kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 17,189
- 16,867
Iko siku wanaume wataonekana hawana jema hata moja walilotenda jana, leo na hata kesho kama tutachagua wanaharakati wa jenda. Mimi mwalimu wangu mkuu katika somo la uumbaji ni viumbe wengine ambao siyo binadamu.
Kwakuwa Mungu ndiye aliyetuumba sisi na viumbe wote bila shaka kuna vitu na tabia amekusudia viwe sawa kwa viumbe wote na viumbe wote wa jinsia moja. Kwakuwa viumbe wote wanahitaji hewa, maji, chakula, kuzaa, kusogea, kwenda haja ndogo na kubwa na wanahisi joto, baridi na maumivu basi Mungu alitenda sawa kwa viumbe wote na tofauti ndogo sana kwa kazi maalumu.
Mimi nimefuga sana njiwa, kuku, bata, mbuzi, ng'ombe na mbwa. Nimechunga sana na kuwahudumia wanyama hawa tangu utotoni mpaka nikajifunza vitu vingi sana juu yao kiasi kwamba nilikuwa nikijirekebisha tabia yangu kwa kuwaangalia wanyama na ndege wanafanya na hawafanyi nini kwenye matukio tofautitofauti.
Sikuwahi kuona dume la mnyama, wala ndege, wala mdudu linalotunza wanawake. Wanawake wetu wanataka watunzwe na wanaume.
Picha tunayojengewa jamii hivi sasa ni ile ya wanaume ni wabaya sana, siyo wazuri, ni makatili, ni wezi, hawajui, hawana uchungu wala huruma, ni matajiri kuliko wanaume, wanapiga wanawake, wanadhulumu wanawake, hawafai, hivyo hawastahili hiki na kile. Kama jambo likisemwa sana mwinshowe inageuka kanuni, sheria na tabia.
Mbona hivi wanaume wanavyoishi na wake zao ndivyo hivyo na wanyama na ndege wanavyoishi na wanawake zao? Mimi sijawahi kuona jogoo anakwenda kumsaidia mkewe kuatamia mayai, wala kumpelekea chakula pale kwenye kiota.
Sijawahi kuona beberu anaruhusu beberu mwingine anatembea na mkewe akamuacha hivihivi. Sijawahi kuona kuku, ng'ombe, simba, mbwa wanaruhusu uchezee watoto wake kipumbavu lazima watakufanyia jambo ujue kuwa wanauchungu na watoto wao.
Lakini pia sijawahi kuona jike la kuku, simba, mbuzi , ng'ombe, nyati, mbwa, nzige, nyuki mkali linakataza mume wake asitembee na majike wengine kwenye kundi.
Mbona wanaume sisi tukiyafanya haya tunaonekana mabaladhuli tunaoonea wanawake? Kwanini sisi tunae Mungu wetu peke yetu na wanyama wana wa kwao?
Mwaka 2025 tunataka viongozi ambao wanawatendea haki wanaume kwa mujibu wa maumbile ya mwenyezi Mungu. Tuepuke wanaharakati wasiyopenda wanaume au wanawake, kila jinsia ipate haki yake kwa mujimu wa maumbile na makusudio ya muumbaji. Wanyama ndiyo wawe walimu wetu kwenye mambo ya jenda.
Kwakuanzia usichague mgombea ambae Hana mke, Hana mume, wametengana, ametelekezwa au anatumza watoto peke yake. Kiongozi wa hivi atalalia upande TU, atahamishia ugomvi wake upande ulee wenye ugomvi nae.