Uchaguzi 2010: Zitto, Mbatia wajitosa Ubunge!

Zito kugombea popote ruksa kwani ni haki yake ya kikatiba hivyo siyo habari kwangu, agombee asigombee yote sawa, nilikuwa namuadmire kama political role model wangu kwa vijana lakini tayari amereveal true color yake,ni mchumia tumbo tu kama walivyo wapinzani wengine waliomtangulia,akina Masumbuko Lamwai,Hiza Tambwe,Kaborou,Msabaha na wengine wa jamii hiyo.
 
ccm nao wana roho mbaya kweli,wameenda kumminya huko jimboni mwake kwa style ile ya divide and rule,mtu aliyekubaliana na baadhi ya sera zao ie mitambo ya dowans?Ama hilo la wapiga kura 15,000 is a none issue?

Wapinzani kama ni kweli wanataka kuliimarisha bunge basi wasiangalie sana sababu binafsi kwenye maamuzi yao,certainly Mh Zitto anaweza akapendelea jimbo la Kinondoni zaidi maybe kwasababu ni karibu na shughuli zake nyingine,labda za binafsi.

Licha ya kwamba sina uhakika wa moja kwa moja,lakini my best bet is wananchi wa hayo majimbo mengine kama Geita,Kigoma nk wana shida kubwa zaidi na za msingi kuliko za hao wa Kinondoni...Kwenda kwenye majimbo hayo certainly ni kujitolea zaidi,hata hivyo pia ni muhimu kuzingatia idadi ya wabunge wa upinzani bungeni kuliko individualism,yani kubakia kusingle out individuals bila kujali si jambo la busara,kwasababu idadi pia ni muhimu especialy pale inapokuja kupitisha bajeti,miswada nk.

Kwa upande mwingine inaoneka pia kama kuna some sort of scramblin amongst the oppositions,Mbatia na Mdee huko Kawe,hapo ndipo utashangazwa na nia halisi ya baadhi ya watu kuutaka ubunge,ether ni ubinafsi ama nia halisi ya kuwatumikia wananchi,yes una haki ya kugombea popote,lakini strategically,what really are they trying to accomplish?kama hakuna any type of collectivism hawataenda popote.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Nimeunda kamati ya uchunguzi (Exploratory Committee) ya watu watatu kwa ajili ya kufanya utafiti wa kina juu ya jimbo gani nigombee Ubunge katika uchaguzi Mkuu wa Mwezi Oktoba mwaka 2010.

So hiyo kamati mheshimiwa unailipa wewe au chadema au CCJ??

Ninatarajia kutangaza rasmi Jimbo nitakalogombea Ubunge mnamo siku ya Jumapili tarehe 28/3/2010.
Naomba ifahamike kuwa bado sijafanya uamuzi rasmi na kwamba uamuzi wangu utazingatia taarifa ya uchunguzi, ushauri wa viongozi wa chama changu (CHADEMA) na matarajio yangu ya kisiasa ya baadae. Ni muhimu kusisitiza kuwa nikiwa Mtanzania nina haki ya kugombea Ubunge mahala popote nchini.
Mheshimiwa uliwahi kusema kuwa Siasa sio chaguo lako la kwanza, we need your comments on this matter,Siasa sio sehemu ya kupumzikia

Uamuzi wowote nitakaoutoa utazingatia kwa kiasi kikubwa sana umuhimu wa kujenga mfumo imara wa demokrasia ya vyama vingi na hasa kuwa na Bunge imara lenye wabunge wengi wa kambi ya upinzani.
Tumeskia unataka ku join CCM,if yes so hiyo ndoto hapo juu itatimia kweli au ndo vile u kalumekenge wa wadanganyika
 
Mkuu alama zote hizo za kuul;iza za nini? yale maamuzi mazito alisema atafanya ndio haya? Au ilikuwa ni baridi ya hapa Germany?
Tumeskia unataka ku join CCM,if yes so hiyo ndoto hapo juu itatimia kweli au ndo vile u kalumekenge wa wadanganyika
 
Ni muhimu kusisitiza kuwa nikiwa Mtanzania nina haki ya kugombea Ubunge mahala popote nchini
Ingawa mimi sishabiki wa Zito...................!
lakini nakuunga mkono kuwa UNAHAKI YAKUFANYA utafiti wa kina kuamua hatima ya ushiriki wako kisiasa hapa Tanzania.

lazima uwe mwangalifu sana, maana hata uswahiba wako na CCM unaanza taratibu kukutumbukia nyongo, wamekuchezea mchezo kuimega hiyo kata ya ,wadinga, nasikia ni mahala ulipozaliwa.

kweli fanya ufafiti wa kina, Na Mungu akusaidie, ila beware with CCM , hawana rafiki wakudumu pale
.
 
