Uchaguzi 2010: Zitto, Mbatia wajitosa Ubunge! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uchaguzi 2010: Zitto, Mbatia wajitosa Ubunge!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Ngongo, Mar 1, 2010.

 1. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #1
  Mar 1, 2010
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,324
  Likes Received: 3,910
  Trophy Points: 280
  MBUNGE wa Jimbo la Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe anatarajia kugombea ubunge katika Jimbo la Kinondoni huku Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia akitarajiwa kugombea Jimbo la Kawe, yote ya jijini Dar es Salaam.

  Wakizungumza na gazeti hili jana kwa nyakati tofauti jijini Dar es Salaam viongozi hao walisema wataweka hadharani nia zao za kugombea nafasi hizo kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu baada ya wiki mbili.

  Zitto aliliambia gazeti hili kuwa mbali na jimbo hilo pia wananchi wa majimbo ya Geita, Kahama, Kigoma Mjini na Kigoma Kaskazini wote wanamuhitaji ili awawakilishe.

  "Hadi sasa nimekwishapokea maombi mengi kutoka kwa wananchi wa Jimbo la Kinondoni, Kahama, Geita, Kigoma Mjini na Kigoma Kaskazini ili niwawakilishe bungeni," alisema Zitto.

  Hata hivyo, Zitto ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chadema alisema hadi sasa bado hajafanya uamuzi rasmi wa jimbo gani kati ya hayo atakwenda kugombea.

  Habari za Zitto kugombea Kinondoni ambako Iddi Azan wa CCM ndiye mbunge huenda zikatoa mshtuko kwa mbunge mwenzake wa Chadema, Suzan Lyimo ambaye pia inadaiwa analiwania jimbo hilo.

  Zitto ambaye mwishoni mwa mwaka uliopita alitangaza kuachana na masuala ya siasa ili afanye kazi zake za kitaaluma alisema ameamua kuvunja msimamo wake huo kutokana na maombi ya wananchi kumtaka asiondoke katika medani ya siasa.

  "Napenda kuchukua nafasi hii kutangaza kuwa nitagombea katika moja kati ya hayo majimbo ambayo wananchi wameniomba, lakini hadi sasa bado sijafanya uamuzi rasmi. Pia nimeuvunja msimamo wangu wa kujiondoa katika siasa kama nilivyotangaza awali, hii ni kutokana na maombi ya wananchi kutaka nibakie katika medani ya siasa," alisema Zitto.

  Zitto alifafanua kwamba uamuzi wa kugombea moja kati ya majimbo hayo utategemeana na utafiti na uchunguzi ambao amekwisha uanza kuufanya kupitia watu wake maalumu pamoja na ushauri kutoka kwa viongozi wa chama chake, ndugu, jamaa na marafiki zake.

  "Pamoja na kuhitajika katika majimbo hayo, siwezi kukurupuka na kutangaza tu kuwa nitagombea jimbo hili. Kwanza nimekwishaanza kufanya utafiti na uchunguzi wa kina katika hayo majimbo pia uamuzi wangu utategemeana na ushauri kutoka kwa viongozi wangu wa Chadema, ndugu, marafiki na jamaa zangu," alisema Zitto.

  Zitto ambaye amerejea hivi karibuni kutoka nchini Ujerumani alikokuwa akisoma alisema wananchi wa Jimbo la Kinondoni wamemtaka kugombea jimboni humo ili aweze kupata muda mwingi wa kuwasaidia vijana nchini katika masuala mbalimbali ya kimaendeleo ikiwemo katika siasa.

  "Ukweli ni kuwa kugombea katika moja ya majimbo yaliyopo Dar es Salaam ni tofauti na majimbo mengine ya mikoani kutokana na kwamba ukiwa mikoani unahitaji muda mwingi kujipigia kampeni tofauti na Dar es Salaam ambapo anaweza kuwasaidia hata wanasiasa wengine ndani ya Dar es Salaam na mikoani pia," alisema.

  Kuhusu jimbo la Geita na Kahama, Zitto alisema wananchi wa majimbo hayo wamemuhitaji kutokana na uwelewa wake wa mambo mengi yanayohusu sekta ya madini.

  Katika Jimbo la Kigoma Mjini na la Kaskazini, Zitto alisema ni vigumu kuwaacha wananchi wa huko kutokana na kwamba ndiko alikozaliwa na kwamba wanamuumiza kichwa.

