Ubungo 2010: Nani zaidi, Nape au Mnyika?

MkuyuMkubwa

Member
Sep 27, 2009
50
0
Kuna taarifa kwamba mmoja wa wapiganaji wa vita dhidi ya ufisadi ndani ya CCM, kijana Nape amezidi kuweka mizizi jimbo la ubungo kuhakikisha anashinda kupitia ccm, huku wakati huohuo, kijana mwenzake John Mnyika akizidi kujipanga kujaribu tena bahati yake.....Binafsi ningetamani kuwaona wote, Mnyiks ns Nape wakiwa bungeni kila mmoja kupitia chama chake...lakini huu ni uchaguzi, ambao ni lazima mmoja apoteze ili mmoja ashinde.....changamoto kubwa ni kwamba wagombea wote wawili wana sifa zinazo fanana kuvutia wapiga kura. je, nani angefaa zaidi kama jf tungeamua?
1.Wote ni vijana
2.Wote wana majina makubwa...ingawa yanazidiana, nani kubwa zaidi?
3.Wote wasomi, ingawa wanazidiana, anani zaidi?
4.Wote wanajitambulisha kama wapinga ufisadi, nani zaidi?

NANI NI NANI HAPA?...TUMPOTEZE NANI? TUMPATE NANI?
 
Binafsi nadhani wote wanafaa kuwakilisha jimbo la Ubungo

Nape amejipambanua kwamba yeye ni mpiganaji hodari ndani ya chama kilichojaa mafisadi.Hili si jambo dogo hasa tukizingatia aliokuwa akipambana nao.Mnyika yuko kwenye chama kizuri lakini bado sijaona mchango wowote wa maana kutoka kwa Myika.

CHADEMA kimepitia hatua nyingi sijaona mchango wa Myika zaidi ya kumwona akivalia nguo za mgambo.Mara kadhaa nimesika Mnyika anajiambatanisha sana na Mwenyekiti wa chama katika mipango mizuri na hata mipango mibaya dhidi ya wanachama/viongozi wa CHADEMA.
 
Nape being representing Chama cha Mafisadi I do not expect much from him. I will for sure go for Mnyika.

Tiba
 
Weka CV ya kila mmoja wao hapa tuone licha ya hayo majina makubwa. Kusema tu kua wote wamesoma haitoshi,wamesoma nini,wapi,ktk level gani? Leadership and potentials zao?
 
Kuna taarifa kwamba mmoja wa wapiganaji wa vita dhidi ya ufisadi ndani ya CCM, kijana Nape amezidi kuweka mizizi jimbo la ubungo kuhakikisha anashinda kupitia ccm, huku wakati huohuo, kijana mwenzake John Mnyika akizidi kujipanga kujaribu tena bahati yake.....Binafsi ningetamani kuwaona wote, Mnyiks ns Nape wakiwa bungeni kila mmoja kupitia chama chake...lakini huu ni uchaguzi, ambao ni lazima mmoja apoteze ili mmoja ashinde.....changamoto kubwa ni kwamba wagombea wote wawili wana sifa zinazo fanana kuvutia wapiga kura. je, nani angefaa zaidi kama jf tungeamua?
1.Wote ni vijana
2.Wote wana majina makubwa...ingawa yanazidiana, nani kubwa zaidi?
3.Wote wasomi, ingawa wanazidiana, anani zaidi?
4.Wote wanajitambulisha kama wapinga ufisadi, nani zaidi?

NANI NI NANI HAPA?...TUMPOTEZE NANI? TUMPATE NANI?


Mleta mada hii sijajua kama kaja kupima upepo ama alitaka kusikia nini toka kwetu sisi . Nape is a waste and opportunist na hivyo hafai hata kidogo .Nchi inaishia mtu anasema nani zaidi ? CCM ina wabunge wasomi wengi na wazuri lakini leo wako wapi ? Ni chatu ukisha ingia unamezwa na ukibisha unaitwa Dodoma akina Guninita wana anza zao. Sijapenda kichw acha habari maana hapa hakuna ushabiki but we are on serious matters .Kuweka CV kwangu hakusaidii maana CCM imejaa watu wenye PhD za kweli wengi na wana nafasi kwa njia moja ana nyingine na hata za Ubunge pekee ila nini kinatokea ? Ni silikubaliani na hili ila naunga hoja mia kwa mia .

Mnyika can make a change . Mlitaka Mnyima abebe pesa zake mfukono apeleke Ubungo ndipo mjue kwamba yupo ama ?
 
Mnyika ni Mwanasiasa Makini na pia Nape anatumia tu agenda hiyo lakini hawezi kufaa katika kuongoza Ubungo then Nape na Keenja hakuna jipya juu yao lakini mimi naona kuwa Mnyika ni Mtu makini sana na Pia Mwanasiasa Makini katika Kizazi Kipya. Kura yangu kwa Mnyika sio huyu Nape wenu
 
Kwa Ubungo kunahitajika mtu makini anayeweza kusimamia maendeleo kwani pale kuna vichwa na wazee wanaojiita ndio wenye nchi. Nape pale hapamfai kwani hawezi kukemea. Kuna mradi wa mzee Kingunge ambao umejaa dhuluma pale Ubungo terminal kwa Nape hawezi kumkemea baba yao Kingunge, Londa na wengineo. Kura yangu ni kwa Mnyika kwani atakuwa ametoka Chama tofauti na wanaojiita wazee.
 
Nape hamuwezi mnyika kwa hapo ubungo,ila ni vizuri kwa watu wa upinzani kama watapata kuchuana na mgombea kama huyo. Lakini kwa Ubungo ccm safari hii hawana jinsi,wahesabu maumivu tu,kura zote ni Mnyika!!!!
 
