenu ikipata hii taarifa patakuwa hapakaliki hapo kwenu. Kwa jinsi ninavyowafahamu hao jamaa wa huko, mambo yataanza upya!
Hahaha! Wanajua mkuu, lile tukio halikuwa la kawaida.. So walijua kabisa. Baada ya lile tukio kulikuwa na mtafutano usiokuwa wa kawaida. Bifu bifu
 
Nani anasema hamini uchawii,,,, siku vup vup toka asubuhi kuelekea skuli naona puuh chini kucheki Machawi yupo kwenye ungooo,spidii yakeeee apoo sio mchezo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siwezi kusoma story za kusadikika. Uchawi ni story za kusadikika

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu pengine uko sahihi lakini pia unaweza ukawa hauko sahihi.

Mimi siyo muumini wa uchawi kwa maana ya kwamba sijawahi kushiriki na sina mpango wa kuja kushiriki katika mambo ya ushirikina/uchawi lakini naamini uchawi upo. Kwa hiyo nitakachokieleza hapa chini kisichukuliwe kama vile na mimi ni mshiriki katika uchawi.
1. Miaka ya nyuma nikiwa mdogo niliwahi kuishi kijijini. Pale kijijini kulikuwa na watu kadhaa waume kwa wake waliokuwa wanajulikana sana kwamba ni wachawi sana. Kati ya hilo kundi kubwa kulikuwa na wazee wa kiume wawili na wabibi wawili waliokuwa wakiaminika kwamba ni wachawi zaidi ya wale wengine wote.

Sasa siku moja jioni alikuja mzee mmoja kututembelea kibiashara akitokea mkoa mwingine mbali kabisa na nyumbani na hiyo ilikuwa ni mara yake ya kwanza kabisa kufika pale kijijini. Huyo mzee kabla hata ya kuja tulikuwa tumeshapata habari zake kwamba ni "muike" yaani ambaye kachanjiwa, harogeki na anaweza kujua hata hatari iliyopo mbele yake. Basi yule mzee alipofika pale nyumbani jioni akalala hadi asubuhi. Nakumbuka tukiwa tumekaa nje kwenye kama saa nne hivi asubuhi na yule mzee mara kwa mbali kama mita 30 hivi akatokea mzee wa pale kijijini ambaye ni mmoja wa wale wanaume wawili wanaoaminika zaidi kwa uchawi wao. Ghafla yule mzee mgeni akiwa anatetemeka kidogo akasema kwa kilugha lakini akimaanisha "huyo mtu anaekuja ni mchawi sana!" Kumbuka hapo ni mara yake ya kwanza kufika kijijini na hamjui mtu yeyote pale kijijini zaidi ya sisi wenyeji wake lakini aliweza kumtambua huyo mzee mchawi.

2. Mwaka fulani nikiwa mjini usiku kuna jirani yetu aliingiliwa na majambazi. Ilidaiwa kwamba hao majambazi walikuwa ni watatu ila wawili waliwahi kukimbia na mmoja hakufanikiwa kukimbia baada ya mwenye nyumba yaani jirani yetu huyo kutoka na bunduki na majirani wengine kumzingira. Nakumbuka kuna watu walikuwa wanampiga yule jambazi kwa magongo makubwa makubwa lakini yule jambazi hakuonekana kushituka au kuumizwa na kipigo hicho. Yaani watu wananyanyua juu gongo na wenye roho ndogo tunageuza shingo ili tusishuhudie jinsi hilo gongo litakavyotua kichwani au mwilini mwa jambazi lakini kila linapotua jambazi wala haonyeshi kuumia chochote. Basi kuna wazee fulani na uzoefu wao wakawatonya pembeni wapigaji kwamba inavyoonekana yule jambazi haumii kwa kipigo kile cha magongo kwa sababu atakuwa na hirizi inayompa kinga ya kutosikia maumivu. Wakawashauri ili aweze kupata maumivu basi wachukue vitu laini kama nyasi au mabua ndiyo wampige nayo. Bahati nzuri hapo pembeni kulikuwa na mabua ya mahindi. Wananchi wakang'oa yale mabua na kuanza kumpiga nayo. Mara tu baada ya kupigwa na yale mabua yule jambazi akaaanza kupiga makelele ya kuumia huku damu zikianza kumtoka kila sehemu. Kufumba na kufumbua akawa kaloa damu mwili mzima. Bahati nzuri polisi walifika wakamchukua na kumpeleka kituoni lakini kesho yake tukapata taarifa kwamba amefariki kutokana na kile kipigo cha wananchi.