  "Jimbo la Kigoma Mjini na lile la Kaskazini, yananiumiza kichwa kutokana na kwamba yote yapo nyumbani nilipozaliwa, lakini natumai uamuzi wangu nitakaoutoa utazingatia mambo muhimu na wananchi watahuheshimu na kukubaliana nami."

  Tayari uongozi wa mkoa wa Kigoma, umemega eneo la Mwandiga la Kigoma Kaskazini ambalo Zitto anakubalika na kulipeleka Kigoma Mjini. Eneo hilo lililomegwa linadaiwa kuwa ngome kuu ya Zitto na kwamba hatua hiyo inaweza kuchukuliwa kama sababu ya kuhamia Dar es Salaam.

  Naye Mbatia alisema uamuzi wa kugombea katika Jimbo la Kawe unatokana na msingi wa kikatiba na haki ya kila Mtanzania ya kuchagua na kuchaguliwa katika chaguzi zozote.

  "Uamuzi wangu umezingatia msingi wa kikatiba na haki ya kila mtu kuchagua na kuchaguliwa katika chaguzi zozote nchini, pamoja na utashi wa kisiasa nilionao," alisema Mbatia na kuongeza;"

  "Nimechukua uamuzi huu mgumu kutokana na hali halisi ya mazingira ambayo yanahitaji kuwa na mgombea ambaye ataweza kuleta upinzani mkubwa dhidi ya CCM ili iweze kushindwa."

  Kwa sasa Jimbo la Kawe linashikiliwa na mbunge wa CCM, Rita Mlaki. Hata hivyo, mbunge wa Viti Maalumu Chadema, Halima Mdee alikwisha tangaza kwamba katika uchaguzi wa mwaka huu anawania jimbo hilo.

  Mbatia alisema kutokana na mazingira ya Bunge yalivyo yanahitaji wabunge wenye uwezo wa kutoa hoja pamoja na kulishinikiza Bunge liweze kuisimamia na kuiwajibisha serikali vizuri katika masuala nyeti na tete.

  "Bunge jipya lijalo linahitaji kuwa na wabunge wenye nguvu na uwezo wa kutoa hoja pamoja na kulishinikiza Bunge liweze kuiwajibisha na kuisimamia ipasavyo serikali katika masuala nyeti na tete ambayo kwa muda mwingi yanaitafuna na kuimaliza nchi," alisema Mbatia Hata hivyo, Mwenyekiti huyo alisema ataweka nia hiyo hadharani baada ya wiki mbili kuanzia sasa.

  "Wananchi wasiwe na wasi kila kitu kitakuwa bayana baada ya wiki mbili kuanzia sasa ya ama mimi nitagombea au la,"alisema Mbatia ambaye amewahi kuwa mbunge wa Vunjo mwaka 1995-2000.

  Mbatia kama mwenyekiti wa NCCR Mageuzi anaungana na Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa TLP, Augustine Mrema kugombea nafasi ya ubunge.

  Mbowe amekwisha tangaza nia ya kugombea katika Jimbo la Hai wakati Mrema anagombea Jimbo la Vunjo.

  Source: Mwananchi

  Kauli ya Zitto:

  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

  Katika Gazeti la Mwananchi na The Citizen ya leo Jumatatu, Tarehe 1/3/2010 kuna habari ya kwamba ninatafakari kugombea ubunge katika Jimbo la Kinondoni, Mkoa wa Dar es Salaam. Nimeona ni vema nitoe taarifa rasmi juu ya jambo hili.

  Nimeunda kamati ya uchunguzi (Exploratory Committee) ya watu watatu kwa ajili ya kufanya utafiti wa kina juu ya jimbo gani nigombee Ubunge katika uchaguzi Mkuu wa Mwezi Oktoba mwaka 2010. Majimbo ambayo nimeomba wayaangalie ni pamoja na
  Kigoma Kaskazini (ukiondoa kata ya Mwandiga ambayo imependekezwa kukatwa na kupelekwa Jimbo la Kigoma Mjini na hivyo kuondoa zaidi ya wapiga kura 15, 000 kutoka jimbo la Kigoma Kaskazini la sasa), Kigoma Mjini, Kahama, Kinondoni na Geita.

  Nimeelekeza kufanyike utafiti (survey) wa kina ili nitakapofikia kufanya maamuzi nifanye maamuzi kutokana na taarifa za kutosha. Tutatumia wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa ajili ya utafiti huo katika majimbo hayo na pia kwa ajili wa uchambuzi wa hali ya kisiasa na kutoa mapendekezo.

