UBUNGO, DAR: Uchaguzi wa Umeya waahirishwa

UBUNGO, DAR: Uchaguzi wa Umeya waahirishwa

kwa ccm wanaweza lazimisha kufanya uchaguzi na kusema kwamba hakidi ilitimia. usiombee ukutane na maccm ni hatari.
Wanataka kuleta mambo ya ujecha sasa yaani kisheria haiwezekani labda kijecha ila huu ni ujinga mwingine kwa ccm hawajui Namba hazidanganyi
 
Wamekula pesa za tetemeko la Bukoba hawajatosheka tu,wsmeshindwa kuwapa wanafunzi mkopo hovyo kabisa
 
kwa ccm ushindi ni lazima. bila ccm kuondoka madarakani hakuna demokrasia ya kweli itakayotamalaki hapa nchini. kinondoni wanaletwa watu ambao hawastahili kuwepo kinondoni ili tu ccm itoe meya. kwa nini ccm wasijipange baada ya miaka mitano ijayo?
 
Uchaguzi Mayor wa Ubungo umeahirishwa mpaka itakapotangazwa tena. Sababu za kuahirishwa hazijawekwa wazi tutaendelea kuwaletea taarifa kamili

Mwanahabari Huru.

=======

View attachment 422828

Wajumbe wa CHADEMA na CUF wamesusia uchaguzi na kutokana na kile walichokiita kuwa baadhi ya wajumbe wa CCM kuwa wameongezwa na kisha wajumbe wawili wa UKAWA wamehamishwa na kuwapeleka ubungo ili kujipatia ushindi

Na miongoni kwa wajumbe walioongezwa Waziri wa Elimu.
Waziri wa Elimu si profesa huyu tena TO nasikia?
Keshaweka akili mfukoni mapema yote hii?
 
Benjamin Sitta (CCM) ndiye Meya mpya wa Kinondoni. Amepata kura za ndio 18 wapinzani wamekimbia. Nafasi ya Naibu Meya imechukuliwa na George Manyama wa CCM kwa kura zote 18.
 
Benjamin Sitta (CCM) ndiye Meya mpya wa Kinondoni. Amepata kura za ndio 18 wapinzani wamekimbia. Nafasi ya Naibu Meya imechukuliwa na George Manyama wa CCM kwa kura zote 18.
 
Benjamin Sitta (CCM) ndiye Meya mpya wa Kinondoni. Amepata kura za ndio 18 wapinzani wamekimbia. Nafasi ya Naibu Meya imechukuliwa na George Manyama wa CCM kwa kura zote 18.
Uchaguzi unarudiwa wanatakiwa madiwani 22
 
Magamba wanajisumbua tu kama walivyojisumbua kwenye umeya Wa jiji mwisho wakaachia Namba hazidanganyi hata siku moja ccm mjifunze kuisoma Namba sasa wananchi walishaamua msiwalazimishe
 
CCM WANAJUA NAMBA, HAWAJUI HESABU!!!

Na. Mtatiro J.

Nimerejea jana DSM. Usiku huo huo nimekutana na madiwani wa UKAWA ambao leo watakuwa wanapambana kulinda ushindi wa wananchi wa Oktoba 25 kwa kuhakikisha Mameya na Manaibu Meya wa Manispaa za Ubungo na Kinondoni wanatoka UKAWA.

NAMBA ZIKOJE KINONDONI:

Madiwani wa CCM kwenye Manispaa ya Kinondoni wako 17 (ukimjulisha hadi Dk. Tulia Ackson - mbunge wa kuteuliwa na Rais). Madiwani wa UKAWA kwa Manispaa ya Kinondoni wako 20.

MCHEZO UKOJE KINONDONI:

Kwanza, Mkurugenzi wa Kinondoni (DED) amewaandikia barua Madiwani wanne wa UKAWA na kuwajulisha kuwa wao si wapiga kura wa Manispaa ya Kinondoni, madiwani hao ni pamoja na Salma Mwasa (Mbunge wa CUF) ambaye amepatia Ubunge wake Jimbo la Kawe lililoko Manispaa ya Kinondoni na hata michakato yote ya kupata Ubunge wake imefanyikia Kawe na NEC na Mkurugenzi wanazo nyaraka zote zinazothibitisha kuwa Mwassa ni diwani wa Kinondoni.

Wakati huo huo mhe. Suzan Lyimo (Mbunge wa Viti Maalum Chadema wa Manispaa ya Kinondoni naye amehamishwa kwa nguvu kwa barua akipelekwa Manispaa ya Ubungo). Uhuni anaofanyiwa Lyimo ndio anaofanyiwa Salma Mwassa wa CUF.

Pili, Mkurugenzi (DED) wa Kinondoni amekokotoa upya idadi ya madiwani wa UKAWA na kumuondoa mmoja, kinyume kabisa na sheria. Mkurugenzi anajisahaulisha kwamba, mamlaka yenye majukumu ya kukokotoa idadi ya madiwani au wabunge wa kila chama ni Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na tume hiyo hufanya hivyo mara baada ya uchaguzi mkuu. Ukokotozi huu mpya wa DED wa Kinondoni ni aibu kuu isiyotekelezeka kisheria, kimantiki na kikanuni.

