Unakosea jambo moja la msingi sana: ni kwamba uchawi upo, ila hauwezi kuwadhuru walio na imani katika Yesu Kristo, kama ulivyo wewe. Ukweli ndugu yangu uchawi upo kabisa na ni matumizi ya nguvu za giza kama mapepo, majini nk wakishirikiana na wachawi. Hata wewe leo hii ukimwasi Yesu utalogwa kirahisi. Kwa hivyo usichanganye kati ya kutokuwepo kwa uchawi na wachawi kushindwa kumloga mtu ni vitu viwili tofauti sana. Hata Biblia inazungumzia habari za wachawi kufany miujiza yao ya kichawi kwa kutumia nguvu za giza.