BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,082
Uchawi bungeni wafika Usalama wa Taifa, Polisi
Stella Nyemenohi, Dodoma | June 15, 2008
Ofisi ya Spika imewasilisha taarifa kwa Polisi na Usalama wa Taifa ili washughulikie madai yaliyojitokeza hivi karibuni kuhusu Mbunge na Ofisa mmoja Mwandamizi wa Bunge kukutwa ndani ya Ukumbi wa Bunge wakifanya vitu vinavyodhaniwa kuwa ni ushirikina.
Tukio hilo lililoripotiwa jana na baadhi ya vyombo vya habari, linadaiwa kufanyika Jumatatu wiki iliyopita likimhusisha Mbunge na Ofisa wa Bunge, ambao hata hivyo, hawakutajwa ni akina nani.
Imedaiwa kuwa watu hao walinaswa wakinyunyizia vitu visivyojulikana katika kila kiti cha Mbunge na kuishia cha Spika. Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuahirishwa semina ya
Wajumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi mjini hapa, Spika Samuel Sitta alisema Kamanda wa Polisi mkoani hapa na Usalama wameanza kufuatilia zaidi tangu juzi ili kubaini ukweli wa suala hilo .
Ingawa alisema bado suala hilo ni uvumi na kwamba halina budi kusubiri kukamilika uchunguzi wa vyombo hivyo vya usalama , Sitta alisema hata hivyo tahadhari zote zinachukuliwa katika Ukumbi wa Bunge.
Hata hivyo, alisema kwa upande mwingine, tahadhari zinaweza kuwa ngumu ikizingatiwa kuwa wanaohusishwa ni watu ambao hawana kipingamizi cha kuingia katika ukumbi huo.
Akizungumzia juu ya tukio hilo , Spika alisema, Inashangaza. Lakini ni suala la uvumi, linachunguzwa. Tusubiri RPC na Usalama wa Taifa wakamilishe uchunguzi waotahadhari zote zinachukuliwa, alisema.
Kwa mujibu wa taarifa zilizoandikwa na baadhi ya magazeti, tukio hilo la ushirikina, linadaiwa kufanyika siku moja kabla ya kikao cha kwanza cha Mkutano wa 12 wa Bunge kuanza Jumanne iliyopita.
Spika alisema wakati wa tukio hilo, kamera sita zilizokuwa katika ukumbi huo, hazikuwa zimewashwa. Isipokuwa inadaiwa, kamera moja ya studio ndiyo iliyoonyesha watu hao.
Hata hivyo, Sitta alisema kamera hiyo ilionyesha picha iliyofifia ambayo ni vigumu kubaini wahusika. Hata hivyo, alisema anaamini kuwa ikifikishwa kwa wataalamu, ndiyo watakaoweza kubaini wahusika.
Alipoulizwa na waandishi kuhusu mantiki ya kuhusisha tukio hilo la ushirikina na ugonjwa wa ghafla wa Mbunge wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe (CCM), Spika alisema halihusishwi ikizingatiwa kuwa taarifa za daktari, zilionyesha kuwa alikuwa na uchovu.
Kwa mujibu wa Spika, Dk. Mwakyembe alianza kujisikia anaishiwa nguvu Alhamisi dakika chache wakati akijaribu kuwasiliana na Spika ndani ya Bunge. Alitoka nje ya ukumbi kwa msaada wa Mbunge mwenzake na kupelekwa hospitalini.
Baada ya Mwakyembe kukabiliwa na maradhi hayo ya ghafla, kesho yake (juzi) ulienea uvumi kuwa amefariki. Wakati Sitta alisisitiza jana kuwa afya yake inaendelea vizuri, HabariLeo ilimshuhudia Mbunge huyo jana akiwa katika viwanja vya Bunge katika hali ya kawaida.
Wakati huohuo, semina ya NEC-CCM ilianza jana na inatarajiwa kumalizika leo mjini Dodoma. Kwa mujibu wa Katibu wa Idara ya Itikadi na Uenezi ya CCM John Chiligati alisema miongoni mwa waliotoa mada ni pamoja na Gavana wa Benki Kuu (BoT), Profesa Beno Ndullu.
"Hatujamaliza semina. Inaendelea hadi kesho (leo). Kwa hiyo, maazimio yote yatakayofikiwa, tutatoa taarifa kesho saa 11," Chiligati aliwaambia waandishi na kusisitiza kuwa lengo la semina hiyo ni kuhusu masuala ya uchumi, hususan kilimo.