Tatu, DED wa Kinondoni ameitisha Mkutano wa Uchaguzi ndani ya saa 24 (kwa dharura) huku akiuita Mkutano Maalum. Nimepitia Kanuni za Uendeshaji wa Manispaa na kujiridhisha kuwa Mkutano wa Uchaguzi wa Meya na Naibu Meya hauingii kwenye "mikutano maalum". Huu pia ni uhuni wa karne, DED alipaswa kutoa notisi walau ya siku 7 ili madiwani wajiandae na uchaguzi huu kwa mujibu wa kanuni. Kinyume chake, anazivunja kanuni za Manispaa kwa makusudi kabisa.

Hayo ni baadhi ya masuala yanayoweza kuitwa UHUNI, ambayo nimeyabaini. Yapo mengine kadhaa siwezi kuyataja.

WITO WANGU;

Mwaka jana (2015) wananchi wa DSM walizungumza, tena walizungumza kwa sauti kuu. Manipaa ya Temeke wakasema madiwani wengi watoke CCM, Ilala wakasema ni UKAWA, Kinondoni wakasema ni UKAWA pia. Hakuna maajabu yoyote yatakayobadilisha hali hiyo, hakuna ushindi wa mezani wala kujuana na REFA.
Serikali ya Magufuli isilazimishe mambo yasiyowezekana. Manispaa ya Kinondoni madiwani wengi ni UKAWA, wako 20. Hakuna namna ya leo kuwafanya wawe 16, hakuna atakayekubali. "PUNDA ATAKUFA LAKINI MZIGO UTABAKI" na lazima ushindi wa UKAWA hapa Dar ulindwe kwa gharama yoyote.

Nawatakia kila la heri madiwani wa Manispaa ya Kinondoni, wakalinde na kutetea SAUTI na Maamuzi ya wananchi. 20 ni kubwa kuliko 17, hata mwanangu Alexa anajua hivyo. Upande wa Manispaa ya Ubungo ushindi wa UKAWA hauhujumiki.

Mpenda haki
23 Okt 2016.
Eti lofa naye amekuwa mtenda hali!!
 
CCM YAVURUGA UCHAGUZI MAYOR KINONDONI,

Uchaguzi wa Mayor Kinondoni uliokua ufanyike ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni umevurugika kutokana na kasoro kadhaa zilizojitokeza kama ifuatavyo:

1. CCM walikua wanazidiwa madiwani na UKAWA, kwahiyo wakaamua kuleta wabunge wanne walioteuliwa na Rais kupiga kura kama madiwani wa Kinondoni kinyume na utaratibu. Wabunge hao ni Dr.Tulia Akson, Prof.Joyce Ndalichako, Balozi Augustine Mahiga, na Prof.Makame Mbarawa.

Madiwani wa UKAWA wamepinga ushiriki wa wabunge hawa kwa sababu Sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 1992, na sheria ya serikali za mitaa ya mwaka 1982 kwa pamoja haziruhusu wabunge zaidi ya watatu walioteuliwa na Rais kupiga kura kwenye Halmashauri moja. Kwahiyo kitendo cha CCM kuleta wabunge wanne, wakati maximum ni watatu ni kinyume cha sheria.

2. Wabunge wawili Prof.Joyce Ndalichako na Balozi Dr.Augustino Mahiga walishaapa kama madiwani wa Halmashauri ya manispaa ya Ilala, sasa iweje wapige kura Kinondoni wakati waliapia Ilala?

3. Mbunge wa Viti Maalumu Kinondoni (CHADEMA) Mhe.Suzan Lyimo ameondolewa kwenye kikao kinyume na utaratibu ili asiweze kupiga kura.

4. Mkutano mkuu wa uchaguzi uliitishwa chini ya saa 24 kinyume na sheria za serikali za mitaa zinazotaka mkutano mkuu kuitishwa angalau masaa 72 kabla. Barua ya mkutano wa leo iliandikwa jana na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo ikieleza kuwa kikao ni leo (less than 24 hours hours).

KILICHOTOKEA:
1. Madiwani wa UKAWA wametoka nje na kuungana na wafuasi na wanachama waliokua nje ya ukumbi huo kuelekea Makao makuu ya CHADEMA (Kinondoni) ambapo Mwenyekiti wa Taifa Mhe.Freeman Mbowe atafanya mkutano na vyombo vya habari.

2. Madiwani wa CCM wamebaki ndani lakini wameshindwa kuendelea na mkutano huo maana akidi haijatimia. Kanuni zinataka angalau 2/3 ya wajumbe kuwepo ili kikao kiwe halali. Na 2/3 ya wajumbe wa leo ni angalau madiwani 24. Lakini madiwani wote wa CCM (including wabunge wanne wateule wa Rais) wapo 18 tu, jambo ambalo limewafanya kushindwa kuendelea na mkutano huo.

Malisa GJ
 
Back
Top Bottom