Uchambuzi wa Press ya Kwanza ya Polepole: Amevuta ushawishi, ameweza kujenga hoja, amefungua mjadala

Uchambuzi wa Press ya Kwanza ya Polepole: Amevuta ushawishi, ameweza kujenga hoja, amefungua mjadala

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2013
Posts
12,151
Reaction score
44,071
Hayawi hayawi sasa yamekuwa, hatimaye Polepole ameweza kufanya press yake ya kwanza na kwa hakika mambo matatu muhimu amefanikiwa kuyafanya.

Jambo la kwanza Polepole amefanikiwa kuvuta ushawishi wa maelfu ya watu kupitia mitandaoni kumfuatilia. Huenda huu ni ushindi mkubwa sana kwake kisiasa. Hakuna siri, kuanzia wanaharakati, makada wa CCM, wapinzani, maafisa waandamizi serikalini , raia wa kawaida na kwenye vyombo vya dola walikuwa busy kusikia neno kwa neno. Huenda matukio mawili yaliyotangulia kabla (kujiuzuru kwako ubalozi na kutekwa kwa dada yake) yanaweza kuwa ni sababu iliyochangia kuvuta hisia za watu wengi kutaka kumsikiliza leo.

Soma > Polepole acharuka: CCM yavunja Misingi, Haki yazimwa, Katiba ilichakachuliwa na Utekaji wazidi kutisha

Jambo la pili, kila mtu aliyemfuatilia leo Polepole atakuwa amemjua vyema kabisa Polepole ni mtu wa namna gani, ametoka wapi na anaelekea wapi na kipi anakisimamia. Kwa ujumla, bila shaka ameeleweka vyema kama ni mtu mwenye historia ya kisiasa yenye mizizi iliyochimbika ndani sana katika CCM na Serikali, na mtu aliyepita viunga vyote muhimu vya juu zaidi vya madaraka, utawala, maamuzi na mikakati ndani ya serikali na CCM, huku akifanikiwa kufanya kazi kwa karibu kabisa na marais watatu, ikiwemo Kikwete, Magufuli na Samia tena katika majukumu yenye viapo vya kisheria vya kutunza siri milele.

Jambo la tatu, Press ya Polepole imefungua mambo mengi kuhusu mwenendo ndani ya Serikali na ndani ya CCM chini ya utawala wa Samia, na Polepole ametufumbua haya;

1. Kwa sasa taifa ni kama halina kiongozi mkuu rasmi (aliyopo ni kivuli??)

2. Wahuni wameshika hatamu ya nchi na CCM huku wakiwa na nguvu na ujasiri wa kufanya chochote bila aibu wala kizuizi.

3. Mambo ya nchi hayaendi sawa karibu kila mahali tangu Samia kushika madaraka. Kwa sababu ya viapo hawezi kufunguka zaidi au kusema kila kitu.

4. Mchakato wa CCM kumpitisha Samia kugombea urais 2025 ni batili kwa 100%, lakini CCM bado kwa sasa inayo nafasi kuufuta ili kufungua mchakato mpya ambao utatoa fursa kwa wanaCCM wengine kuomba kugombea.

5. Ufisadi ndani ya serikali ni mkubwa kupita maelezo na hakuna juhudi zozote kuudhibiti. Mfano hai ukiwa ni ripoti ya CAG kushindwa kufanyiwa kazi.

6. Desturi rasmi ya siri ndani ya CCM hairuhusu baadhi ya watu kupewa nafasi ya kugombea urais (mfano: Waziri mkuu, Spika, Makamu wa rais).

7. Waliomteka dada yake ni wale wale wahuni anaopingana nao, mtandao wao anaufahamu, atapambana kisiasa kuuangamiza.

8. Anachokipigania amewahi kuwashirikisha watu muhimu (akiwemo waziri wa mambo ya nje, waziri mkuu, naibu waziri mkuu, makamu wa rais, wanaCCM wengine waandamizi) lakini walishindwa (wamesita? Kuogopa?) kuchukua hatua.

9. Harakati zake za kupingana na huu mfumo mbovu wa sasa zimewahi kumpelekea kuitwa kujieleza katika kamati za wabunge wa CCM, Kamati za nidhamu ndani ya CCM na kuonywa mara kadhaa na Ndugai kuwa huenda zikagharimu maisha yake!

10. Wapo viongozi wanaCCM waandamizi na maafisa wa juu wa serikali wakiwemo mabalozi kadhaa ambao kimya kimya wanamuunga mkono huku nao wakitaka mabadiliko muhimu ya kimfumo yafanyike ndani ya CCM na serikali.


Ni hayo tu kwa sasa.
 
Muhtasari bomba sana.

Kuna lile alilosema kwamba Sisiemu lazima ianze na viongozi wapya kabisa kwenye uchaguzi huu ili KUIHUISHA chama.

Hii inaingia kwenye hoja yako namba 4 hapo juu.
 
Naona Jf GT ikirudi mahala pale ..mchakato urudiwe, period.
 
Back
Top Bottom