Ubungo 2010: Nani zaidi, Nape au Mnyika?

Sure! Labda siku hizi kuna kubadilika kidogo, tena kwa kuwa ni mjini. Lakini kwa uzoefu wa Bongo, CCM ikiweka msukule inashinda bwana. Hali itabadilika chama kipya kingine kikiingia madarakani angalau na kubadilisha viburi vyote vya ccm juu ya uhalisia wa kila kitu. Ndio maana kwa ccm kipindi kigumu zaidi kwao katika masuala ya uchaguzi ni kipindi cha maoni ya uteuzi wa wagombea. Vijijini bado mzuka wa ccm ndio huo. Katiba ya nchi ikibadilishwa kuwezesha vyama vingi kiukweli, na tume ya uchaguzi ikiwa huru kweli, hapo CCM itakuwa na kazi ngumu. SIo sasa. Mjini ndiko kwenye upinzani kwa ccm kwa sababu watu wanajua mambo mengi. Kijijini wanajua CCM ndio amani yao, wengine bado wanaamini raisi wake ni Nyerere mpaka leo, na TANU ni chama chake ila kimebadili jina na kuwa CCM.
 
Tuwekeeni basi na wasifu wa Mnyika

Mnyika is readily available online. Ukitype jina kwenye google tu huyo kaja chap chap,mpaka glob yake utaiona. So easy! Lakini huyo mwingine historia yake imejifichaficha tu! Eti Nape ana certificate,stashahada,stashada,stashada,stashada,shahada ya india,anasoma masters(where,when? siri ya chama)
 
Mnyika yukoo juu sana kimawazo, fikra hata kiutendaji kumlinganisha na huyooo mpendaa sifa nape na wale wote wanaojiita wapinga ufisadi uliowaweka hapo walipoooo..

Ubungo for Mnyika, period.
 
Nadhani Achebe ametusadia wakati tukisubiri ya Mnyika nimepata miaka na vyuo alivyosoma Nape. Na kwakweli ni kati ya wanasiasa walosoma kwa kukaa darasani na sio online kama za 'ma Dr' flani tunaowajua. Na nimethibitisha na watu wa TUC, wanaohusika na uthibitishaji wa vyeti.

...2002/2003-Kivukoni- Stashahada
...2003/2004-Chuo cha Diplomasia Dar
Stashahada ya Diplomasia
...2005/2008- Bangalore University India
Shahada ( B.A- Psychology)
...2008/2009- Mzumbe Univer.
MPA
Nk.
Sasa tulinganishe na Mnyika ambaye hata degree ya kwanza imemshinda kumaliza,tena bado mtoto wa mama,anakula na kulala kwa mama yake, Nape anamke na anajitegemea!
Lakini hata hoja,hivi kweli tukiacha ushabiki,UBAFIKI WA MNYIKA KWA CHAMA CHAKE MNATAKA KUMLINGANISHA NA NAPE ALIYETHUBUTU KUPINGA UFISADI HADHARANI WA VIGOGO WA CHAMA CHAKE?
TENA AKASIMAMA KIDETE MPAKA IMEKUJA JULIKANA ALICHOKISIMAMIA KILIKUWA KWELI? MNYONGE MNYONGENI HAKI YAKE MPENI.

From that above CV, Nape hana uwezo wa kuongoza jimbo lilo jaa wasomi kama Ubungo... Send the kid somewhere else.
 
From that above CV, Nape hana uwezo wa kuongoza jimbo lilo jaa wasomi kama Ubungo... Send the kid somewhere else.

Tell them. Wakamfanyie kampeni sehem nyingine kama kweli wanampenda. Kumwacha Ubungo ni sawa na kumuua nyani tu(usimwangalie usoni). Ushauri wa bure huo sitaki reward ktk hilo. Come 2010, we want to prove our hypotheses!
 
Cha muhimu hapa kama wewe ni mkazi wa Ubungo jitahidi kuhamasisha na kujiandikisha. Wameanza tokea jana kujiandikisha hicho ndo kitu muhimu.
Sitaki kumwaga mchele kwenye kuku wengi kama wewe nimtu mwenye kujiamini hakikisha kura zinazopigwa haziibiwi na mafisadi.

Kampeni za *** wameanza siku nyingi sitegemei kama Nape atapata kwenye chama chao.
 
Jibu la swali hili linategemea na nani mwenye mfuko zaidi ya mwenzake!..Ndio reality hakuna sababu nyingine kwa Mdanganyika. Kama Mnyika anazo zaidi ya Nape basi bila shaka Mnyika lakini kama wote ni walalahoi utapima umaskini wao..
Nitarudia maneno yangu huwezi kushinda uchaguzi wa Ubunge Tanzania kama huna FEDHA..hicho ndicho kipimo, hivyo nani zaidi ni yule mwenye fedha kwa minajiri ya Takrima.
 
