Uchawi haupo, ni imani tu

Kutokana na mada yako: nikwambie uchawi upo.


Kwa hakika naona wewe umejiweka kumtegemea Mungu ndio mana huoni madhara wala huoni uchawi wenyewe.


Sisi ambao tumshashuhudia kwa macho kabisa tutakwambia tu uchawi upo.

Unakumbuka hiki kisa;

The LORD said to Moses and Aaron, "When Pharaoh says to you, 'Perform a miracle,' then say to Aaron, 'Take your staff and throw it down before Pharaoh,' and it will become a snake." So Moses and Aaron went to Pharaoh and did just as the LORD commanded. Aaron threw his staff down in front of Pharaoh and his officials, and it became a snake. Pharaoh then summoned wise men and sorcerers, and the Egyptian magicians also did the same things by their secret arts. (Exodus 7:8-11)

Sent from my CPH1803 using JamiiForums mobile app
 
Imani ni nini?

Imani ni hakika ya mambo yatarajiwayo. Ni bayana ya mambo yasiyoonekana. Resubmit!.
Ewaaa!!!!,Kumbe unakubaliana nami kuwa ikiwa utaweka ktk akili yako kuhusu Uchawi basi itakuwa hivyo.
 
Ewaaa!!!!,Kumbe unakubaliana nami kuwa ikiwa utaweka ktk akili yako kuhusu Uchawi basi itakuwa hivyo.

Imani siyo kutaka wewe. Ni hakika na siyo utashi wako. Ni bayana na siyo hisia.
Utake usitake, utaathirika na masuala yasiyoonekana kwa macho. Haijalishi unajua, unapenda, unahisi ama hutaki.
Kikubwa uwe na nguvu ya kuzuia hizo athari hasi maana zipo na haziangalii utashi wako.
 
Unasema yesu ni Mungu na hapohapo unasema Yesu alikufa na kufufuka, swali: Je Mungu anaweza kufa???!!
Ndio maana nimesema hilo ni Fumbo la Imani, Fumbo maana yake ni nini mkuu?
 
Mkuu mpaka ajuue kusoma Lugha hiyo ndipo aelewe.
 
Ngoja nianze kupractice
 
Imani ni zawadi kutoka kwa Mungu,muombe Mungu akujalie zawadi hiyo.
 
Kwa

Soma habar ya mussa, uchawi upo na utaendelea kuwepo.
Nani kakwambia kwamba fimbo ya mussa siku ile ilimaliza wachawi wote?
Iman thabiti, husaidia kuwa kinga na tiba ya mambo ya kichawi.
Ila usishangae, siku moja ukija sikia/ambiwa/shuhudia kuwa hata Padri wako, Baba au Mama mchungaji wako, paroko wako, au Askofu wako ni Mchawi.
Kuna wachawi ukiambiwa huyu ni mchawi, unaweza bisha. Kutokana na status zao kwenye jamii.
Madhara ya kuamini sana uchawi, ni jamii kuwa jinga na maskini.
Indicator mojawapo ya jamii inayothamini sana uchawi ni uwepo kwa umaskini wa kutupa.

#Mshana Jr. anaweza toa maelezo ya ziada hapa.
U
 
Samahanini, ninauliza tu ili kutaka kujua...Hivi unaweza kuwa huamini kama Kuna Uchawi lakini unaamini kwamba Kuna Mapepo??[emoji848]
 
Imani ni zawadi kutoka kwa Mungu,muombe Mungu akujalie zawadi hiyo.


Nnachoona tunatofautiana kwa kuwa hujui maana ya imani.

Kwa kuwa umemtaja Mungu, tuende na Yeye.

Soma hapa:-

Mambo ya Walawi 19:31 inasema: "Msiwaendee wenye pepo, wala wachawi; msiwatafute; ili kutiwa unajisi na wao ..
Mambo ya Walawi 20:6 inasema: "Na mtu yule atakayewaendea wenye pepo, na wachawi, ili kuzini pamoja nao, nitakaza uso wangu juu ya mtu yule, nitamtenga na watu wake.
Kumbukumbu la Torati 18:12 inasema kwamba kuwasiliana na pepo wala mchawi wa wafu ni "chukizo."

Ufunuo wa Yohana 21:8 Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.

IKIWA MUNGU ANASEMA UCHAWI UPO, WEWE UNAPATA WAPI AUDACITY YA KUPINGANA NA MUNGU KWAMBA UCHAWI HAUPO?
 
Tatizo hapa mtoa mada ni mlokole
Anaingiza iman yake ya DINI katika neno uchawi ,,,
Uchawi ni neno lenye tafsiri pana
Hata paulo mtume wa Kristo Yesu aliitwa mchawi kwa sbb alikuwa anacheza na nyoka katika moto na nyoka awakuungua
Watu wakamuita Paulo ni mchawi
 
Mtumishi unasali kanisa gani? hujawahi ona watu wanatolewa uchawi au watu wanatoa shuhuda za kusumbuliwa na nguvu za giza?
 
Alafu kuna mtu Kwa uchache wake wa kutambua nini maana ya Mapepo, ,
Anasema mapepo ni uchawi
Mapepo ni neno la kiswahili( majini)
Wapo majini wabaya na wapo majini wazuri
hii nayo ni mada kubwa
Wakristo wote duniani wanaamini mapepo( majini wote ni mashetwan
Awajui ya kwamba shetwan ni sifa sio kiumbe..
 
Wewe jamaa hujui unachotetea hapa. Uchawi upo kabisa. Tambua kuwa kuna pande mbili kwenye kila kitu, upande wa nuru na upande wa giza. Kama vile ambavyo kuna upande wa Mungu pia kuna upande wa shetani. Kusingekuwa na haja ya kusali kama hakuna uchawi. Kwa maana watu wanasali kumwomba Mungu awaepushe dhidi ya wachawi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…