UBUNGO, DAR: Uchaguzi wa Umeya waahirishwa

UBUNGO, DAR: Uchaguzi wa Umeya waahirishwa

Husomeki[emoji216] [emoji196]

CCM WANAJUA NAMBA, HAWAJUI HESABU!!!

Na. Mtatiro J.

Nimerejea jana DSM. Usiku huo huo nimekutana na madiwani wa UKAWA ambao leo watakuwa wanapambana kulinda ushindi wa wananchi wa Oktoba 25 kwa kuhakikisha Mameya na Manaibu Meya wa Manispaa za Ubungo na Kinondoni wanatoka UKAWA.

NAMBA ZIKOJE KINONDONI:

Madiwani wa CCM kwenye Manispaa ya Kinondoni wako 17 (ukimjulisha hadi Dk. Tulia Ackson - mbunge wa kuteuliwa na Rais). Madiwani wa UKAWA kwa Manispaa ya Kinondoni wako 20.

MCHEZO UKOJE KINONDONI:

Kwanza, Mkurugenzi wa Kinondoni (DED) amewaandikia barua Madiwani wanne wa UKAWA na kuwajulisha kuwa wao si wapiga kura wa Manispaa ya Kinondoni, madiwani hao ni pamoja na Salma Mwasa (Mbunge wa CUF) ambaye amepatia Ubunge wake Jimbo la Kawe lililoko Manispaa ya Kinondoni na hata michakato yote ya kupata Ubunge wake imefanyikia Kawe na NEC na Mkurugenzi wanazo nyaraka zote zinazothibitisha kuwa Mwassa ni diwani wa Kinondoni.

Wakati huo huo mhe. Suzan Lyimo (Mbunge wa Viti Maalum Chadema wa Manispaa ya Kinondoni naye amehamishwa kwa nguvu kwa barua akipelekwa Manispaa ya Ubungo). Uhuni anaofanyiwa Lyimo ndio anaofanyiwa Salma Mwassa wa CUF.

Pili, Mkurugenzi (DED) wa Kinondoni amekokotoa upya idadi ya madiwani wa UKAWA na kumuondoa mmoja, kinyume kabisa na sheria. Mkurugenzi anajisahaulisha kwamba, mamlaka yenye majukumu ya kukokotoa idadi ya madiwani au wabunge wa kila chama ni Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na tume hiyo hufanya hivyo mara baada ya uchaguzi mkuu. Ukokotozi huu mpya wa DED wa Kinondoni ni aibu kuu isiyotekelezeka kisheria, kimantiki na kikanuni.

Tatu, DED wa Kinondoni ameitisha Mkutano wa Uchaguzi ndani ya saa 24 (kwa dharura) huku akiuita Mkutano Maalum. Nimepitia Kanuni za Uendeshaji wa Manispaa na kujiridhisha kuwa Mkutano wa Uchaguzi wa Meya na Naibu Meya hauingii kwenye "mikutano maalum". Huu pia ni uhuni wa karne, DED alipaswa kutoa notisi walau ya siku 7 ili madiwani wajiandae na uchaguzi huu kwa mujibu wa kanuni. Kinyume chake, anazivunja kanuni za Manispaa kwa makusudi kabisa.

Hayo ni baadhi ya masuala yanayoweza kuitwa UHUNI, ambayo nimeyabaini. Yapo mengine kadhaa siwezi kuyataja.

WITO WANGU;

Mwaka jana (2015) wananchi wa DSM walizungumza, tena walizungumza kwa sauti kuu. Manipaa ya Temeke wakasema madiwani wengi watoke CCM, Ilala wakasema ni UKAWA, Kinondoni wakasema ni UKAWA pia. Hakuna maajabu yoyote yatakayobadilisha hali hiyo, hakuna ushindi wa mezani wala kujuana na REFA.
Serikali ya Magufuli isilazimishe mambo yasiyowezekana. Manispaa ya Kinondoni madiwani wengi ni UKAWA, wako 20. Hakuna namna ya leo kuwafanya wawe 16, hakuna atakayekubali. "PUNDA ATAKUFA LAKINI MZIGO UTABAKI" na lazima ushindi wa UKAWA hapa Dar ulindwe kwa gharama yoyote.

