Ubungo bus terminal dump ya uchafu, jiji wapi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ubungo bus terminal dump ya uchafu, jiji wapi?

Discussion in 'Jamii Photos' started by Saint Ivuga, Dec 31, 2011.

 1. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #1
  Dec 31, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,252
  Likes Received: 19,382
  Trophy Points: 280
  Mlibisha na mtaendelea kubisha lakini ukweli utabaki pale pale..watz wana IQ ndogo...
  hapa ni ubungo kila siku iendayo kwa Mungu watu an magari yanalipa kodi lakini kusafisha tu kitendo cha dakika hata kumi hawataki ..na wananchi hawana wasi wasi wapo free wanaishi tu.IQ ni ndogo sana ..msisitizo hapo kwenye sana..
  DSCF5790.JPG DSCF5791.JPG DSCF5792.JPG
   
 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  Dec 31, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,252
  Likes Received: 19,382
  Trophy Points: 280
  picha kwa hisani ya godwine
   
 3. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #3
  Dec 31, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG] [​IMG]

  Sipati picha uchafu kufurika eneo ambalo watu usiku na mchana wapo, na bus terminal kama hii ni shauri kuwa na wafanyakazi kama wawili hivi ambao muda wate wanazungukia maeno yote na kuokota uchafu na kwenda kuuweka sehemu ambayo imehifadhiwa kwa shughuli hii. Mpaka hayo tunahitaji misaada ya wahisani?
   
 4. babuwaloliondo

  babuwaloliondo JF-Expert Member

  #4
  Dec 31, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 378
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Ivuga, katika vitu ambavyo sisi watanzania wengi hatupendi kuambiwa ni ukweli kuusu mitazamo yetu hasi ya maisha.
  Tu wabishi sana, imani potofu pasipo kufikiri, uchafu uliokithiri, kutokuwajibika, tabia za kuombaomba kila kukicha.
  Hatutaendelea kamwe, labda tutawaliwe tena.
   
 5. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #5
  Dec 31, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,607
  Likes Received: 4,599
  Trophy Points: 280
  Serikali ya Halmashauri ya jiji kweli hapo nyumbani ipo?Uchafu mijini namna hii Ahhh jamani nchi yetu haina viongozi.
   
 6. Roulette

  Roulette JF-Expert Member

  #6
  Dec 31, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 5,618
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  So, what did the photographer do? Au ndio hivi kakupa uje kutwambia? And what are YOU planing to do?
   
 7. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #7
  Dec 31, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,406
  Trophy Points: 280
  Hii stendi ni chafu mno.

  Haijakaa kimpangilio. Ukiwa unamsindikiza mtu kuna ada unayotakiwa kulipa (shilingi 200 kama sikosei). Lakini cha ajabu kwenye lango la kuingilia hakuna ubao unaosema wasindikizaji wanatakiwa kulipia.

  Kama upo ama wameuweka siku za karibuni au haupo sehemu unapoweza kuonekana kiurahisi. Kwa ujumla kila kitu kimekaa shaghalabaghala tu hapo.

  Halafu pananuka kichizi.
   
 8. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #8
  Dec 31, 2011
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Nikitilia maani uwiano wa idadi ya watu wanaopita hapo kwa nikilinganisha na sehemu nyingine; mbona hapo pana uafadhali!!
  Mara ya mwisho nimecheck kama wiki tatu hivi, vyoo vilikuwa na maji na viko katika kiwango cha kutumika kwa mtu aliyebanwa!!! Kumbuka kuna pahala penye mikusanyiko nimefika, yaani hata kama haja imekubana, unconsciously unajikuta umepata ahueni baada ya kuona mazingira yenye kinyaa chakupindukia pahala pa kujisaidia.

  Wizi wa vitu pia umepungua, maana hawaruhusu tena wapokeaji kuingia ndani ya uzio kiurahisi kama ilivyokuwa mwanzo. Mabasi pia yanaondoka on time kuanza safari zake.

  Uchafu kama unavyoonekana hapo kwenye picha ni matokeo ya hulka za wengi wetu. Ndivyo tulivyo; haswa Dar na 'umjini-umjini' kama sifa'!!! Inaudhi sana na ni kero kubwa.
   
 9. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #9
  Dec 31, 2011
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Ni moja ya sehemu zinazoonyesha wazi wazi kuwa hatuwezi kufanya vitu vyetu kwa namna ambayo kila mmoja akajivunia. Hapo tuna kila aina ya viongozi, lakini tumeendekeza ubinafsi. Ubungo terminal inatakiwa ijiendeshe kisasa zikiwemo miundo mbinu za kisasa. Hapo unaweza kuambiwa huwa wanasubiri gari la manispaa kuwatolea uchafu wakati ni kiasi cha kununua gari lao wenyewe, kuajiri watu wao wenyewe wawe wanawalipa mishahara hadi na serikali kukata kodi.

