Uchaguzi huu October 2015, Ni Mahakama ya Kadhi V/S CCM. (Tutaona nani Mshindi).

MZIMU

JF-Expert Member
Apr 29, 2011
4,057
1,371
Naangalia TBC sasa hivi, Namuona Rais wa Nchi yetu akiongolea suala la kura kwa katiba Pendekezwa. Inaonekana Rais amelishwa maneno mengi ya Uongo kuhusu ukusunywaji wa Maoni ya Katiba hiyo.

Waislamu wote na Taasisi zake walitoa Maoni kuhusu Mahakama ya Kadhi, lakini Sio Jaji Joseph Warioba wala Kundi la Kina Endrew Chenge waliothamini maoni ya Waislamu hao.

Leo Rais ametuthibitishia kua Serekali haita anzisha Mahakama ya Kadhi wala haita igaramia. Jukumu hilo ni la Waislamu wenyewe.

Mimi nimemuelewa sana Muheshimiwa Rais kua, Nyie Waislamu tumewachezea vya kutosha, tumewatumia vya kutosha, tumetumia majina yakiislamu kwa maslahi yetu. Tumewazuga vya kutosha. Imekula kwenu mtajua wenyewe.

Huo ndio uliokua msimamo wa Serekali ya CCM tangu zamani, ila wanapo ona wamebanwa hukimbilia kwa Waislamu na Misikitini kama ilivyokua Uchaguzi wa 2010. Waislamu waliokua wanaswali Msikiti Kichangani ni Mashuhuda ya hili ninalo lisema. Pale Yule Sheikh Kijana Mweupe alipokua akisimama na ijumaa takribani tatu za Mwisho kabla ya Uchaguzi na kuwabadilsha Waislamu muelekeo. Kua tumchague mwenzetu. Je Sheikh Umemuona mwenzetu huyo na kundi lake?

Sheikh Jongo hili tulikwambia. Sasa umeyaona. Sasa tunasubiri yale uliyoyasema pale Msikiti wa Gadafi Dodoma.

Sasa Jukumu la Mahakama ya Kadhi lipo Mikononi mwa Waislamu wenyewe. Haya sasa Waislamu ni Mpambano kati ya Dunia na Akhera.

Kila nafsi itauonja Umauti.

Je tutaendelea kudanganywa na kutumika kama punda kubeba mizigo tusio jua thamani yake.

This October, tutumie kura zetu kwa Maslahi yetu lengo liwe kuwaadabisha walio tusaliti.

SIKU chache kupita baada ya Mkutano wa 19 wa Bunge kumalizika,na serikali kuutupia mbali mswaada wa sheria ambao unaruhusu kuwepo makakama ya Kadhi nchini kutajadiliwa kwenye mkutano huo.

Nayo Jumuiya na Taasisi za Kiislam nchini wameibuka na kutoa tamko zito kwa kuwataka waislam wote nchini kutoshiriki kwenye kura ya maoni ya kupitisha katiba pendekezwa Bunge Maalum la Katiba,kwa madai kwamba serikali haina nia nzuri na waislam nchini kwa kitendo chake cha kukataa kuwepo mahakama ya Kadhi nchini.

Vilevile Taasisi hiyo imewataka pia waislam wote kujitokeza kujiandikisha kwenye Daftari la wapiga kura na kujiandaa kufanya uamuzi mgumu ambao wanasema hajawai fanywa na waislam nchini tangu taifa kupata Uhuru.

Akisoma Tamko hilo lenye kura sita jana jioni kwenye msikiti wa Kichangani uliopo Magomeni Jijini Dar es Salaam ,Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya na Taasisi ya Kiislam nchini Sheikh Mussa Kundesha kwa niaba ya asasi za kiislam 11 zinazounda umoja huo na kushuhudiwa na Mamia ya waumini wa dini hiyo pamoja waandishi wa Habari ambapo Sheikh Kundesha alisema-

Waislam wote nchini wamechoka na uonevu wanaodai kufanyiwa na Serikali iliyoko madarakani kwa kitendo cha kuondo Mswaada wa Mahakama ya kadhi Bungeni ambapo alisema ni kuendelea kuchochea vita ya kidini nchini.

