Uchafu na harufu mbaya machinjio ya kuku

Tella Mande

JF-Expert Member
Jun 2, 2018
494
674
Nimekuwa kila nikipita maeneo ya masoko mengi yenye machinio ya kuku hapa Dar haswa Shekilango na Manzese ninarudishwa na harufu kali inayotoka kwenye machinjio hayo.

Cha kushangaza uongozi wa masoko hayo, serikali za mtaa na uongozi wa halmashauri zimekuwa kimya kabisa.

Kukiwa na mvua au manyunyu harufu ni kali ya uozo wa masalia ya kuku na damu.

Au hili tatizo naliona peke yangu? Viongozi wanapelekwa mbali humo hawafiki kabisa.

Hii imekaaje wadau?
 
Soko linatoa harufu kama kuna mizoga au maiti pale.

Cha ajabi kuna watu wanalipa kodi na uongoxi upo tu pale
 
Mkuu nenda pale nyuki tegeta sokoni wanapochinjia kuku Kuna arufu na vumbi la ajabu Cha kushangaza wale jamaa wanaochinja wameshazoea hile hali na unakuta wameagiza chakula wanakula kule ndani Kuna siku niliingia Mle ndani nilipata mafua na homa kali.
 
Shekilango instakiwa wachimbe ma septic tank ya kuzamisha mabaki ya kuku. Otherwise hali ni mbaya.
 
Hiyo harufu hapo ni kali sana,damu zinatakiwa zijengewe chemba au shimo lifunikwe juu kwa zege,hiyo harufu hapo ni konki, halafu hao wanyonga kuku wamejazana kwenye hiyo kona nyuma ya kituo cha mafuta.
 
Mhhh huku hakukaliki, kinapuliza hatari. Haruf km mtu kafa.

Wala kuku mnainjoi eeh ila mjue wengine hapakaliki hasa sisi wa dirisha za police post.

Wasalaam.
 
Dar es salaam Inanuka Uozo karibu kila mahali

Hasa Posta na mitaa ya Ferry
 
Back
Top Bottom