Uchaguzi Mkuu huu, CCM wameshinda pambano ila wamepoteza vita

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
13,502
51,098
Uchaguzi umepita, ila consequences za Uchaguzi huu zitaathiri Nchi hii na Chama cha Mapinduzi kwa miaka mingi sana ijayo kwa maoni yangu binafsi CCM imeshinda pambano (japo kwa umafia wa kila aina) lakini imepoteza vita pana, kitu ambacho kitaiathiri Chama hicho na Nchi kwa miaka mingi sana ijayo.

1. Kilichotokea Zanzibar kimepigilia msumari katika muungano wa ridhaa
Hussein Mwinyi hata afanyeje, siyo chaguo la Wazanzibar, Wazanzibari wanajua, Afrika inajua na Dunia inajua!. Huhitaji kuwa Profesa kuona kuwa kilichotokea Zanzibar ni mazingaombwe au kiini macho cha kumlazimisha mtu ajifanye hajaona, lakini wote tumeona kwa macho yetu kilichotokea kule.

Kitendo kilichotokea kule kimewaaminisha Wazanzibar zaidi kuwa Tanganyika ndiye mkoloni wao, na kwamba Tanganyika ndiyo itakayowapangia wa kuwatawala, watake wasitake. Kinachofuata hapo, Wazanzibar wataona siasa ni upuuzi mtupu na kwamba kushiriki chaguzi ni ujinga mtupu, lakini kamwe hawatoacha kutaka kujikomboa kutoka katika makucha ya Tanganyika.

Watafanyaje?, Mimi sijui lakini sioni kwa namna yoyote ikawa ni kupitia mifumo hii rasmi inayotawaliwa na Tanganyika. Sasa hivi Wazanzibari Wapemba kwa Waunguja wameunganishwa na udhalimu waliofanyiwa katika uchaguzi huu, matendo ya Serikali ya Tanganyika yamewafanya kuwa kitu kimoja, wote wanajiona ni victims wa ukandamizaji wa Tanganyika dhidi yao!. Lazima watatafuta namna ya kuwa huru tu, hiyo ndo hulka ya binadamu, Sijui watafanyaje ila inaweza kuwa ni very ugly scenario.

2. Kama Jinsi tukio la Lissu lilivyoisumbua serikali hii, hata uchaguzi huu utaisumbua sana serikali hii kwa miaka angalau mitatu ijayo
Tukio la kupigwa risasi Lissu ni mambo yaliyoipaka matope makubwa serikali hii katika muhula wake wa kwanza wa uongozi, hili tukio ndilo lililomuongezea Lissu mtaji wa Kisiasa, Huruma ya umma ilikuwa kubwa sana kwake, kwa sababu kiukweli umma ulichukizwa sana na kile kitendo.Kilichofanywa katika uchaguzi huu sasa kimeukasirisha umma mara nyingi zaidi kuliko tukio la Lissu kupigwa risasi. Taifa zima lilikuwa nyonge mno baada ya kushuhudia lenyewe michezo ya ghiliba katika uchaguzi ule.

Watu wameona wenyewe tangu mwanzo wa kampeni wapinzani wakiporwa fomu kinguvu, mawakala kuzuiwa kusimamia chaguzi, wameshuhudia uenguaji wa wagombea wa upinzani kibabe, wameshuhudia polisi wakivamia wagombea wa upinzani, kupiga wapinzani mabomu, kura kwenye mabegi, namba za kura za wabunge zisizotally na idadi ya kura za rais wakati watu hupigia kura watu watatu. Yote haya yanawafanya wananchi waone haki yao imeibwa, na hivyo chuki dhidi ya serikali hii kuwa mara nyingi mno. Sioni ni kwa namba gani CCM inaweza kurejesha egitimacy yake kwa umma.

3. Wapinzani wamefanikiwa kupata moral Support ya nje
Mataifa yote makubwa kuanzia Marekani, Uingereza, EU na hata Japan wameonyesha kutoridhishwa na uchaguzi huu. Hii ni victory kubwa kwa kambi ya upinzani, Unapoona Taifa la watu honest kama Japan linaweka question mark kwenye mchakato nyeti kama uchaguzi, basi ujue kuwa uchaguzi wetu umekuwa kituko cha karne. Kwa hiyo hii maana yake ni kuwa Serikali hii itakapikuwa kwenye vikao na wawakilishi wa nchi nyingins, basi wajue tu kuwa mioyoni mwa wale wawakilishi wanakuoneni kuwa ni viongozi msio na uhalali wa umma wenu, hawatakupeni heshima ya kweli, watakuchekeeni tu kwa vicheko feki.

Kilicho positive ambacho kinaweza kuwa ni outcome ya yote haya, ni shinikizo la dhahiri au siri la wahisani kutaka mabadiriko ya msingi katika mifumo ya uchaguzi ya nchi hii. La sivyo, kama tumejipanga kufanya chaguzi kwa staili tuliyoifanya juzi basi tujiandae kuwa tunafinance chaguzi kwa pesa zetu wenyewe ili tuwe huru kufanya utopolo tulioufanya kwenye uchaguzi huu. Lakini hii inaweza kwenda mbali zaidi ikiwemo wahisani kupunguza shauku ya kusaidia miradi tunayowaomba watusaidie

4. CCM haitokuwa na hofu tena ya wananchi kwa sababu haiwategemei wao kukaa madarakani
CCM sasa hivi ni kama wamefikia muafaka baina yao, kuwa mwananchi si lolote si chochote katika mlinganyo wa mamlaka. Ni kama wamejiaminisha kuwa mwenye kumiliki amri juu ya wanaobeba silaha ndiyo kila kitu, wameuchukua msemo wa Mao Tse Tung kuwa Power emanates from the barrel of the gun yaani nguvu za kisiasa zipo katia mtutu wa bunduki.