"Kuna kila sababu ya kuamini kuwa Serikali ya CCM imeshindwa kulishughulikia suala la mahakama ya Kadhi katika uhalisia wake kama ilivyoahidi kupitia ilani yake kwenye uchaguzi ibara ya 108 (b) mwaka 2005 na sasa inafanya hadaa za kisiasa kuwadanganya waislam ili waonekane inalishughulikia suala la mahakama ya Kadhi kama walivyoahidi"

"Kwa ubabe huu wanaotufanyia waislam sasa tunawaomba waumini wote wa kiislam nchini kutoipigia kura katiba pendekezwa kwasababu sio katiba nzuri kwa waislam harafu tunawataka kila mmoja aliyetimiza miaka 18 ajiandikishe kwenye Daftari wa wapiga kura kujiandaa kufanya uamuzi mgumu ambapo utalitikisa nchi"alisema Sheikh Kundesha.

Alisema kuwa kitendo cha Serikali kuwatambua Makadhi wa Bakwata pamoja wanachosema ni ‘Mahakama hewa ya Kadhi' chini ya Bakwata ni kinyume na Katiba ya nchini ibara 19(1) na (20) kwa kuwalazimisha waislam wawe chini ya Bakwata ambapo wanasema hawatakubaliana nalo.

KUHUSU TAMKO LA MAASKOFU.
Pia katika Tamko la Taasisi hiyo kiislam ambapo litasomwa kila msikiti Ijumaa wiki hii nchi nzima pia wamezungumzia Matamko mawili yaliyotolewa Jukwaa la kikiristo nchini ambapo Taasisi hiyo ya Kiislam wameonyesha masikitiko yao kwa kusema ni dhahili hapa nchini kuna serikali dhaifu kwa kuwaacha maaskofu kutoa matamko ambayo wanadai ni ya kichochezi.

"Ushahidi kwamba ni chuki tu husda ni pale ambapo hata waislam tuliopendekeza mahakama ya Kadi iwekwe kwenye Katiba pendekezwa,lakini tunashangaa hawa maaskofu wamekuwa wakiipinga Mahakama hii wakati hii dini tofauti na y a kwao na sisi waislam tumewavumilia lakini tunahoji hawa maaskofu wanataka nini"

KUHUSU KESI ZA MASHEIKH NA KUNYIMWA DHAMANA.
Pia Taasisi ya Kiislam wameonyesha kuchukizwa kwa kitendo cha Masheikh mbalimbali akiwemo shehe Ponda ambao wapo mahabusu na kunyimwa Dhamana na Serikali ila wanashangaa kitendo cha Serikali kuwamwachia Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Askofu Josephat Gwajima wanadai kitendo hicho kinaonesha Serikali kuwapendelea wakristo.

"Masheikh mbalimbali wako mahabusu wakinyimwa Dhamana bila sababu za msingi kwa kesi za uchochezi au kwa kisingizio cha Ugaidi wakati huo huo tumeshuhudia Maaskofu wakitoa kauli za uchochezi pasina kuchukuliwa hatua yeyote ikiwemo sakata la Askofu Gwajima"

KAMPENI WANAO DAI KUUA MADRASA.
Pia Taasisi hiyo wamezungumia kitendo cha Serikali kuwakamata wa Mashehe mbalimbali wanaowafundisha watoto majumbani kwa madai ya serikali kutofuata taratibu za mafunzo likiwemo matukioa tofauti yaliyotokea mkoani arusha-

Kwa kusema ni wazi serikali imejitosa kuua madrasa nchini.