Nawatakia kila la heri madiwani wa Manispaa ya Kinondoni, wakalinde na kutetea SAUTI na Maamuzi ya wananchi. 20 ni kubwa kuliko 17, hata mwanangu Alexa anajua hivyo. Upande wa Manispaa ya Ubungo ushindi wa UKAWA hauhujumiki.

Ccm-Mhafidhina
23 Okt 2016.
 
Hao ndio Ccm bana, chama kilichodumisha amani ya Tanzania kwa miaka 55 huku kikiiletea maendeleo makubwa

Nasikia na wateuzi wa Magufuli Arusha wanafanya ipasavyo kazi aliyowatuma wanawaseka ndani madiwani wa upinzani na kuwapangia posho ya 10,000
Sijakusoma..
Wanawasweka na kuwapa posho 10000?
 
Halafu kwenye majukwaaa eti mkaongoze malaika mbinguni

Labda watakuwa miungu yenu ya kishenzi
 
Hali ya usalama Uchaguzi Meya Kinondoni asubuhi hii, walioruhusiwa kuingia ni wapiga kura pekee,na Vyombo vya habari sita pekee ndivyo vimeruhusiwa kuingia ndani ya uzio kuripoti, vizuizi vimewekwa na hakuna asiyehusika kuingia katika eneo la kupigia kura.

Awali ilidaiwa kwamba baadhi ya wajumbe wa kamati kuu ya CHADEMA, wakiongozwa na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na Ndugu Edward Lowassa wangehudhuria uchaguzi huo kujionea mwenendo mzima.

Taarifa za awali kutoka manispaa ya Ubungo ni kwamba uchaguzi wa meya wa Ubungo umeahirishwa na mgombea ubunge wa UKAWA, Boniface Jacob, amekamatwa na polisi.
 
Siasa za Bongo ni Pasua Kichwa!Ingekuwa Ni Upande wa Pili Ndio Una Madiwani Wengi,Hizi Figisu figisu tusingeziona!
 
Ukawa wamegoma kushiriki uchaguzi wa meya wa Kinondoni, wadai baadhi ya wajumbe wa CCM wameongezwa, taarifa kamili kutolewa baadaye leo.

--------------------
CCM WAVURUGA UCHAGUZI WA UMEYA KINONDONI:

Uchaguzi wa Mayor Kinondoni uliokua ufanyike ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni umevurugika kutokana na kasoro kadhaa zilizojitokeza kama ifuatavyo:

1. CCM walikua wanazidiwa madiwani na UKAWA, kwahiyo wakaamua kuleta wabunge wanne walioteuliwa na Rais kupiga kura kama madiwani wa Kinondoni kinyume na utaratibu. Wabunge hao ni Dr.Tulia Akson, Prof.Joyce Ndalichako, Balozi Augustine Mahiga, na Prof.Makame Mbarawa.

Madiwani wa UKAWA wamepinga ushiriki wa wabunge hawa kwa sababu Sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 1992, na sheria ya serikali za mitaa ya mwaka 1982 kwa pamoja haziruhusu wabunge zaidi ya watatu walioteuliwa na Rais kupiga kura kwenye Halmashauri moja. Kwahiyo kitendo cha CCM kuleta wabunge wanne, wakati maximum ni watatu ni kinyume cha sheria.

2. Wabunge wawili Prof.Joyce Ndalichako na Balozi Dr.Augustino Mahiga walishaapa kama madiwani wa Halmashauri ya manispaa ya Ilala, sasa iweje wapige kura Kinondoni wakati waliapia Ilala?

3. Mbunge wa Viti Maalumu Kinondoni (CHADEMA) Mhe.Suzan Lyimo ameondolewa kwenye kikao kinyume na utaratibu ili asiweze kupiga kura.

4. Mkutano mkuu wa uchaguzi uliitishwa chini ya saa 24 kinyume na sheria za serikali za mitaa zinazotaka mkutano mkuu kuitishwa angalau masaa 72 kabla. Barua ya mkutano wa leo iliandikwa jana na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo ikieleza kuwa kikao ni leo (less than 24 hours hours).

KILICHOTOKEA:
1. Madiwani wa UKAWA wametoka nje na kuungana na wafuasi na wanachama waliokua nje ya ukumbi huo kuelekea Makao makuu ya CHADEMA (Kinondoni) ambapo Mwenyekiti wa Taifa Mhe.Freeman Mbowe atafanya mkutano na vyombo vya habari.

