Uchaguzi ujao ni kizungumkuti nguo kuchanika

X_INTELLIGENCE

JF-Expert Member
Mar 25, 2014
9,680
12,253
Ndugu zangu Watanzania, Kila nikiutazama uchaguzi ujao haki vile nabaki mdomo wazi. Mimi ni shabikia mkubwa sana wa serikali iliyopo madarakani. Nampenda sana Rais SSH. na katika ndoto zangu ninazoota naamini ipo siku nitapeana nae mkono🙆{sijui kama ndoto hii itatimia🤣🤣🤣}

Lakini Kila nikitazama kwenye dira ya mambo yajayo simuoni Rais huyu kama anaweza kuja kutuongoza tena Kwa msimu ujao. Japo mzee toboa tobo alisema kuwa Rais ajae ni Samia. Lakini haki vile CCM nawajua ni mabingwa wa sanaa za kubadili gia angani.

Mimi binafsi simuoni Rais Samia akiwa tena pale kwa msimu ujao. Anaweza akaondoka yeye mwenyewe Kwa kupenda kwani kwajinsi anavyoonekana ni kama amechoka kubeba mzigo tuliomtuisha. UONGOZI tena Urais sio mchezo ndugu zangu.

Uchaguzi ujao utakuwa na mambo mengi ya kustaajabisha inawezekana watu wasijitokeze kabisa kupiga kura.

Inawezekana kijana mmoja wa Marais wastaafu akajitokeza kuwania hiyo nafasi.

Inawezekana pia baadhi ya mikoa kukatokea purukushani za hapa na pale. Kama mnavyo jua uchaguzi unavyo kuwaga.

Chama tawala kipo kwenye hali ngumu sana hivi sasa. Ndani Kwa ndani hawaelewani hivyo ni kama uchaguzi huo utawapa wakati mgumu sana. Nguvu ya chama tawala inajulikana ila kutokana na sababu za hapa na pale haswa ule mpasuko ulioigawa CCM kwenye uchaguzi uliopita na baadhi ya wanachama wenye ushawishi kututoka 🙆😭 chama kimebaki kinaelea.

Uchaguzi ujao unaweza ukawapa nguvu kubwa vyama pinzani. Japo sioni kama watapata nguvu kwani kamata kamata ya upinzi itazidi kusonga mbele.

Kwa upande wa upinza ni kama baadhi ya matukio ya kutisha na kuogofya yalio wahi kuwatokea baadhi ya waandamizi wa upinza, yamewarudisha nyuma hivyo ni kama upinzani wanaogopa...{wanadai upinzani ni CCM "B" 🌟🤣🤣🤣}

Uchaguzi ujao utakuwa mgumu sana. Tuzidi kuliombea Taifa. 🙏🙏🙏

N.b

{Narudia ngoja nifanye kazi kwanza}​
 
Sijaona maoni yako juu ya yanayo endelea sasa. Au asali imekolea yakhe
Mimi ni mdau wa usafirishaji wa transit goods najua adha zilizokuwepo hapo Bandarini kuna kipindi nilienda kutoa Scania r420 nikakuta tachograph imeibiwa nikaambiwa niende kuinunua Tabata dampo.

Uwekezaji hapo bandarini ni jambo zuri sana na nampongeza Raisi wangu mpendwa Samia kwenye hilo.

Kuhusu mkataba kama kuna walakini urekebishwe tu bila kelele
 
Hakuna uchaguzi mgumu, CCM inalijua hilo na Samia akipenda ataendelea bila shida yoyote. Watanzania walio wengi hawajali na hawashtushwi na maswala ya kitaifa, ila ukitaka kujua hasira zao korofisha ligi au mechi ya Simba na Yanga.
 
Nchi yenye azimio lenye tumaini,
Ndiwe peke yako mwanga wa Watanzania,
Ninakuthamini hadharani na moyoni,
Unilinde name nikulinde hata kufa.

Majira yetu haya, yangekuwaje sasa
Utumwa wa nchi, Nyerere ameukomesha X2

 
Back
Top Bottom