"Lakini Takriban mwezi mmoja sasa,njama hizi za kuua madrasa zetu zimeibuka kwa kasi kubwa na nguvu kwa kuendesha kamatakamata ya waalimu wa madrasa zao katika hali duni majumbani mwao wakifundisha Quran na mafunzo mengine ya Uislam kama tulivyoshudia huko mkoan Moshi na Arusha"

"Tunataka Serikali itusaidie kufundisha Elimu ya dini ya Kiislam kwa mujibu wa sheria ndiyo ipi,sheria hiyo ilipitishwa lini na Bunge lipi?kwa mujibu wa Katiba ya nchi ibara 20 (1) kazi ya kutangaza dini ni suala binafsi,iweje sasa Serikali inakuja na madai haya ya kufundisha dini kinyume na Sheria kwa walimu wetu wa madrasa"

Chanzo:
FullHabari Blog

Kwa hiyo Mahakama ya Kadhi ni Chama siku hizi? Itapambana vipi na CCM?Sijaelewa heading yako mleta mada
 
Naangalia TBC sasa hivi, Namuona Rais wa Nchi yetu akiongolea suala la kura kwa katiba Pendekezwa. Inaonekana Rais amelishwa maneno mengi ya Uongo kuhusu ukusunywaji wa Maoni ya Katiba hiyo.

Waislamu wote na Taasisi zake walitoa Maoni kuhusu Mahakama ya Kadhi, lakini Sio Jaji Joseph Warioba wala Kundi la Kina Endrew Chenge waliothamini maoni ya Waislamu hao.

Leo Rais ametuthibitishia kua Serekali haita anzisha Mahakama ya Kadhi wala haita igaramia. Jukumu hilo ni la Waislamu wenyewe.

Mimi nimemuelewa sana Muheshimiwa Rais kua, Nyie Waislamu tumewachezea vya kutosha, tumewatumia vya kutosha, tumetumia majina yakiislamu kwa maslahi yetu. Tumewazuga vya kutosha. Imekula kwenu mtajua wenyewe.

Huo ndio uliokua msimamo wa Serekali ya CCM tangu zamani, ila wanapo ona wamebanwa hukimbilia kwa Waislamu na Misikitini kama ilivyokua Uchaguzi wa 2010. Waislamu walikua wanaswali Msikiti Kichangani ni Mashuhuda ya hili ni nalo lisema. Pale Yule Sheikh Kijana Mweupe alipokua akisimama na ijumaa takribani tatu za Mwisho kabla ya Uchaguzi na kuwabadilsha Waislamu muelekeo. Kua tumchague mwenzetu. Je Sheikh Umemuona mwenzetu huyo na kundi lake?

Sheikh Jongo hili tulikwambia. Sasa umeyaona. Sasa tunasubiri yale uliyoyasema pale Msikiti wa Gadafi Dodoma.

Sasa Jukumu la Mahakama ya Kadhi lipo Mikononi mwa Waislamu wenyewe. Haya sasa Waislamu ni Mpambano kati ya Dunia na Akhera.

Kila nafsi itauonja Umati.

Hongera Rais Kikwete kwa kuweka mambo bayana. Long live my President
 
Mbona mchokozi hivi MZIMU! Wewe kweli ni Mzimu, Maneno gani tena haya?

"Mimi nimemuelewa sana Muheshimiwa Rais kua, Nyie Waislamu tumewachezea vya kutosha, tumewatumia vya kutosha, tumetumia majina yakiislamu kwa maslahi yetu. Tumewazuga vya kutosha. Imekula kwenu mtajua wenyewe"

Acha ujinga wako. HAKIKA HUU NI UPOTOSHAJI NA NI UCHONGANISHI AMBAO MSINGI WAKE HAUNA NIA NJEMA KWA WATANZANIA NA NCHI YAO.

