Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 269,633
- 697,754
Mojawapo ya dhana zinazotikisa katika jamii yetu ni hii dhana ya uchawi KWAMBA UPO AMA HAUPO!...Na Kwakweli unapoongelea kuhusu uchawi unaonekana mtu usiyeelimika kabisa ama mtu fulani wa kuogopwa
Ndani ya dunia kuna;
1. Ulimwengu unaoonekana
Huu ni ulimwengu wa ithibati za kisayansi, ulimwengu wa formula, ulimwengu wa halisi (sio uhalisia) ulimwengu wa mwili wa nyama.,ulimwengu wa vinavyoonekana kwa macho na kugusika kwa mikono.
2. Ulimwengu usioonekana, ulimwengu usio na ithibati za kisayansi, ulimwengu wa roho, ulimwengu wa nafsi. Ulimwengu wa kiza... Ulimwengu huu ndio injini ya ulimwengu unaoonekana yaani ndio unaoendesha dunia ya sayansi na ithibati
Sina tatizo hata kidogo na watu wasioamini uchawi kama hawamwamini Mungu mmoja (wapagani), lakini nina tatizo na mashaka makubwa na wale wenye imani kamili juu ya Mungu mmoja, muumba wa mbingu na nchi na vyote vilivyomo (ukiwemo uchawi)! Shida yao hii hapa! Aidha wanasoma misahafu yao kwa kukakiriri bila kuelewa, ama wanapotoshwa na wengine.....
Vile vile inawezekana kabisa wengi wanajichanganya kwenye kuamini uchawi kama dhana ya msingi na kuamini waganga wa kienyeji. ...iko hivi unaweza uamini katika uchawi lakini usiamini katika wachawi na waganga wa kienyeji
Maranyingi tumeona wale wasiomini wakitoa changamoto ya kurogwa kama kweli uchawi upo! Huku ni kupotoka kabisa na kukosa uelewa wa mambo..
Kuwepo kwa uchawi ni kitu cha kwanza lakini kuwepo na mtu akaweza kuutumia huo uchawi kwa muktadha fulani ni kitu kingine kabisa
Malumbano mengi pia yametokea kwenye kutaka ithibati za kuwepo kwa uchawi! Hizi ni fikra tengefu..
Ulimwengu wa roho ni software huwezi kuuona kwa macho ya mwili wala kuushika kwa mikono yako...tusichanganye vinavyoonekana na visivyoonekana, tukafanya hiki ndio kile na kile ndio kile
-simu unayo na unafanya mawasiliano yote ninini kinafanyika mpaka umudu kufanya hayo yote?
-Akili unayo na ukiulizwa hutabisha je ukiambiwa ionyeshe utaweza?
-Usingizi unao je kufumba macho ndio kulala usingizi?
Ni vema kuelewa kwama uchawi ni sehemu ya ulimwengu usioonekana, upo lakini hauna ithibati za kisayansi kwakuwa huwezi kuushika nk ....
Kama ilivyo nguvu iliyopo kwenye mashine yoyote ana mwanga kwenye taa yoyote ama software kwenye kifaa chochote cha kielectronic...kama ulivyo uhai ndani ya mwili
Tafakari....!
Jr