Jambo jema kufanya study kabla ya kufanya maamuzi. Ila nivyema aweke na mikakati ya kuweka mrithi (succession plan) au wagombea mbadala katika hayo maeneo anayosema anakubalika na wananchi wanamwomba aende kule.Kwa kuzingatia dhima nzima ya kukuza upinzani na kuhakikisha tunaendelea kuongeza idadi ya wapinzani bungeni. Nitoe tahadhari tena katika hili maana inawezekana kikawa chanzo kingine cha migogoro ndani ya chama. Ni vyema mchakato wa kumpata mgombea kichama ufuatwe. Maana wameshakua wawili ndani ya chama wanaoliwania Kinondoni ( Suzan na Zitto(iwapo utafiti wake utamfavor). isitokee mmja kama kawaida akahisi yeye ndo anastahili na mwingine hastahili. Maamuzi na michakato ya kupata mgombea kwa katiba na kanuni za chama vifuatwe na kila mgombea ajifunze kuelewa na kuheshimu maamuzi ya chama.
 
all the best ..huko Kigoma kwao inakuwaje ?
Bana siasa zetu si hasa, watu waanangalia mkate wao wakila siku, Zitto na wenzake hawana vision kwanini aligombea Ubunge kuwawakilisha wanakigoma wale,anachopaswa kutueleza, mission yake ilikamilika, sasa anataka kwenda jimbo lingine kupeleka maendeleo.....

Mtu anaibuka anataka kuja mjini kugombea.....kwani lazima uwe mwanasiasa....?
 
huyu kijana kwisha habari yake................. ni miujiza tu ndiyo inayoweza kumrudisha bungeni...................

mipango yake imevuja ndo maana magazeti yaliandika mpango huu kabla hajausema............. mara anamsapoti kafulila kgm kaskzn na kumpa magari (aliyoyapata kifisadi) kumsaidia kampeni............. halafu leo anasema kati ya majombo anayoyafikiria ni pamoja na kigm kaskzn!!!!!!!!!!!!!!!!!......... anataka akagombane na kafulia (nccr) na yryr (chdm)................. mmh, hapa kuna habari ya kitoto sana............... huyo kishakataliwa huko kgm kaskzn na nec imemaliza kwa kuitoa mwandiga na kuipeleka kgm mjin................. kwisha kabisa huyu dogo...........

ccm walimlia taiming zammani, wakamwonjesha ladha ya pesa za bila jasho....... akawehuka........... akanyea kambi yake iliyomtoa mavumbini (chdm)................. sasa mara anaunda timu (posho anazowapa si za kifisadi??????????, zinakidhi matakwa ya muswada mpya wa fedha za uchaguzi???????????)........... huyu ndiye mBunge wa kwanza kutangaza kwenye vyombo vya habari kutoa takrima uchaguzi huu................ HII NAYO NI REKODI YA AINA YAKE.............

upuuuzi upuuzi upuuuzi............. akishindwa uchaguzi wansheria watamlia dili watamkonvince akate rufaa wale hela zilizosalia halafu akimwagwa kotini.............. ATAENDA KUOMBA KAZI KWA MAKAMBA..................... HUYU SI MWANASIASA................ ANA MAMBO YA KITOTO SANA.................NASHANGAA ETI ANASHABIKIWA NA WATANZANIA!!!!!!!!!!!!!!!!..................... AAH, INAUDHI SANA.............

asubiri miujiza....................... kwani bongo nako miujiza haiishi...........

sasa fikiria dogo alivyochoka na bado ni katibu mkuu msaidizi wa chadema?? teh teh teh
sasa hicho chadema vipi? kama kiongozi wake wa juu kachoka namna hiyo?
 
Hizi chuki binafsi bwana, iliyobaki kunywa tindikali tu maana unatia huruma.
 
Zitto,
Kama hayo yanatoka rohoni kabisa, basi hapo kuna tatizo. Siamini kama ktk siasa kuna mwenye umaarufu kiasi cha kuwa huru kuzunguka majimbo kiasi hicho.

At your age, I can see the bad station where you are likely to be in the next10 years.
 
...pamoja na kuwa dhamira ya kugombea ubunge ni ya kibinafsi zaidi lakini kwa mapana ni msukumo aliokuwa nao mgombea juu ya changamoto za kuleta maendeleo mahali fulani. Na msukumo huu hauji ghafla kama mwivi avamiapo mahali fulani (ingawa yeye mwizi hupanga).

Sasa hili suala la kufanya feasibility study kujua ni jimbo gani atagombea, na pia kuweka wazi kwa wananchi kabla ya kuchagua jimbo la kugombea, nadhani si njia nyofu kwa mbunge huyu mtarajiwa na nitatoa sababu:
i) Mwananchi wa jimbo lolote kati ya hayo ambapo Zitto ataamua kugombea (ukitoa Kigoma Kaskazini) wataona Zitto anawatumia kama mgongo wa kisiasa, na si mtetezi wa dhati wa changamoto zao
ii) Sijawahi kusikia mahali popote kwa mbunge kufanya feasibility study publicly. Huwa wanafanya kimyakimya na wanapojitokeza huonekana kweli wamedhamiria kupigania maendeleo ya jimbo husika. Na hata kama imewahi kufanyika mahali fulani, mgombea lazima atakuwa kwenye lose-lose situation.
iii) Pia inaweza kuleta mgongano wa kimaslahi katika chama chake, kwa kuwa nina imani, kuna watu tayari wamesha earmark hayo maeneo mengine (ukiachia Kigoma Kaskazini).