Jamani kama ni wasikilizaji, watazamaji na wafuatiliaji wazuri Rais Kikwete jana alizungumza na Kamati ya Amani ya Viongozi wa Dini ya mkoa wa Dar es Salaam ambapo alisema amesikitishwa na tamko la Jukwaa la Wakristo Tanzania, linalowahamasisha waumini wao kupigia Katiba Inayopendekezwa kura ya Hapana.

Akifafanua suala la Mahakama ya Kadhi, Rais Kikwete alisema Serikali ina msimamo wa mambo mawili katika mahakama hiyo.

Kwanza, alisema Serikali haina mpango wa kuianzisha na kuiweka katika Katiba na pili, haihusiki kuiendesha na badala yake, Waislamu wenyewe ndio watakaoiendesha kama wataihitaji.

Kwa msingi huo wa sehemu ya haotuba ya Mhe. Rais jana ndiyo maana katika Katiba Inaypoendekezwa kuhusu masuala ya dini inasema “Uhuru wa imani ya dini Ibara ya 41. (2) Kazi ya kutangaza dini, kufanya ibada na kueneza dini itakuwa ni huru na jambo la hiari kwa mtu binafsi ilimradi hakiuki sheria za nchi. Na (3) Shughuli ya uendeshaji wa jumuiya za dini itakuwa nje ya shughuli za mamlaka ya Serikali”.

Asante Mhe. Rais kwa ufafanuzi huo maana humu JF watu wachache wanawahadaa wenzao kwa kuwa wanaweza kusema na kushawishi, WASOMAJI WA JF WATU WANAOTOA MAELEZO YA KUWAPOTOSHA WENGINE HAWANA NIA NJEMA NA NCHI YAO. TUJENGE NCHI YETU KWA MANUFAA YA SASA NA VIZAZI VIJAVYO USIJIFURAHISHE KWA KUANDIKA TU TAMBUA UNAWEZA KUANGAMIZA NA KUWAPOTOSHA AMBAO WANAAMINI BILA KUFANYA UTAFITI.
 
Hilo jina lako na unachoandika havina tofauti, huwezi kumkejeli Rais kiac hicho kwani sio mjomba yako yule, uwe na hekima na busara na uungwana.

Acha kujificha kwenye kivuli chako Juha wewe. Soma uwelewe nini kimeandikwa.
 
Mbona mchokozi hivi MZIMU! Wewe kweli ni Mzimu, Maneno gani tena haya?

"Mimi nimemuelewa sana Muheshimiwa Rais kua, Nyie Waislamu tumewachezea vya kutosha, tumewatumia vya kutosha, tumetumia majina yakiislamu kwa maslahi yetu. Tumewazuga vya kutosha. Imekula kwenu mtajua wenyewe"

Acha ujinga wako. HAKIKA HUU NI UPOTOSHAJI NA NI UCHONGANISHI AMBAO MSINGI WAKE HAUNA NIA NJEMA KWA WATANZANIA NA NCHI YAO.

Jamani kama ni wasikilizaji, watazamaji na wafuatiliaji wazuri Rais Kikwete jana alizungumza na Kamati ya Amani ya Viongozi wa Dini ya mkoa wa Dar es Salaam ambapo alisema amesikitishwa na tamko la Jukwaa la Wakristo Tanzania, linalowahamasisha waumini wao kupigia Katiba Inayopendekezwa kura ya Hapana.

Akifafanua suala la Mahakama ya Kadhi, Rais Kikwete alisema Serikali ina msimamo wa mambo mawili katika mahakama hiyo.

Kwanza, alisema Serikali haina mpango wa kuianzisha na kuiweka katika Katiba na pili, haihusiki kuiendesha na badala yake, Waislamu wenyewe ndio watakaoiendesha kama wataihitaji.