Kama hizo story mbili zinathibitisha kama kuna uchawi au la sina hakika juu yake.
 
Mkuu pengine uko sahihi lakini pia unaweza ukawa hauko sahihi.

Mimi siyo muumini wa uchawi kwa maana ya kwamba sijawahi kushiriki na sina mpango wa kuja kushiriki katika mambo ya ushirikina/uchawi lakini naamini uchawi upo. Kwa hiyo nitakachokieleza hapa chini kisichukuliwe kama vile na mimi ni mshiriki katika uchawi.
1. Miaka ya nyuma nikiwa mdogo niliwahi kuishi kijijini. Pale kijijini kulikuwa na watu kadhaa waume kwa wake waliokuwa wanajulikana sana kwamba ni wachawi sana. Kati ya hilo kundi kubwa kulikuwa na wazee wawili na wabibi wawili waliokuwa walioaminika kwamba ni wachawi zaidi ya wengine wote.

Sasa siku moja alikuja mzee mmoja kututembelea kibiashara akitokea mkoa mwingine mbali kabisa na nyumbani na hiyo ilikuwa mara yake ya kwanza kabisa kufika pale kijijini. Huyo mzee kabla hata ya kuja tulikuwa tumeshapata habari zake kwamba ni "muike" yaani ambaye kachanjiwa, harogeki na anaweza kujua hata hatari iliyopo mbele yake. Basi yule mzee alipogika pale nyumbani jioni akalala hadi asubuhi. Nakumbuka tukiwa tumekaa nje kwenye kama saa nne hivi asubuhi na yule mzee mara kwa mbali kama mita 30 hivi akatokea mzee wa pale kijijini ambaye ni mmoja wa wale wanaume wawili wawili wanaoaminika zaidi kwa uchawi wao. Ghafla yule mzee mgeni akiwa anatetemeka kidogo akasema kwa kilugha lakini akimaanisha "huyo mtu anaekuja ni mchawi sana!" Kumbuka hapo ni mara yake ya kwanza kufika kijijini na hamjui mtu yeyote pale kijijini zaidi ya sisi wenyeji wake lakini aliweza kumtambua huyo mzee mchawi.

2. Mwaka fulani nikiwa mjini usiku kuna jirani yetu aliingiliwa na majambazi. Ilidaiwa kwamba hao majambazi walikuwa ni watatu ila wawili waliwahi kukimbia na mmoja hakufanikiwa kukimbia baada ya mwenye nyumba au jirani yetu huyo kutoka na bunduki na majirani wengine wakamzingira wakawa wamemzingira. Nakumbuka kuna watu walikuwa wanampiga yule jambazi kwa magongo makubwa makubwa lakini yule jambazi hakuonekana kushituka au kuumizwa na kipigo hicho. Yaani watu wananyanyua juu gongo na wenye roho ndogo tunageuza shingo ili tusishuhudie jinsi hilo gongo litakavyotua kichwani au mwilini mwa jambazi lakini kila linapotua jambazi wala haumii chochote. Basi kuna wazee fulani na uzoefu wao wakawatonya pembeni wapigaji kwamba inavyoonekana yule jambazi haumii kwa kipigo kile cha magongo kwa sababu atakuwa na hirizi inayompa kinga ya kutosikia maumivu. Wakawashauri ili aweze kupata maumivu basi wachukue vitu laini kama nyasi au mabua ndiyo wampige nayo. Bahati nzuri hapo pembeni kulikuwa na mabua ya mahindi. Wananchi wakang'oa yale mabua na kuanza kupiga nayo. Mara tu baada ya kupigwa na yale mabua yule jambazi akaaanza kupiga makelele ya kuumia huku damu zikianza kumtoka kila sehemu. Kufumba na kufumbua akawa kaloa damu mwili mzima. Bahati nzuri polisi walifika wakamchukua na kumpeleka kituoni lakini kesho yake tukapata taarifa kwamba amefariki.

Kama hizo story mbili zinathibitisha kama kuna uchawi au la sina hakika juu yake.
Aisee, uchawi upo mkuu. Ukizaliwa hapo Upanga ukasomea Muhimbili primary, sekondari ukaenda Tambaza then chuo ukaenda UDSM. Bila shaka utaona hizi ni habari za kusadikika
 
Nisaidie namna ya kumpata huyo mganga na me namtu nataka nimfundishe adabu ila me sitaua
 
Back
Top Bottom