UBUNGO, DAR: Uchaguzi wa Umeya waahirishwa

UBUNGO, DAR: Uchaguzi wa Umeya waahirishwa

CCM WANAJUA NAMBA, HAWAJUI HESABU!!!

Na. Mtatiro J.

Nimerejea jana DSM. Usiku huo huo nimekutana na madiwani wa UKAWA ambao leo watakuwa wanapambana kulinda ushindi wa wananchi wa Oktoba 25 kwa kuhakikisha Mameya na Manaibu Meya wa Manispaa za Ubungo na Kinondoni wanatoka UKAWA.

NAMBA ZIKOJE KINONDONI:

Madiwani wa CCM kwenye Manispaa ya Kinondoni wako 17 (ukimjulisha hadi Dk. Tulia Ackson - mbunge wa kuteuliwa na Rais). Madiwani wa UKAWA kwa Manispaa ya Kinondoni wako 20.

MCHEZO UKOJE KINONDONI:

Kwanza, Mkurugenzi wa Kinondoni (DED) amewaandikia barua Madiwani wanne wa UKAWA na kuwajulisha kuwa wao si wapiga kura wa Manispaa ya Kinondoni, madiwani hao ni pamoja na Salma Mwasa (Mbunge wa CUF) ambaye amepatia Ubunge wake Jimbo la Kawe lililoko Manispaa ya Kinondoni na hata michakato yote ya kupata Ubunge wake imefanyikia Kawe na NEC na Mkurugenzi wanazo nyaraka zote zinazothibitisha kuwa Mwassa ni diwani wa Kinondoni.

Wakati huo huo mhe. Suzan Lyimo (Mbunge wa Viti Maalum Chadema wa Manispaa ya Kinondoni naye amehamishwa kwa nguvu kwa barua akipelekwa Manispaa ya Ubungo). Uhuni anaofanyiwa Lyimo ndio anaofanyiwa Salma Mwassa wa CUF.

Pili, Mkurugenzi (DED) wa Kinondoni amekokotoa upya idadi ya madiwani wa UKAWA na kumuondoa mmoja, kinyume kabisa na sheria. Mkurugenzi anajisahaulisha kwamba, mamlaka yenye majukumu ya kukokotoa idadi ya madiwani au wabunge wa kila chama ni Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na tume hiyo hufanya hivyo mara baada ya uchaguzi mkuu. Ukokotozi huu mpya wa DED wa Kinondoni ni aibu kuu isiyotekelezeka kisheria, kimantiki na kikanuni.

Tatu, DED wa Kinondoni ameitisha Mkutano wa Uchaguzi ndani ya saa 24 (kwa dharura) huku akiuita Mkutano Maalum. Nimepitia Kanuni za Uendeshaji wa Manispaa na kujiridhisha kuwa Mkutano wa Uchaguzi wa Meya na Naibu Meya hauingii kwenye "mikutano maalum". Huu pia ni uhuni wa karne, DED alipaswa kutoa notisi walau ya siku 7 ili madiwani wajiandae na uchaguzi huu kwa mujibu wa kanuni. Kinyume chake, anazivunja kanuni za Manispaa kwa makusudi kabisa.

Hayo ni baadhi ya masuala yanayoweza kuitwa UHUNI, ambayo nimeyabaini. Yapo mengine kadhaa siwezi kuyataja.

WITO WANGU;

Mwaka jana (2015) wananchi wa DSM walizungumza, tena walizungumza kwa sauti kuu. Manipaa ya Temeke wakasema madiwani wengi watoke CCM, Ilala wakasema ni UKAWA, Kinondoni wakasema ni UKAWA pia. Hakuna maajabu yoyote yatakayobadilisha hali hiyo, hakuna ushindi wa mezani wala kujuana na REFA.
Serikali ya Magufuli isilazimishe mambo yasiyowezekana. Manispaa ya Kinondoni madiwani wengi ni UKAWA, wako 20. Hakuna namna ya leo kuwafanya wawe 16, hakuna atakayekubali. "PUNDA ATAKUFA LAKINI MZIGO UTABAKI" na lazima ushindi wa UKAWA hapa Dar ulindwe kwa gharama yoyote.