  Ninatarajia kutangaza rasmi Jimbo nitakalogombea Ubunge mnamo siku ya Jumapili tarehe
  28/3/2010.

  Naomba ifahamike kuwa bado sijafanya uamuzi rasmi na kwamba uamuzi wangu utazingatia taarifa ya uchunguzi, ushauri wa viongozi wa chama changu (CHADEMA) na matarajio yangu ya kisiasa ya baadae. Ni muhimu kusisitiza kuwa nikiwa Mtanzania nina haki ya kugombea Ubunge mahala popote nchini.

  Uamuzi wowote nitakaoutoa utazingatia kwa kiasi kikubwa sana umuhimu wa kujenga mfumo imara wa demokrasia ya vyama vingi na hasa kuwa na Bunge imara lenye wabunge wengi wa kambi ya upinzani.  (imesainiwa)

  ZZK.

  1/3/2010
   
 2. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #2
  Mar 1, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,484
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Ha ha ha...lolz..I'm speechless na hizi sarakasi wajameni.
   
 3. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #3
  Mar 1, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,891
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  .
  angalau wameelewa uwezo na nguvu yao, hili ni jambo jema. nawapongeza.
   
 4. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #4
  Mar 1, 2010
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,323
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Professor Lipumba vipi? Mwiba wapi?
   
 5. kilemi

  kilemi JF-Expert Member

  #5
  Mar 1, 2010
  Joined: Mar 13, 2009
  Messages: 524
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Tatizo ni hii mijambazi ya kura!! Wasije mfanyizia kama walivyofanya kwa Mnyika mwaka jana!!
   
 6. r

  rumenyela Member

  #6
  Mar 1, 2010
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hata mimi najiandaa kugombea Ubunge jimbo la kigoma Mjini kupitia Chadema.

  Naombeni mnipe changamoto mbalimbali za kuwa addressed ktk jimbo hili.
   
 7. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #7
  Mar 1, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Mmh ngoja niendelee kusubiri na kujionea mwenyewe.
   
 8. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #8
  Mar 1, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,292
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  KAAZ kweli kweli!poleni sana WAHA:D:D
   
 9. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #9
  Mar 1, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,684
  Likes Received: 172
  Trophy Points: 160
  Lipumba nadhani anakwenda kufanya usanii wa miaka yote! Hatuna haja ya kuuliza maana tunajua mwisho wa siku yeye hatakosa kwenye seleka za kugombea urahisi. Nadhani safari hii naye atapewa uwaziri wa heshima kutokana na MOU ya seif na karume
   
 10. Brooklyn

  Brooklyn JF-Expert Member

  #10
  Mar 1, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,457
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 145
  Hii inadhihirisha nguvu na kukubalika kwa Mh. JMK!! Sijui Lipumba ataenda kugombea wapi?

  Naamini Rais Kikwete ataweka historia ya kuwa Rais wa kwanza Tanzania kupita bila kupingwa katika mfumo wa vyama vingi kwenye uchaguzi mkuu ujao!!

  Kama namuona 'mkwere' anavyojipongeza kwa mvinyo!!

  Kweli CCM CaterPillar....na vyama vya upinzani Vibajaji!!
   
 11. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #11
  Mar 1, 2010
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Prof Lipumba atagombea Jimbo la Ilala.
   
 12. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #12
  Mar 1, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,891
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  Zipo dalili za JK kushinda, lakini bado hajashinda, mapambano yanaendelea.
  kwa Mbowe kugombea ubunge ni sawa, maana aliishawahi kugombea urais akashindwa, sasa ni vyema kupisha wengine ktk nafasi hiyo, ni changamoto kubwa, hivyo ni vyema kujitathmini.
  JK na urais bado naona sijui kama naota kuwa kuna mtu atajitokeza na atamsumbua JK...NATUSUBIRI TUONE.
   
 13. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #13
  Mar 1, 2010
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,902
  Likes Received: 1,133
  Trophy Points: 280
  Mwisho wa Zitto kuwa mbunge naona unakaribia. Namshauri tu asithubutu kuja kugombea jimbo lolote Dar es Salaam, atabwaga chini na bungeni hana lake. Politics is a dirty game!!!! Wanamdanganya!!! Mbunge wa sasa ataendelea kutetea kiti chake!!!!
   
