Uchaguzi wa mwaka 2020 tutegemee kuona upinzani wenye hoja dhidi ya ubabe wa nguvu ya dola

SHILLINGS

Senior Member
Oct 24, 2013
160
648
Uchaguzi wa mwaka 2020 tutegemee kuona upinzani wenye hoja dhidi ya ubabe wa nguvu ya dola. Yale mapambio ya kusifia utawala wa Magufuli yatageuka kuwa mapambano ya nguvu dhidi ya maarifa. Ukimya wa CHADEMA una maana kubwa sana kwa mambo yanayoendelea kwa sasa kwenye nchi hii.

Kazi ya inayofanyika ndani ya CHADEMA kwa sasa itatoa mshindo mkubwa ambao utamshangaza JPM na wapambe wake. Tutegemee upinzani wenye mbinu mpya za mapambano ya hoja, hoja zitapanguliwa kwa kwa hoja, tutegemee upepo wa kisiasa nchini utabadilika kwa kasi ya kimbunga.

2020 ni mwaka ambao siasa za nchi hii zinakuwa na taswira tofauti kabisa toka mfumo wa vyama vingi uanze. Yale ambayo wengi wanadhani ni mafanikio makubwa sana katika utawala wa JPM yana siri kubwa sana ndani yake ambayo inakuja kufumuka mwaka 2020. Nawaombea wale makamanda ambao mtaongoza mapambano mwaka 2020 Mungu aendelee kuwajaza maarifa na ujasiri.
 
Back
Top Bottom