Siasa chafu na mambo ya kijinga sisi wananchi tumenyimwa haki ya kufanya mkutano wa wananchi kisa eti serikali ya mtaa walimwita Mbunge kujibu hoja:
Tuna kero 3 kubwa.
1. Kutapeliwa wananchi na serikali ya mtaa katika zoezi la urasimishaji Ardhi
2. Mradi wa maji umesimama bila sababu. Hatuna majibu
3. Mapato na matumizi ya mtaa hayajulikani miaka 3 sasa.
4. Uchafu umezagaa mtaani na kuhatarisha afya zetu.
5. Usalama ni mdogo sana ujambazi na hata wanawake na watoto kubakwa.
Mkutano unakatazwa kwa Faida ya nani.