Uchaguzi Mkuu TFF - 27 Oktoba 2013: Jamal Malinzi Rais Mpya wa TFF!

CHAI CHUNGU

JF-Expert Member
Feb 20, 2012
7,113
930
Kwishney:

- Jamal Malinzi kura 73, Nyamlani 52.

Kwisha habari yake huyu hakimu mla rushwa.

Wakuu bila shaka leo ndio siku iliyokua ikisubiliwa kwa hamu na wadau wa mpira wa miguu Tanzania.

Nini kinaendelea huko?

Maana nimepitia humu ndani sijaona post yoyote inayoelezea updates za uchaguzi Mkuu wa TFF,au siyo leo?

Tunaomba updates please.
Jumla ya wapiga kura ni 127
Uchaguzi unaendelea katika Ukumbi wa Water Front jijini Dar.
Lakini vituko vimetawala na wagombea wamekuwa wakilalama kutokana na maandalizi ya kikao hicho.
Saa 9:00 Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo (Taswa), Juma Pinto anawaambia waandishi kugomea kuripoti uchaguzi kutokana na TFF kuonyesha dharau waziwazi dhidi yao. Waandishi wengine wanaanza kuondoka eneo la tukio.
Saa 7:45 Hali hiyo inatokana na uamuzi wa TFF kuwaondoa katika sehemu husika waliyokuwa wamekaa na wanataka kuwatoa
Saa 7:30 Lakini kuna mvutano mkubwa kati ya Polisi na Waandishi wa habari .
Saa 4:30 Kwa sasa ni mapumziko na wajumbe wakiwemo wagombea wamekwenda kupata chakula cha mchana.

UPDATES:

- Wallace Karia ameshajinadi...
- Makamu wa pili wa rais, Ramadhani Nassib anajinadi mbele ya wajumbe...
- Mwenyekiti wa uchaguzi anamwomba Nassib anadi sera zake na si kuwazungumzia wagombea wengine...
- Madega ametinga shati jeupe na tai nyeusi. Anasema yeye ni Seneta na kazi yake ya uanasheria inampa muda zaidi...
- Madega anasema pamoja na kuwahi kuiongoza Yanga anamtoa wasiwasi Aden Rage kuwa hatoipendelea Yanga..!
- Ajabu ya mkutano mkuu huu ni kuwa hata safari hii Yanga hawakuleta mjumbe mpiga kura. Yussuf Manji jina lake limeitwa lakini hakuonekana. Simba inawakilishwa na Aden Rage... Hivyo wapiga kura ni 126
- Rage anamtania Madega kwa kutaka ufafanuzi wa Useneta wake; wa Marekani au wa Jangwani?
- Madega anasema aliwahi kujiuzuru Yanga kwa uzembe wa uongozi hivyo yeye akichemsha kazi suala la kujiuzulu si halina mjadala
- Wanafuatia Malinzi na Nyamlani: Kaanza Malinzi, anasema sisi wote ni familia ya mpira. Tuyasahau ya nyuma, anamshukuru Tenga. Anazungumzia ilani yake. Anasema iko kwenye Facebook, Twitter na kwengineko... Anaendelea kutoa historia yake
Ndio kura zinapigwa sasa....!!
 
wanasimba wengi wanamuunga mkono Malinzi

Kweli Tz mtu ana uwezekano mkubwa wakuwa ama shabiki wa Yanga au simba.
Lakini Rais wa TFF hatachaguliwa kwa usimba au uyanga wake.
Sifa nyingine ba hasa uwezo ndio kitu muhimu. Tenga kaacha mfumo wa kitaasisi ambao unafunika unazi kwa kiasi kikubwa
 
Japokuwa wote hawafai, ila Nyamlani HAFAI KABISA.
Ni bora Tanzania tukaufuta kabisa mchezo wa soka kuliko TFF ikaongozwa na Nyamlani.

Poor Nyamlani.

Mmmmh, Jamani Nyamlani anachukiwa yaani angejua! hata Fomu asingechukua. Kila kona anapondwa tu, sijui kwa sababu anapigiwa Kampeni na Le Mutuz - KICHWA BOGA
 
hadi sasa uchaguzi bado haujaanza, ila wagombea na wapande wanapita uku na kule wakijichekesha pia kuna harufu kubwa ya rushwa maana wajumbe 70% wote wamefikia landmark hotel ubungo kambi zote ziko pale
 
kuna mchezaji nguli kabisa ananiambia tukitaka soka la Tanzania life tumpe Malinzi, lakn wenziie waliokuwepo nwakampinga sana
 
Uchaguzi unaendelea katika Ukumbi wa Water Front jijini Dar.
Lakini vituko vimetawala na wagombea wamekuwa wakilalama kutokana na maandalizi ya kikao hicho.

Kwa sasa ni mapumziko na wajumbe wakiwemo wagombea wamekwenda kupata chakula cha mchana.
Lakini kuna mvutano mkubwa kati ya Polisi na Waandishi wa habari .
Hali hiyo inatokana na uamuzi wa TFF kuwaondoa katika sehemu husika waliyokuwa wamekaa na wanataka kuwatoa.
 
kuna mchezaji nguli kabisa ananiambia tukitaka soka la Tanzania life tumpe Malinzi, lakn wenziie waliokuwepo nwakampinga sana

Huyo mchezaji analijua soja vema kabisa. Mtajutia kumsapoti Malinzi.
 
source; Saleh Ally Jembe

Back
Top Bottom