  Cha msingi tumeacha kukaa chini na kufikiri mazuri, tunawaza short-cut ya jinsi tutatajirika haraka bila kuumiza vichwa ili kupata vitu kiuhalali. Sehemu ya abiria kusubiri usafiri au kupokelea wageni zimegeuzwa za makampuni binafsi which is wrong, Bus terminal kama hiyo ilitakiwa kila mtu akifika anasema kweli hii ni moja ya maeneo yanaelezea vyetu. J. J. Mnyika, tafadhali onyesha kukerwa pia na hiyo hali.
   
 10. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #10
  Dec 31, 2011
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280

  Katika mambo yananikera, ni inshu ya uchafu bongo. Inabidi sheria kali zitungwe na watu waajiriwe ili kuzilinda, na mtu akikamatwa anatupa hovyo sheria inachukua mkondo. Utakuta mtu anakula kitu kwenye bus/daladala baada ya hapo anatupa barabarani tena bila aibu.

  Hapo ubungo ni afadhali lakini bado tuna kazi kubwa ya kuelimishana kuhusu usafi kwa ujumla.
   
 11. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #11
  Dec 31, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,392
  Likes Received: 81,396
  Trophy Points: 280
  Jiji lote la Dar ni dampo ya uchafu. Mie sioni hata sehemu yenye afadhali. 2010 Dar ilikuwa jiji la 7 kwa uchafu duniani na ya tatu kwa uchafu Afrika sidhani kama kuna ahueni yoyote iliyotokea 2011. Wamethubutu, wameweza na sasa wanasonga mbele.
   
 12. Ab-Titchaz

  Ab-Titchaz Content Manager Staff Member

  #12
  Dec 31, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 14,702
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Wala hujakosea mkuu. Mwaka jana niilipokua Dar desemba nilishangaa hata nikawa najuta kuwasili Bongo mchana kweupeee!!

  Mchizi nilikua niko juu ya daladala trying to get the home feeling na amini usiamini kulikua na jamaa kasimama barabarani akikojoa mtaroni laivu!!!...Mwenzio mbona nikamaka kwa mshangao na abiria aliyekua amekaa ubavu wa pili akaniuliza "hivi wewe ni mgeni hapa mjini?" namii nikamwambia ndivyo na ndo nimelandi kutoka Marekani. Jamaa akacheka kisha akanijibu "karibu nyumbani, utazoea tu". Nilishangaa na nikakataa kauli yake eti "nitazoea'....there is no way in hell nitaozea kumwona mtu mzima hoyvoo, dudu nje akimwaga jojo kadamnasi mitaa ya Sinza.

  Kisha kuanzia mitaa ya Mikocheni hadi Kawe ndo hapafai kabisa maana ni arufu mtindo mmoja!!! Maji taka hayazolewi na hata wakifanya kuzoa ni upuzi mtupu. Jamaa wanatoa uchafu ndani ya mtaro na kuuweka right at the top. In simple common sense, when it rains wont all this trash go right back into the drains jamani!!!? Nilipohoji nikaambiwa jama wanafanya hivyo maksudi ndo waweza kuhifadhi kibarua for the next day...Gaaadem!...Yaani Bongo kivyakevyake aisee. Kisha maeneo yenyewe nd'o barabara inayopitiwa na matasha na nikahooji tena kwani hawaoni hali ilivyo hususan kukinyesha. Nikaambiwa ukilinganisha na swala la kwamba jamaa wanaendesha mashangingi fuli-kipupwe, kwani wanaipata hio harufu?...najua ushapata jibu hapo!

  Kisha ukiingia mjini wakati mambo ya umeme yanaleta kasheshe utajuta!...Kelele ya majenereta ni kama kuzimu! Yaani waliohujumu wananchi wa Tanzania kwa skendo za ishu za umeme hawakuwatenedea wananchi haki...but then again, who cares.

  Kisha hapo Ubungo nitawaachia wenyewe wajadli. Kama Nyani alivyosema hapo juu watu wanaosindikiza abiria wanatozwa hela lakini
  hujui hela inaenda wapi au ni ya nini. There is no official communication for that matter. Kisha kila mtu ni mwizi/tapeli hususan kipindi cha krismasi na shamrashamra za New Year. Utauziwa tikiti na jamaa kisha mkishamalizana na umekaa kwenye nafasi yako, anatokea konda mwengine anakudai hela zaidi. Ukijaribu kumtafuta aliyekukapa tikiti humuoni. Mwenzenu niligoma kushuka basi la Tanga kwa upuzi huo. Jamaa ilibidi nimmwagie kimombo na kumsuta mbaya sana. Tatizo langu lilkua usumbufu tu wa hawa matapeli. At the end of the whole saga tukawa washkaji mpaka kubadili namba za simu na niikapata kupiga tripu zengine mbili na jamaa hadi Mombasa na kurudi Dar.