2. Madiwani wa CCM wamebaki ndani lakini wameshindwa kuendelea na mkutano huo maana akidi haijatimia. Kanuni zinataka angalau 2/3 ya wajumbe kuwepo ili kikao kiwe halali. Na 2/3 ya wajumbe wa leo ni angalau madiwani 24. Lakini madiwani wote wa CCM (including wabunge wanne wateule wa Rais) wapo 18 tu, jambo ambalo limewafanya kushindwa kuendelea na mkutano huo
 

Attachments

  • IMG-20161023-WA0018.jpg
    IMG-20161023-WA0018.jpg
    66.9 KB · Views: 41
ccm wamelazimisha kupata meya kinondoni nje ya utaratibu. ukawa wameamua kususa na ccm imelazimisha kihairishwa uchaguzi wa ubungo ili wajipange upya. kwa kweli afrika ni shiida...
 
ccm hii ya john ni hatari zaidi kuliko ile ya jakaya. demokrasia ni msamiati mkubwa kwao. poleni sana wapenda demokrasia na ukawa kiujumla...
 
UCHAGUZI MEYA: Ukawa wamegoma kushiriki uchaguzi wa meya wa Kinondoni, wadai baadhi ya wajumbe wa CCM wameongezwa, taarifa kamili kutolewa baadaye leo.
Kamanda ungesubiria habari kamili ndo umwage jamvini..
Unawachanganya Teamlumumba[emoji196] [emoji216]
 
CCM YAVURUGA UCHAGUZI MAYOR KINONDONI,

By Malisa GJ,

Uchaguzi wa Mayor Kinondoni uliokua ufanyike ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni umevurugika kutokana na kasoro kadhaa zilizojitokeza kama ifuatavyo:

1. CCM walikua wanazidiwa madiwani na UKAWA, kwahiyo wakaamua kuleta wabunge wanne walioteuliwa na Rais kupiga kura kama madiwani wa Kinondoni kinyume na utaratibu. Wabunge hao ni Dr.Tulia Akson, Prof.Joyce Ndalichako, Balozi Augustine Mahiga, na Prof.Makame Mbarawa.

Madiwani wa UKAWA wamepinga ushiriki wa wabunge hawa kwa sababu Sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 1992, na sheria ya serikali za mitaa ya mwaka 1982 kwa pamoja haziruhusu wabunge zaidi ya watatu walioteuliwa na Rais kupiga kura kwenye Halmashauri moja. Kwahiyo kitendo cha CCM kuleta wabunge wanne, wakati maximum ni watatu ni kinyume cha sheria.

2. Wabunge wawili Prof.Joyce Ndalichako na Balozi Dr.Augustino Mahiga walishaapa kama madiwani wa Halmashauri ya manispaa ya Ilala, sasa iweje wapige kura Kinondoni wakati waliapia Ilala?

3. Mbunge wa Viti Maalumu Kinondoni (CHADEMA) Mhe.Suzan Lyimo ameondolewa kwenye kikao kinyume na utaratibu ili asiweze kupiga kura.

4. Mkutano mkuu wa uchaguzi uliitishwa chini ya saa 24 kinyume na sheria za serikali za mitaa zinazotaka mkutano mkuu kuitishwa angalau masaa 72 kabla. Barua ya mkutano wa leo iliandikwa jana na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo ikieleza kuwa kikao ni leo (less than 24 hours hours).

KILICHOTOKEA:
1. Madiwani wa UKAWA wametoka nje na kuungana na wafuasi na wanachama waliokua nje ya ukumbi huo kuelekea Makao makuu ya CHADEMA (Kinondoni) ambapo Mwenyekiti wa Taifa Mhe.Freeman Mbowe atafanya mkutano na vyombo vya habari.

2. Madiwani wa CCM wamebaki ndani lakini wameshindwa kuendelea na mkutano huo maana akidi haijatimia. Kanuni zinataka angalau 2/3 ya wajumbe kuwepo ili kikao kiwe halali. Na 2/3 ya wajumbe wa leo ni angalau madiwani 24. Lakini madiwani wote wa CCM (including wabunge wanne wateule wa Rais) wapo 18 tu, jambo ambalo limewafanya kushindwa kuendelea na mkutano huo.

Malisa GJ
 
Back
Top Bottom