Sasa haya ni mawazo mafupi sana kwa sababu ili waendelee kushika mamlaka kwa mtindo huu itabidi waendeleze mfumo huuhuu wa kutegemea vyombo vya dola, Lakini kama ikitokea siku wakapata mtawala akajisahau na kutoa chance kidogo kwa demokrasia huo ndo utakuwa mwisho wao, La sivyi kama wakiamua kuwa undavaundava uendelee basi nayo pia itabackfire kwa sababu watapata resistance wasiyoitegemea tu kutoka mlemle wanapodhani wao wana upper hand, na inaweza kuja ghafla wakashangaa kuwa imekuwajekuwaje!.

Na ikitokea hivyo wananchi wataingia mitaani kushangilia kwa sababu hao CCM waliwadharau wananchi, waliwaona si chochote si lolote!. Hatotokea mtu hata mmoja wa kuwafura machozi au kuwasitiri watakapokuwa wanakimbia kama digidigi kutafuta hifadhi!

5. Wapinzani wamejihakishia nafasi ya pekee kwenye mioyo ya wananchi
Nawapongeza wapinzani kwa kutosusia uchaguzi huu, maana wangesusia wananchi wasingeona ni kwa namna gani CCM inavyoweza kwenda that low na kufanya waliyoyafanya. Sasa hivi wananchi wako na upinzani, wako sympathetic nao. Na hili suala la Bunge lote kuwa ni 99% CCM, itawapa picha halisi wananchi kuwa CCM ni chama cha namna gani, miswada itakayopelekwa mle, michango yao, Ahadi walizoahidi, wananchi wanawatazama tu. Kwa hiyo kushindwa kokote kutimiza ahadi, haitokuwa sababu ya wapinzani, bali wao wenyewe. Wananchi wanasubiri kuona ajira milioni 8, Nyongeza za mishahara za wafanyakazi, Bima ya Afya kwa kila mtu. CCM ya sasa japo inaamini haimuhitaji mwananchi ili kukaa madarakani, lakini bado kuna consequences za kutowatimizia wananchi matakwa yao, kelele zinazoudhi nazo pia ni sehemu ya consequence hizo, nazo japo haziui lakini zinakera, na kila mtawala hupenda astaafu kwa heshima au siyo?

Kwa hiyo ninachoweza kusema ni kuwa, uchaguzi huu, jinsi ulivyoendeshwa ni disaster, ni doa zito sana kwa CCM na nchi yetu, huenda ukabadiri aina ya siasa zetu kwa miaka mingi sana ijayo. Watu wamepoteza imani katika chaguzi, Je siasa za baada ya imani hiyo kupotea zitafananaje?, Binafsi sioni, lakini kamwe haziwezi kuwa njema kwa CCM yenyewe na nchi yetu kiujumla!
CCM wameshinda pambano, japo kwa kila aina ya uhuni, lakini kiukweli kabisa wamepoteza vita maana legitimacy yao mbele ya umma kwisha habari yake!
 
Inawezekana wewe ni Tundu Lissu,
Maana unatoa povu sana kuhusu zanzibar
Jibadili sasa wewe uwe Mzanzibali na upige Kura ya ushindi kwa unayemtaka.
 
Kuna wanaccm wanajitapa chama chao kimeshinda kwa kishindo, nasema hivi CCM ilishinda ushindi wa LUSHINDO sio kishindo.
 
Kwa maoni yangu ccm peke bila uwepo wa upinzani itakufa kabisa kwa sababu haiwezi kufanya siasa peke yake,haina inayepingana naye,kipindi hiki ziara za chama hazitakuwepo na vikao vya chama havitakuepo kwa sababu hawatakuwa na mikakati ya kupambana naye,ni suala la muda tu ccm itapotea jukwaani kabisaaa!
 
Hahaha nchi hii HAKUTAKWA NA UCHAGUZI TENA.

Hakuna mwananchi mwenye akili timamu utamwambia akapige kura akakuelewa.
 
Wamejichagua wenyewe Kwa nguvu
Wanajua hawana legitimacy..
Ndo maana hawaogopi tena
 
Wamejichagua wenyewe Kwa nguvu
Wanajua hawana legitimacy..
Ndo maana hawaogopi tena
Kuanzia kwenye kura za maoni ndani ya chama chao, walichagua watoa rushwa, kisha wakawashindisha watoa rushwa kinguvu. Kwa hiyo maana yake ni kwamba sasa bungeni tumepeleka mijitu ya rushwa!. Sasa unaweza kuimagine unapokuwa na Bunge lililojaa watoa rushwa utakuwa na bunge la namna gani?.
Huu ni msiba mzito kwa Taifa!
 
2494093_magu.jpeg
 
Back
Top Bottom