  Bongo tambarare wakuu...akili mukichwa!
   
 13. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #13
  Dec 31, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,392
  Likes Received: 81,396
  Trophy Points: 280

  ....Ahsante sana Mkuu kwa mchango wako mzuri. Miezi michache iliyopita nilipata bahati ya kutembelea mitaa mbali ya jiji la Dar ambayo miaka ya nyuma ilikuwa bomba sana. Enzi hizo kulikuwa na garden zimekatwa majani vizuri sana na maua ya kila aina na taa za barabarani za kumwaga. Kwa kweli ilikuwa inapendeza sana. Miezi michache iliyopita nikapita katika mitaa hiyo na kukuta zile garden sasa hivi zimekuwa ni vichaka sijui majana hayajakatwa kwa miaka mingapi, maua hakuna hata moja. Barabara ambazo zilikuwa zinapendeza mno kwa lami ya hali ya juu sasa hivi kumejaa makorongo na taa zote hazifanyi kazi (kulikuwa hakuna mgao wakati huo). Nikabaki nasikitika tu jinsi hali ya jiji inavyozidi kudidimia.

  Siku moja nilikuwa mitaa ya Ilala naona gari linapita huku likirusha uchafu ambao ulikuwa unapeoerushwa na upepo. Nikauliza hili gari mbona linafanya uchafuzi kiasi hiki? Nikaambiwa hilo ni gari la kubeba taka!!!! Nikabaki kushangaa, gari la kubeba taka liko wazi!!! Uchafu wote waliobeba unasambaa hovyo hovyo na hivyo kuchangia katika uchafuzi wa jiji. Hivi wamekosa kutafuta magari yaliyozibwa ili uchafu ukishawekwa ndani ya gari la taka usisambae tena mitaani!? Nikaambiwa ndio bongo hii!!! Duh! Nikachoka kabisa.

  Nikasema hapa Dar kuna utitiri wa wanaoitwa Viongozi wa jiji kuanzia Mkuu wa Mkoa, Meya wa Jiji, Mkuu wa wilaya ya Ilala, Temeke na Kinondoni hivi kuna haja ya kuendelea kuwalipa hawa mishahara na marupurupu manono wakati wameshondwa kusimamia kazi ya kuboresha jiji!? Sheria za kuhakikisha jiji linakuwa safi zipo nyingi sana lakini hakuna hata anayezitilia maanani na sasa Jiji limekuwa Jiji la mafuriko hali ndio itakuwa mbaya zaidi na si ajabu kama itafanyika tena tathmini ya majiji machafu duniani/afrika basi Dar itachukuwa nafasi ya kwanza katika category zote mbili.....Kweli Dar tambarare!!!!

   
 14. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #14
  Jan 1, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,252
  Likes Received: 19,382
  Trophy Points: 280
  sijui nani katuloga
   
 15. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #15
  Jan 1, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,252
  Likes Received: 19,382
  Trophy Points: 280
  wapo wanakusanya kodi..ukiwatapa ubaya acha kulipa kodi utakiona cha mtema kuni
   
 16. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #16
  Jan 1, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,252
  Likes Received: 19,382
  Trophy Points: 280
  oo i even dont know what to say...our country is just amazing ...may be we love kipindupindu...and i dont understand our journalists. these guys are using this bus terminal everyday but you cant hear em saying anything.
   
 17. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #17
  Jan 1, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,252
  Likes Received: 19,382
  Trophy Points: 280
  sasa kwa nini hawataki kuuondoa?kodi wanapeleka wapi jamani.
   
 18. Roulette

  Roulette JF-Expert Member

  #18
  Jan 1, 2012
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 5,618
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Then YOU do something. Sijasema ukuzoe ule uchafu but try to use your right as a citizen to exercise some agency...
   
 19. Dunda kwetu

  Dunda kwetu JF-Expert Member

  #19
  Jan 1, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 265
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  unajua zile pesa za ushuru uwa zina walevya wanaokusanya na wanaotumia,cheki pale lango kuu la kuingilia walivyo wakali na wanavyo toa mimacho kwa wasiokuwa na ticket
   
 20. AMINATA 9

  AMINATA 9 JF-Expert Member

  #20
  Jan 1, 2012
  Joined: Aug 6, 2011
  Messages: 2,132
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  umenikumbusha huo utaratibu upo hadi leo kwani? mana loh! ulikua unaniboa kinoma yani
   
Loading...