Kwa msingi huo wa sehemu ya haotuba ya Mhe. Rais jana ndiyo maana katika Katiba Inaypoendekezwa kuhusu masuala ya dini inasema "Uhuru wa imani ya dini Ibara ya 41. (2) Kazi ya kutangaza dini, kufanya ibada na kueneza dini itakuwa ni huru na jambo la hiari kwa mtu binafsi ilimradi hakiuki sheria za nchi. Na (3) Shughuli ya uendeshaji wa jumuiya za dini itakuwa nje ya shughuli za mamlaka ya Serikali".

Asante Mhe. Rais kwa ufafanuzi huo maana humu JF watu wachache wanawahadaa wenzao kwa kuwa wanaweza kusema na kushawishi, WASOMAJI WA JF WATU WANAOTOA MAELEZO YA KUWAPOTOSHA WENGINE HAWANA NIA NJEMA NA NCHI YAO. TUJENGE NCHI YETU KWA MANUFAA YA SASA NA VIZAZI VIJAVYO USIJIFURAHISHE KWA KUANDIKA TU TAMBUA UNAWEZA KUANGAMIZA NA KUWAPOTOSHA AMBAO WANAAMINI BILA KUFANYA UTAFITI.

We dada. Sio watu wote ni wajinga kama wewe!
 
Wakati Nyaraka zinasambazwa Makanisani katika uchaguzi wa 2010, CCM walikimbilia Misikitini na kujinusuru. Na kweli hiyo karata imekua ikiwasaidia tangu zamani. Not any More. You will see. Mark My words. BAKWATA, haiwakilishi Waisalamu kabisa zaidi ya wale Masheikh bora liende nipate tonge Mdomoni.
 
We dada. Sio watu wote ni wajinga kama wewe!

Umezidi bwana! Ebo! Acha kutuchanganya na mambo yako yasiyo na msingi. Ujinga wako peleka huko hapa ni majadiliano yenye hoja natija kwa nchi yetu. Acha tabia zako tena kalale kama umechoka. Tena mjinga kabisa. Kweeeeeeendaaaaaa!
 
Mhhh! Hapo ndio Mwisho wako! Haya wapishe wenye kujua waje wajadili.
 
Inawezekana macho yako hayaoni tena vua miwani, mi humu nipo kuelimisha watanzania na wenye mapenzi mema na nchi yao na hatima ya Tanzania hasa kuhusu mambo ya kijamii.
 
Tunaitaka iyo mahakama lkn hamna atakayeenda bal watakula ela kwa hal ya sasa n mwanamke gan atakaye kubal kua chin ya mwanaume wanahitaj n mrad wa kupga ela uo
 
Mhh! Haya na wewe hoja yako ni ipi?
 
Huyu Mzimu ana boa sana.Nadhani wachunguzi wamfuatilie inawezekana siyo mtanzania huyu.Waislam wenyewe wenye akili nzuri hii mahakama ya sharia hawaitaki sasa wewe ni Nani mpaka ujifanye una uchungu sana?una boa mno.
 
Kweli kabisa wala haeleweki nahc anaweza kuleta chuki baina ya watu.
 
Huyu Mzimu ana boa sana.Nadhani wachunguzi wamfuatilie inawezekana siyo mtanzania huyu.Waislam wenyewe wenye akili nzuri hii mahakama ya sharia hawaitaki sasa wewe ni Nani mpaka ujifanye una uchungu sana?una boa mno.

Mzimu anajitahidi kupotosha kweli. Labda anataka kuonekana mwema lakini ni sawa na kung'ata na kupuliza ambayo ni hatari kwa mustakabali wa Taifa letu. Hongera KgHM kwa kuliona hilo.
 
Huyu Mzimu ana boa sana.Nadhani wachunguzi wamfuatilie inawezekana siyo mtanzania huyu.Waislam wenyewe wenye akili nzuri hii mahakama ya sharia hawaitaki sasa wewe ni Nani mpaka ujifanye una uchungu sana?una boa mno.

Acha unafiki waislamu wanaitaka.
 
Back
Top Bottom