Ukiachilia sababu hizo, ninakubaliana naye kimsingi kabisa kuwa kama mtanzania, ana haki ya kujitosa kugombea nafasi ya ubunge mahali popote. na kwakuwa dhamira yake pana ni ya kitaifa zaidi, yaani ukiwa mbunge huongelei, hupitishi miswada ya jimbo lako pekee. Unakuwa pale kwa manufaa ya taifa zima.

Labda nimtakie kila la heri kwa zoezi hilo, lakini pia asisahau angalizo lile pale juu.

Nimeipenda hii analytical thinking yako Mkuu.Nitakutafuta uwe campaigning strategist wangu mwaka 2015!
 
Kigoma mjini ni moja ya ngome za CHADEMA Tanzania ambayo haitetereki. Wanachama wa chama hicho huko wana msimamo thabiti kiasi kwamba ni vigumu kupata wafuasi watiifu muda wote kwa kiongozi bila kujali kiongozi huyo anafanya nini. (Privilege anayopata Odinga huko kwao na Seif huko Pemba)

Katika hali ya kawaida, kama ushauri wa RCC wa kuiweka Mwandiga Kigoma mjini utapitishwa, ingekuwa rahisi sana kwa Zitto kushinda ubunge huko kuliko jimbo lolote Tanzania. Lakini baada ya sarakasi za mara kuisaidia NCCR Kigoma kusini, mara tulimtenda Wangwe, utafiti wake inabidi uwe makini kweli. Nawafahamu sana hawa ndugu zangu wa Kigoma mjini, si aina ya watu wa kuburuza upendavyo, no matter how famous you are!

Namtakia heri kwenye safari yake kisiasa.
 
1.zitto ukigombea Dar ujue ndo umekufa kifo kitakatifu kisiasa.CCM hawataruhusu Kinondoni iende upinzani.Watafanya kila wawezalo,iwe kwa njia halali au haramu.
2.umechemka kutangaza unafanya survey{polling}.Siasa haiko hivyo,Usifikiri wale ambao hawatangazi kama wanafanya polling,usifikiri hawafanyi. Unahitaji kumwajiri "David Axelord" mzuri.Ulie nae hayuko fiti.
 
Mwakyembe team nayo inafanya utafiti kama huohuo wa Zitto,Mambo yakiwa magumu Kyela mpaka Mwezi wa nne anaweza kujitupa Kawe...subiri
 
Bana siasa zetu si hasa, watu waanangalia mkate wao wakila siku, Zitto na wenzake hawana vision kwanini aligombea Ubunge kuwawakilisha wanakigoma wale,anachopaswa kutueleza, mission yake ilikamilika, sasa anataka kwenda jimbo lingine kupeleka maendeleo.....

Mtu anaibuka anataka kuja mjini kugombea.....kwani lazima uwe mwanasiasa....?

Zitto alikuwa na nia ya kugombea ubunge katika mojawapo ya majimbo ya mkoa wa Dar es salaam, alitoa sababu eti anataka kuwa mbunge wa kitaifa. Anaamini kwamba akiwa mbunge jijini Dsm atakuwa na nafasi nzuri zaidi ya kuzungumzia masuala ya kitaifa kuliko kuwa mbunge wa Kalinzi ambako muda mwingi anatakiwa kuzungumzia masuala ya jimbo lake zaidi kulio masuala ya kitaifa.
Nadhani umaarufu alioupata baada ya kutimuliwa bungeni kwa kumkomalia Karamagi na issue ya buzwagi ilimfanya apate wazo kwamba anakubalika nchi nzima kwahiyo anaamini kwamba anaweza kugombea jimbo lolote na kuibuka mshindi, kitu ambacho ni chema ingawa kwa tabia za wakazi wa Dar es salaam, asijekushangaa jinsi watakavyomshangaza!!Watu wa dsm hawaaminiki sana, tumeshuhudia jinsi walivyomimina kura katika uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka jana kwa nambari wani!!
Afadhali agombee kigoma mjini angalau kuna uhakika walau asilimia 70 ya kushinda, ukizingatia wapiga kura wake wa mwandiga wamehamishiwa huko.
Lakini kwa kuwa ameunda synovate yake ngoja tusuiri majibu na uamuzi wake hapo tarehe 28 march. Ila awe mwangalifu sana na huo utafiti wa synovate yake. Suala la msigi aangalie mtego wake wa nyumbu usije ukamnasa simba, atabaki kusimulia tu.......!!!!
 
Back
Top Bottom