Tindo
JF-Expert Member
- Sep 28, 2011
- 61,965
- 108,619
Wanabodi,
Unapotoa ushauri fulani ukapuuzwa, katika ushauri huo ukashauri the right thing to do na matokeo ya kutofuatwa kwa ushauri huo, halafu baada ya kupata matokeo, sasa ndio wanaamka, wanakumbuka shuka kumekucha, na sasa ndio kuanza kujipanga, japo ni kwa kuchelewa lakini ile kujitambua tuu pekee, inastahili pongezi, hivyo hili ni bandiko la pongezi kwa Chadema, the input ya JJ.MNYIKA inakwenda kuonekana.
Nimemuona Mwenyekiti wa Chadema, Mhe. Freeman Mbowe akitembelea jimbo lake na kuhutubia, japo ni kweli kabisa kwa Tanzania, kitendo cha Wenyeviti wa vyama vingine vyote wakizuiliwa kuhutubia wanachama wao national wide, kufuatia ile marufuku batili ya shughuli za kisiasa national wide, wakati ni Mwenyekiti wa chama kimoja tuu, akizunguka nchi nzima na kulihutubia taifa mubashara kwa ile kofia yake nyingine, lakini wabunge wote waliruhusiwa kufanya mikutano ya hadhara kwenye majimbo yao throughout a year, walikuwa wapi siku zote, hadi huu mwaka wa uchaguzi ndio tunawaona wakipishana majimboni, isn't this too little too late, or just better late than never, bora chelewa ufike?.
Jana nimesoma, mkakati wa JJ.Mnyika kuandaa ilani mzuri ya Uchaguzi wa 2020.
John Mnyika, Kibadili chama kutoka chama lalamishi na andaa ilani iliyobebwa na ajenda zenye maslahi kwa watu
This is a good, hatimaye Chadema sasa imeanza kusikia, ingekuwa inasikia tangu enzi zile, saa hizi Chadema zamani ingekuwa Ikulu.
Elections 2015 - Kuelekea 2015: CHADEMA Kuchukua Nchi Kwa Kishindo!... Only If...!
Watu tumeanza kuishauri Chadema tangu 2010...
CCM Imechokwa, CHADEMA Haijajipanga!
Tukashauri
CHADEMA MUST now Reform and Restructure!
Tukashauri
Ushauri wa Bure kwa CHADEMA: Heri Nusu Shari Kuliko Shari Kamili! - Kuepusha Shari, Kubalini Kosa!
Tukashauri
Ushauri kwa CHADEMA: Japo ni Haki, lakini chondechonde Msiandamane. Mwenye Nguvu Mpishe!
Tukashauri
CHADEMA ni sikio la kufa? Iambiwe vipi ili isikie? Masha ana hoja za msingi, zisikilizwe, zizingatiwe, zisipuuzwe!
Tukashauri
CHADEMA Hamkujipanga, hamjajipanga, hamjipangi na hamtajipanga!-2015 ni CCM tena!
Tukashauri
Handling of Serious Security Issues: Kama CHADEMA Takes Things For Granted Kwa Uzembe Hivi!, Jee Ikulu Yetu Wangeiweza?!
Je, CHADEMA inaweza kushinda 2020? Is it serious, credible & mature enough opposition?!.
Hatimaye sasa ndio Chadema inasikia japo kwa kukumbuka shuka kumekucha, Chadema inastahili pongezi za dhati, swali linabaki will this help kwa uchaguzi wa 2020?, or it's too little too late?.
Kwa wenzetu wa ibada nawatakia Ijumaa Kareem Njema,
Kwa sisi wengine, nawatakia Furahi Dei Njema.
Paskali
Paskali acha kuambatanisha hayo mabandiko yako ya zamani, ambatanisha hata mistari ya vitabu vitakatifu, bila tume huru ya uchaguzi hakuna mtu anayejitambua atashiriki huo ushenzi. Siku kukiwa na tume huru ya uchaguzi ndio uje na haya mapamphlet yako kwa cdm.