 14. Shishye

  Shishye JF-Expert Member

  #14
  Mar 1, 2010
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 269
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Historia tu? CCM katapila tu?

  Subiri kwanza tuone hao wapinzani kama wataupata huo ubunge. Itapendeza kuona hiyo historia ya ukatapila wa CCM ikiwa na wabunge wachache kuliko upinzani bungeni. Hapo ndio JK atapojipongeza kwa mvinyo sawasawa.
   
 15. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #15
  Mar 1, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,235
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0
  Zitto Kabwe, Mb.
  Kigoma Kaskazini.

  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

  Katika Gazeti la Mwananchi na The Citizen ya leo Jumatatu, Tarehe 1/3/2010 kuna habari ya kwamba ninatafakari kugombea ubunge katika Jimbo la Kinondoni, Mkoa wa Dar es Salaam. Nimeona ni vema nitoe taarifa rasmi juu ya jambo hili.

  Nimeunda kamati ya uchunguzi (Exploratory Committee) ya watu watatu kwa ajili ya kufanya utafiti wa kina juu ya jimbo gani nigombee Ubunge katika uchaguzi Mkuu wa Mwezi Oktoba mwaka 2010. Majimbo ambayo nimeomba wayaangalie ni pamoja na Kigoma Kaskazini (ukiondoa kata ya Mwandiga ambayo imependekezwa kukatwa na kupelekwa Jimbo la Kigoma Mjini na hivyo kuondoa zaidi ya wapiga kura 15, 000 kutoka jimbo la Kigoma Kaskazini la sasa), Kigoma Mjini, Kahama, Kinondoni na Geita.

  Nimeelekeza kufanyike utafiti (survey) wa kina ili nitakapofikia kufanya maamuzi nifanye maamuzi kutokana na taarifa za kutosha. Tutatumia wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa ajili ya utafiti huo katika majimbo hayo na pia kwa ajili wa uchambuzi wa hali ya kisiasa na kutoa mapendekezo.

  Ninatarajia kutangaza rasmi Jimbo nitakalogombea Ubunge mnamo siku ya Jumapili tarehe 28/3/2010.
  Naomba ifahamike kuwa bado sijafanya uamuzi rasmi na kwamba uamuzi wangu utazingatia taarifa ya uchunguzi, ushauri wa viongozi wa chama changu (CHADEMA) na matarajio yangu ya kisiasa ya baadae. Ni muhimu kusisitiza kuwa nikiwa Mtanzania nina haki ya kugombea Ubunge mahala popote nchini.

  Uamuzi wowote nitakaoutoa utazingatia kwa kiasi kikubwa sana umuhimu wa kujenga mfumo imara wa demokrasia ya vyama vingi na hasa kuwa na Bunge imara lenye wabunge wengi wa kambi ya upinzani.

  (imetiwa sahihi)
  ZZK.
  1/3/2010
   
 16. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #16

 17. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #17
  Mar 1, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Hongera zake.Mimi nashauri agombee Kinondoni.Sababu nitazisema baadaye.
   
 18. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #18
  Mar 1, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Dar haina mwenyewe kwa hiyo yupo free kugombea sehemu kubwa wakazi wa Dar ni wahamiaji ila aangalie asije akawa mbunge wa Dar anashinda kigoma!kingine akiwa Dar itakuwa ni rahisi kwake kuimarisha CHADEMA akiwa kama kiongozi wa juu ila akishindwa imekula kwake!
   
 19. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #19
  Mar 1, 2010
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Tunakua kidemokrasia kama Taifa kwa sasa. Kutangaza ufanyikaji wa utafiti wa nigombee jimbo gani kati ya hayoo yalioonyesha nia ya kumhitaji ni MTAJI WA KISIASA KWA MH ZITO.

  Zito siku zote amekuwa akithubutu jambo ambalo ni SIFA PEKEE KWA KIONGOZI KUANZIA NGAZI YA FAMILIA HADI KIJAMIII..

  Namtakia Mh Zito utafiti makini na maamuzi bora kwa mustakabali wa Demokrasia ya Taifa letu.
   
 20. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #20
  Mar 1, 2010
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,387
  Likes Received: 5,752
  Trophy Points: 280
  Hayaaa tutaona fitna za CCM kutokubali Dar mpinzani apate jimbo..kumbuka Mrema na Mtemvu??zitatembea fitna hadi asubuhii...
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.

Loading...