Keenja ametangaza kutogombea?

Mkuu Masanilo, Keenja anaweza kutangaza wakati wowote kuanzia sasa nia yake ya kutogombea ubunge mwaka 2010.

Mjadala huu unaelekea kujaribu kupiga kampeni ya nani anaetakiwa kuwa mshindi wa Ubunge (Ubungo)
utakapofika uchaguzi wa mwaka 2010. Nadhani muda ukifika, ndipo itakuwa rahisi zaidi kutabiri nani anaeweza kushinda na kuwa Mbunge (Ubungo).

Kwa sasa hata kama kelele zetu za nani anaeweza, anaefaa na atakaeshinda zikipamba moto kiasi gani, hazimaanishi kuwa matokeo ndivyo yatakavyokuwa. Watu wengi hubadili mawazo wanapofika kwenye sanduku la kura. Kura nyingi nchini huwa ni floating votes. Zinaweza kumwangukia yeyote.

Nadhani tusubiri tuone. Nina uhakika kuwa CCM itakuwa na ushindani mkubwa sana katika kura za maoni kuliko katika uchaguzi mkuu. Maana kila mwezi jina moja huongezeka katika wanaotarajia kugombea Ubunge (Ubungo).

Ukweli ni kuwa, vita dhidi ya ufisadi haitakuwa ajenda kuu katika uchaguzi huo. Wananchi wameshasikia mengi sana, na wanajua udhaifu uko wapi na nini kinachotakiwa kufanyika. Kusema kuwa fulani au chama chake kinapinga ufisadi na hivyo ndie mtu/chama kinachofaa ni kujidanganya sana. Mafisadi wakishakabiliwa ipasavyo ina maana ndio mwisho? Inatakiwa wakabiliwe, na vile vile mipango ya maendeleo iwe ndio ajenda muhimu zaidi. Ufisadi ni uhalifu kama wizi na ujambazi. Haiwezekani kupambana na wezi ikawa ndio ajenda pekee na yenye umuhimu peke yake.
 
Mnyika is often reside in America and seldomly in Tanzania put away his constituency.
I'll never bet on it B'se Nape is handsome to Mnyika meanwhile politics is not only about ability but even appearance.
 
Nyie thinkes acheni wapiga kura wapige kwanza....mbona mna kiherehere kama mchuzi wa matembele
 
hatuchagui mtu wala sura hapa,tutaangalia sera za chama zenye menufaa na tija kwa wananchi wa jimbo la ubungo.

Marehemu baba wa taifa aliwahi kusema kama unapenda mtu kwa sura yake au umaarufu wake mchukue uende ukanywe nae kahawa au whisky
 
Mnyika is often reside in America and seldomly in Tanzania put away his constituency.
I'll never bet on it B'se Nape is handsome to Mnyika meanwhile politics is not only about ability but even appearance.

Jamani hii lugha ya wenzetu tuwaachie wenyewe kama hatuiwezi.
 
hatuchagui mtu wala sura hapa,tutaangalia sera za chama zenye menufaa na tija kwa wananchi wa jimbo la ubungo.

Marehemu baba wa taifa aliwahi kusema kama unapenda mtu kwa sura yake au umaarufu wake mchukue uende ukanywe nae kahawa au whisky


dogo una akili sana!! tatizo hawakusikii
 
nyie thinkes acheni wapiga kura wapige kwanza....mbona mna kiherehere kama mchuzi wa matembele
si busara kuwaachia wapiga kura kupiga kura,maoni haya hapa yanafaa kuwasaidia wapiga kura kujua hasa wamchague nani.
Isitoshe kati ya hawa wachangiaji hapa wapo wapiga kura pia. Isitoshe mnyika na nape huingia hapa jf ikiwezekana wasign in tuwaulize hapa!
 
Hivi kweli Nape anasemwa hafai kwa jimbo la wasomi kama Ubungo,hivi nani afadhali kati ya Nape anayemalizia degree ya pili na Mnyika ambaye hata degree ya kwanza imemshinda kama mwenyekiti wake Mbowe??
Kuna moja hapa kadai alimsikiliza Nape kwenye mdahalo itv akagundua hana uwezo, hii nayo ya ajabu,siku hiyo nlikuwa namtazama Nape na baadhi ya Maprofesa wa chuo kikuu walikiri kuwa kijana ana uwezo na hasa alivyoweza kufafanua yanayoendelea Pemba nk
 
Kuna moja hapa kadai alimsikiliza Nape kwenye mdahalo itv akagundua hana uwezo, hii nayo ya ajabu,siku hiyo nlikuwa namtazama Nape na baadhi ya Maprofesa wa chuo kikuu walikiri kuwa kijana ana uwezo na hasa alivyoweza kufafanua yanayoendelea Pemba nk

Hao maprofesa wa chuo kikuu sio litmus test ya nani anafaa au kutofaa
 
Back
Top Bottom