Michael Amon
JF-Expert Member
- Dec 22, 2008
- 8,775
- 3,610
kama ni uchafu basi jiji la Dar limekithiri. Jamani watanzania tubadilike, hadi tuchapwe viboko jamani?
kama ni uchafu basi jiji la Dar limekithiri. Jamani watanzania tubadilike, hadi tuchapwe viboko jamani?
Nashangaa kuona baadhi wakisema hapo Ubungo stendi ni pasafi.
Nikitilia maani uwiano wa idadi ya watu wanaopita hapo kwa nikilinganisha na sehemu nyingine; mbona hapo pana uafadhali!!
Mara ya mwisho nimecheck kama wiki tatu hivi, vyoo vilikuwa na maji na viko katika kiwango cha kutumika kwa mtu aliyebanwa!!! Kumbuka kuna pahala penye mikusanyiko nimefika, yaani hata kama haja imekubana, unconsciously unajikuta umepata ahueni baada ya kuona mazingira yenye kinyaa chakupindukia pahala pa kujisaidia.
Wizi wa vitu pia umepungua, maana hawaruhusu tena wapokeaji kuingia ndani ya uzio kiurahisi kama ilivyokuwa mwanzo. Mabasi pia yanaondoka on time kuanza safari zake.
Uchafu kama unavyoonekana hapo kwenye picha ni matokeo ya hulka za wengi wetu. Ndivyo tulivyo; haswa Dar na 'umjini-umjini' kama sifa'!!! Inaudhi sana na ni kero kubwa.
Kaka naona unatetea kwa Nguvu zoote; pamoja na hulka za ajabu za Watanzania ambazo si suala la kubishia lakni si unaona pipa limejaa!!!.....unategemea watu wafanyeje?..na huo uchafu ulioko chini ni zaidi ya pipa mbili, hali inayoashiria kuwa hakuna umakini katika kufuatilia usafi wa mazingira stendi hapo, watu wakishafagia asubuhi wanaona kazi imeisha!