KERO Ubovu wa Barabara ya Kawawa unatupa mateso makali Wananchi wa Goba Matosa

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Naomba ujumbe huu uwafikie Viongozi wetu wa huku kwetu Goba Matosa Uzaramuni kuna changamoto ya Barabara ya Kawawa (Kawawa Road) imeharibika kwa kiwango kikubwa.

Huu ni mwezi wa nne tangu hali iwe mbaya zaidi, kila kiongozi anayekuja kazi yake ni kupiga picha na kuondoka lakini utekelezaji ni zero.

Barabara imeharibika kuanzia Msikitini wa Uzaramuni hadi Bondeni, Watu nyumba zao zinaning’inia kutokana na uharibifu wa mvua za tangu Mwaka jana (2023) hadi Mwaka huu (2024), tuomba kusaidiwa jamani, viongozi wetu wa Wilaya ya Ubungo (Dar es Salaam) wanatakiwa kuwajibika kwa kinachoendelea.

Wakati huu mvua zinanyesha hali ni mbaya zaidi kufika kwenye makazi yetu.
WhatsApp Image 2024-04-09 at 16.21.49_035ed92a.jpg

WhatsApp Image 2024-04-09 at 16.18.39_45ed3d2f.jpg

WhatsApp Image 2024-04-09 at 16.18.28_247498a2.jpg
 
Huko matosa ni pabaya kishenzi, nlipita juzi kwa kutokea pale njia nne kwenda kimara mwisho , Aisee hapafai, kama mtu anaishi kule alafu amepanga nyumba ,akapimwe akili yake
 
Back
Top Bottom