Nawatakia kila la heri madiwani wa Manispaa ya Kinondoni, wakalinde na kutetea SAUTI na Maamuzi ya wananchi. 20 ni kubwa kuliko 17, hata mwanangu Alexa anajua hivyo. Upande wa Manispaa ya Ubungo ushindi wa UKAWA hauhujumiki.

Mpenda haki
23 Okt 2016.
Ahsante sana Mtatiro kwa uchambuzi wako
 
Aisee ni bora hii inch iwe ya chama kimoja....nia aibu sana, sasa kwa kitu kidogo hivi ccm wanafanya ubabe na ukandamizaji inakuwe kwenye swala la urais na ubunge
 
Baada ya kuona lipumba hajafanikiwa kugawanya hawa madiwani ili ukawa washindwe wameingia kwa upande mwengne... Najuta kusomaga JF maana hasira unazokuwa nazo waweza itwa mchochezi
 
Ccm wanapima upepo kilichobaki safari hii ukawa tusifanye ukondoo huku tunapoelekea hata uchaguzi 2020 watajitangazia tena kwa mabavu
 
Hii la umeya linaonesha wazi kabisa hulka za ccm.
Hawa hawa amini katika democrasy ya nchi.
Hawakubali kushindwa
Na wapo tayari kufanya hiana yoyote almradi wao watawale milele.
Hii hofu kutokana na wizi na ufisadi mkubwa wanaofanya.
Tuliona zanzibar wameshindwa lakini wametumia jeshi kufanya mapinduzi.
Ccm inabidi kupambana nao kisawa sawa .
 
Uchaguzi wa Umeya umeshafanyika na ma Mayor ni CCM kwa hiyo hakuna lingine zaidi ya kukubali matokeo
 
Kisheria hakuna ukawa. Uchaguzi ufanyike au usifanyike CCM ishashinda Kinondoni. Huo ndo ukweli, na msema kweli ni mpenzi wa Mungu.
mkuu mungu ganianayeruhusu watu 17 wapewe mamlaka dhidi ya watu 20?
 
MWALLA Tunapoongea kwenye majukwaa tunasema kuwa maendeleo hayana chama!..kumbe ni "uongo".Tuliposema kuwa walioshindwa 2015 wakubali kushindwa na wajipange kwa mwaka 2020! ...kumbe ni "ulaghai" Tuliposema kuwa tutafanya kazi na meya wa ukawa...kumbe ilikuwa ni "unafiki".Tulipo sema kuwa watanzania wote ni wamoja na tuutashirikiana kwa pamoja kuleta maendeleo yetu....kumbe ilikuwa ni "hadaa".Lakini,hata farao aliwazungusha sana wana wa israel kwa style hiyohiyo pale walipoomba ruhusa ya kurudi kanaan.Farao aliwategemea miungu na siyo MUNGU wa kweli.ALISHINDWA!.Wana wa israel WAKASHINDA!.Unaweza kuamini nguvu za dola na ufundi wa kubadili sheria,kanuni na taratibu zilizowekwa kwa kudanganya hadhira na ili watu wakuamini,Lakini mungu hadanganyiki kwa namna unavyofikiria.Unaweza kujidanganya kuwa baada ya kutenda dhambi kwa makusudi nitaungama.Dhambi ya makusudi haina toba.
Fanyeni uchaguzi wa mameya wa kinondoni na ubungo kwa haki na kwa kufuata sheria,kanuni na taratibu ili viongozi hao wapatikane kwa haki na hii itampendeza MUNGU wa kweli tunayemuabudu.
 
