Jaji Mfawidhi
JF-Expert Member
- Feb 20, 2016
- 14,047
- 20,411
Sungusia ni nani?
Mbali na uzoefu wake wa zaidi ya miaka 20 kwenye uwakili na kufanya kazi na mashirika mengi ya ndani na kimataifa, Sungusia ni mtu mwenye uzoefu mkubwa kwenye kuendesha taasisi za kijamii ambazo hazitegemei bajeti ya serikali.
Sungusia ni mentor wa mawakili wengi sana na si mchoyo wa kugawa karama zake kwa wengine. Sungusia ni mwaminifu na mnyenyekevu. Sungusia ni mtu mwenye maono na ndiye aliyetoa wazo na kusaudiakutengebeza Strategic Plan ya TLS kwa Mara ya kwanza ambayo bahati mbaya hadi Sasa uongozi umeshindwa kuendelea kureview ili kuendana na mazingira halisi ya Sasa.
Sungusia ni mkufunzi mbobevu katika mambo ya uwajibikaji, utawala bora na kadhalika.
Kwanini Sungusia sasa na siyo kesho?
Ni wakati wa TLS kuacha ubosi na kuwa mtumishi wa mawakili ambao ndio mabosi wake. Ni wakati wa TLS kuwapunguzia mizigo isiyo ya lazima wanachama wake ikiwa ni pamoja na ada za EALS ambazo ni chakula cha watu fulani.
Ni wakati wa TLS kurusidusha mafunzo ya kila mwaka kwa mawakili wachanga ambapo kila mwaka mawakili 50 wslipelekwa kwenye mafunzo kueawezesha jinsi ya kuendesha law firm lakini tangu uongozi wa sasa uingie mafunzo hayapo tena.
Ni wakati wa TLS kuendesha miradi mingi ambayo itanufaisha mawakili pia ambapo toka uongozi huu uingie hakuna donor funded project kabisa.
Ni wakati wa TLS kuhakikisha inawapa ywakilishi wa kisheria mawakili wanaofikishwa Kamati ya Maadili jambo ambalo liliishia awamu ya nyuma.
Ni wakati wa TLS kusimamia nashauri ya maslahi ya umma kwa kutumia funds mbalimbali ili kunufaisha jamii lakini pia mawakili kupata fursa.
Ni wakati wa TLS kuanzisha utaratibu kabambe wa kuboresha mazingira ya practice.
Ni wakati wa TLS kufanya exchange program za mawakili hasa wachanga kwenda nchi nyingine kujifunza kama ilivyowahi fanyika huko nyuma na mawakili walipelekwa China.
Ni wakati wa TLS kuweka utaratibu na miongozo ya uanzishwaji na uendeshashi wa law firm.
Hayo yote yanawezekana kwa kupata kiongozi thabiti na mwenye maono sahihi.
Furahia kazi ya Uwakili chagua Sungusia mtu wa kuaminika.