KERO Uchafuzi wa mazingira kwa kuchimba moramu na kulipua mawe kutumia baruti eneo la Kijiji cha Nyangomango kitongoji Nyaruhama kata Usagara

KERO Uchafuzi wa mazingira kwa kuchimba moramu na kulipua mawe kutumia baruti eneo la Kijiji cha Nyangomango kitongoji Nyaruhama kata Usagara

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Eneo hili Kuna uharibifu mkubwa wa mazingira kwa uchimbaji molamu na kulipua mawe kwa kutumia baruti ambazo zinatoa mlipuko kama bomu.Wakazi wa maeneo haya mwaka jana 2025 walilalamika kwenye ofisibza NEMC mkoa wa Mwanza na wakazuia mhusika kuendelea kuchimba badala yake afukie hili shimo.

Katika Hali ya kushangaza Leo 24.03.2026 badala ya kufukia shimo wanaendelea na uchimbaji wa molamu eneo hili.

Eneo hili limekuwa hatarishi sana kwa watoto na wakazu wamaeneo haya kwani ni eneo la makazi ya watu.

Uongozi wa Kijiji inaonekana umeongwa nakuruhusu uharibifu huu uendelee na kuhatarisha makazi ya watu.

OMBI:
Tunaomba wizara ya ardhi iingilie kati ili eneo hili lifukiwe kuendelea kuchimba kutaleta maafa makubwa

IMG-20260324-WA0078.jpg
IMG-20260324-WA0084.jpg
IMG-20260324-WA0083.jpg
IMG-20260324-WA0082.jpg
IMG-20260324-WA0081.jpg
IMG-20260324-WA0079.jpg
IMG-20260324-WA0080.jpg


 
Hawa jamaa wanachojali ni pesa tu na muhimu kwao ni kwamba hawaishi hayo maeneo. Ila kiukweli hii kitu inaharibu sana na kuhatarisha mazingira. Nakupongeza sana kwa kuiwasirisha
 
Back
Top Bottom