Tatuzo ni pale viongozi wakuu wa upinzani wanapo kua ndumilakuwili kwa maslahi yao binafsi. Kwa mfano walimwita El fisadi papa, baadae ndo akawa mpeperusha bendera ya upinzani. Emu nieleze hii imekaaje?
Hiyo inahusianaje na uchaguzi wa meya na idadi ya madiwani?
 
Uchaguzi Mayor wa Ubungo umeahirishwa mpaka itakapotangazwa tena. Sababu za kuahirishwa hazijawekwa wazi tutaendelea kuwaletea taarifa kamili

Mwanahabari Huru.

=======

View attachment 422828

Wajumbe wa CHADEMA na CUF wamesusia uchaguzi na kutokana na kile walichokiita kuwa baadhi ya wajumbe wa CCM kuwa wameongezwa na kisha wajumbe wawili wa UKAWA wamehamishwa na kuwapeleka ubungo ili kujipatia ushindi

Na miongoni kwa wajumbe walioongezwa Waziri wa Elimu.
Hao ndio gambaz...watapambana lakini hawatashinda. Na hili ndilo lilikuwa lengo ka kugawa wilaya ya Kinondoni ili watumie mbinu hiyo kuchakachua matokeo. Hata wafanyeje hawawezi kushinda uchaguzi huo....patachimbika!
 
Uchaguzi wa Mayor Kinondoni uliokua ufanyike ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni umevurugika kutokana na kasoro kadhaa zilizojitokeza kama ifuatavyo:

1. CCM walikua wanazidiwa madiwani na UKAWA, kwahiyo wakaamua kuleta wabunge wanne walioteuliwa na Rais kupiga kura kama madiwani wa Kinondoni kinyume na utaratibu. Wabunge hao ni Dr.Tulia Akson, Prof.Joyce Ndalichako, Balozi Augustine Mahiga, na Prof.Makame Mbarawa.

Madiwani wa UKAWA wamepinga ushiriki wa wabunge hawa kwa sababu Sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 1992, na sheria ya serikali za mitaa ya mwaka 1982 kwa pamoja haziruhusu wabunge zaidi ya watatu walioteuliwa na Rais kupiga kura kwenye Halmashauri moja. Kwahiyo kitendo cha CCM kuleta wabunge wanne, wakati maximum ni watatu ni kinyume cha sheria.

2. Wabunge wawili Prof.Joyce Ndalichako na Balozi Dr.Augustino Mahiga walishaapa kama madiwani wa Halmashauri ya manispaa ya Ilala, sasa iweje wapige kura Kinondoni wakati waliapia Ilala?

3. Mbunge wa Viti Maalumu Kinondoni (CHADEMA) Mhe.Suzan Lyimo ameondolewa kwenye kikao kinyume na utaratibu ili asiweze kupiga kura.

4. Mkutano mkuu wa uchaguzi uliitishwa chini ya saa 24 kinyume na sheria za serikali za mitaa zinazotaka mkutano mkuu kuitishwa angalau masaa 72 kabla. Barua ya mkutano wa leo iliandikwa jana na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo ikieleza kuwa kikao ni leo (less than 24 hours hours).

KILICHOTOKEA:
1. Madiwani wa UKAWA wametoka nje na kuungana na wafuasi na wanachama waliokua nje ya ukumbi huo kuelekea Makao makuu ya CHADEMA (Kinondoni) ambapo Mwenyekiti wa Taifa Mhe.Freeman Mbowe atafanya mkutano na vyombo vya habari.

2. Madiwani wa CCM wamebaki ndani lakini wameshindwa kuendelea na mkutano huo maana akidi haijatimia. Kanuni zinataka angalau 2/3 ya wajumbe kuwepo ili kikao kiwe halali. Na 2/3 ya wajumbe wa leo ni angalau madiwani 24. Lakini madiwani wote wa CCM (including wabunge wanne wateule wa Rais) wapo 18 tu, jambo ambalo limewafanya kushindwa kuendelea na mkutano huo
 
Back
Top Bottom