Nape hamuwezi mnyika kwa hapo ubungo,ila ni vizuri kwa watu wa upinzani kama watapata kuchuana na mgombea kama huyo. Lakini kwa Ubungo ccm safari hii hawana jinsi,wahesabu maumivu tu,kura zote ni Mnyika!!!!

This is good news.Kila mtakia mema taifa hili angependa hii iwe kweli.One BIG question is: mkuu,do you have any research results supporting this?
 
Theory ya Ayubu Rioba haifanyi kazi hapo? kwamba CCM hata wakiweka Ng'ombe mchaguliwa ni CCM?
 
Mnyika namkubali kwa uwezo alotuonyesha mbele ya Mzee kama keenja na pia Mnyika yuka serious kwenye politiki! Nape anajaribu tu kutumia influnce ya wazee wake lakini sioni potantiality kwake.
 
tatizo la Nape tayari anajiona kamaliza safari kabisa....pia personal issues zitamponza, katika umri alionao si busara aendelee kukaa kwa baba mkwe wake pale Jesus Village-Changanyikeni, itashusha imani kwa wapiga kura...pia hana ukaribu na vijana wengi waliopanga pale kwa baba mkwe wake, Brigadia Hemed, wanamlaumu sana kwa kujifanya hana time hata na salamu tu..na mwisho kabisa,ukiwaweka Nape na Mnyika kwenye mjadala, Nape ataachwa mbali sana...but tusubiri tuone coz hata Shamsa nae yumo..
 
Sichagui CCM ng'o! CCM haiwezi kubadilishwa na mtu mmoja. Hata Dk Slaa akiamia CCM, ajue kura yangu hapati. Lazima muelewe siasi za Chama. No one is ever bigger than Chama. In the end, bila kuwa na support, mtu binafsi hawezi kubadilisha chama. Hivyo Nape ni propaganda tu anafanya. Hawezi kabisa kuleta mabadiliko.
 
Nape anatumia umaarufu wa wa vita dhidi ya ufisadi kuchukua agenda politica lakini Mnyika bado yupo makini sana katika siasa, Nape labda aende kugombea udiwani wa CCM ndio utamfaa kwa kupiga majungu
 
Theory ya Ayubu Rioba haifanyi kazi hapo? kwamba CCM hata wakiweka Ng'ombe mchaguliwa ni CCM?
Inawezekana sana hasa ukiangalia jinsi watanzania walivyo ;wajinga.' lakini hata akishindwa jimboni bado ana nafasi ya kuteuliwa kuwa mbunge... mwenyekiti wao ana nafasi kumi za kuteua wabunge
 
Wote awafai kabisa ,Mnyinka ni kibaraka wa mbowe ana neneo mbele yake.
Nape ana hasira na maisha yalivyomuendea kombo toka kizazi cha baba yake mpaka chake.-kwahiyo akipata ubunge itakuwa shida tupu.
mimi ndio nafaaa kuwa mbunge wa ububgo.
 
Wote wanajitambulisha kama wapinga ufisadi, nani zaidi?

Hapa Nape anapinga Ufisadi upi? Ulionzishwa na nani? tunajua ufisadi umeanzishwa na CHADEMA wakiongozwa na Mwanasheria wao Lissu pale walipowataja vigogo 22 na wote wakasema wanaenda mahakamani na hakuna aliye enda hadi leo kushitaki. Kwa maana kuwa yaliyosemwa yote ni kweli! Hebu Nape atulie asitusumbue Mshaurini hivyo.hatutaki kujua nani zaidi kwani Pumba na mahindi vinaonekana
 
Huyu Nape anatoka katika chama cha Matajiri, mafisadi, waleta umasikini, njaa, maradhi na ujinga. kwa absolute NO, hafawi kupewa hata ujumbe wa nyumba kumi, tangu lini mtu atoke kundi la washabikia maovu apambane na uovu, chama chake kimeshikilia jimbo la Ubungo na nchi muda mrefu sana hakuna mabadiliko yoyote ya maana yy Nape analipi jipya ambalo ni tofauti na yaliyotangulia kwa wananchi wa Ubungo na Tanzania?
Nampa advs kijana huyu shupavu Mnyika, hapahitaji tochi hapo, chama chake kina rekodi nzuri tu ya mapambano zidi ya uovu na ufisadi, yy mwenyewe ana 'vision' nzuri kwa kauli na matendo. Mwisho wananchi wanahitaji mabadiliko, tayari weshapima pumzi za CCM jimboni mwao na wanajuwe zilipowafikisha ndo hayo hayo kila mahala...ilani imetekelezwa asilimia mia...huku wananchi wanalala hoi...mpeni Mnyika si kwa kujaribu bali kwa kuwa anaweza na chochote kitafanyika bila ya shaka.
 
kumbukeni jamani mnapochagua mnachagua chama na sera zake hapa sio swala la Mnyika v/s Nape ila ni Chadema v/s CCM. Mimi chaguo langu ni la chama gani kinafaa kushika jimbo la Ubungo......let us give chadema a chance
 
Mnyika wala huwezi kumlinganisha na Nape. Mnyika ana uwezo zaidi wa uongozi na ana mtaji tayari katika jimbo. Nape nina wasiwasi kama atapita ndani ya mchuzo wa chama chake. Hata akipita atakuwa majeruhi tayari wakati Mnyika atakuwa anasubiri majeruhi gani wa kudili nae. Nape bora atafute jimbo lingine la Dar. Ubungo ni ya CHADEMA, Ubungo ni ya Mnyika!
 
Back
Top Bottom