G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,555
- 35,880
Zilikuwa ni kauli za kipuuzi kwa muda wake wa kipuuzi. Tunamshukuru Mungu zimekoma kabisa kabisa.
Mungu akikupa mamlaka usiyatumie kama fimbo kwa kuwa unao uwezo wa kuyatumia kama fimbo na ukapata unachotaka. Tunamshukuru aliyekomesha kauli hii na za aina yake.
Narudia tena "Mungu ni mwema" Nawatakieni wana Kigoma ambapo kuna majimbo mawili ya uchaguzi, uchaguzi mwema usio na vitisho wala mipasho inayotoa jasho na michirizi ya damu yenye michosho!
Kibondo hakukuwa na kipondo vivyo hivyo Mihambwe hakukuwa na ombwe!
----
MATOKEO YA UCHAGUZI JIMBO LA MUHAMBWE
Mgombea wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwenye uchaguzi mdogo wa Jimbo la Muhambwe Dkt. Florence Samizi amepata ushindi katika uchaguzi mdogo wa jimbo hilo baada ya kupata kura nyingi zaidi ya wagombea wengine.
Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Muhambwe, Bw. Diocles Rutema amemtangaza Dkt. Samizi kuwa mshindi baada ya kupata kura 23,441.
Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo Bw. Rutema alisema Dkt. Samizi alifuatiwa na Mgombea wa Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo), Bw. Masabo Julius aliyepata kura 10,847 wakati Mgombea wa Democratic Party (DP), Bw. Philipo Fumbo alikipata kura 368.
Baada ya kutangaza matokeo ya uchaguzi huo Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Muhambwe, Bw. Diocles Rutema alimkabidhi cheti cha ushindi Dkt. Samizi kama inavyoelekezwa kwa mujibu wa sheria za uchaguzi.
Uchaguzi Mdogo wa Ubunge Jimbo la Muhambwe ulifanyika Mei 16 mwaka 2021 pamoja na Uchaguzi Mdogo wa Ubunge Jimbo la Buhigwe katika Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe mkoani Kifoma na Uchaguzi wa Madiwani katika Kata Tano za Tanzania Bara.