SoC01 Uboreshaji wa Shule za Upili za Ufundi Tanzania kuleta tija zaidi

Stories of Change - 2021 Competition

Aidx2021

Member
Jul 17, 2021
11
15
Shule za Upili za Ufundi Tanzania (Technical Secondary Schools in Tanzania) ni shule maalumu zilizoanzishwa kwa dhumuni la kuandaa wataalamu. Zilijidhatiti zaidi kuandaa vijana wenye umri mdogo, mafundi makenika, umeme, useremala, ujenzi, usanifu, ushonaji na ususi. Lengo kuu lilikuwa ni kuandaa vijana watakao weza kuhimili kishindo cha ajira wamalizapo masomo kwa kuwajengea uwezo wa kujiajiri au wajitegemee katika maisha yao bila kutegemea ajira za Serikali wala Mashirika.

Kipindi shule hizi zinaanzishwa, serikali ilidhamilia kuandaa Taifa la vijana wenye kujitegemea kama sera ya wakati ule ilivyokuwa ikijieleza kuwa “Taifa la Ujamaa na Kujitegemea”. Suala hili liliwekwa wazi zaidi katika Azimio la Arusha (1967). Pia, wazo hili lilikuwa ndio kiini cha Falsafa ya Baba wa Taifa, Mwl. Julius K. Nyerere aliamini katika kujitegemea katika nyanja tofauti mfano kielimu, kisiasa, kiafya, kijamii, kimaendeleo, n.k. katika kutengeneza Taifa Bora la Tanzania.

Tunaweza kusema kuwa Shule za Upili za Ufundi ilikuwa ni shabaha na mwarubaini wa ajira kwa Taifa. Shule hizi zilikuwepo kabla ya Uhuru na kuendelezwa na Baba wa Taifa J.K Nyerere. Miradi kama hii ni hadhina kwa Taifa iliyoachwa na Wazungu. Inasikitisha kuwa imetelekezwa na serikali hata wanaharakati hawapambanii hili. Machungu yamebaki kwa wale waliosoma katika shule hizi kama mimi. Mambo sio mazuri kwa sasa shule zinashuka hadhi kila kukicha, kitaaluma, kimaendeleo n.k.

Ukipata muda, wekeza kwa kutembelea shule mojawapo, utakachokikuta ni hadhina ya mashine na walimu vikongwe waliobaki kujitolea kwa ajili ya vijana wa leo. Kitu ambacho kinavunja moyo kwa kutupwa mkono shule hizi. Unaweza kusema hakuna usimamizi wala mkakati wa kuendeleza shule hizi kwa namna Wizara na Serikali kwa ujumla walivyotupa kisogo katika suala hili.

Katika chapisho hili nitakutajia shule zilizokuwa zikifundisha masomo ya Ufundi, Ususi, Ushonaji na Udobi. Shule hizo ni kama zilivyoorodheshwa hapa chini katika jedwali;

Shule Program Dokezo
Ifunda tech, Iyunga tech, Tanga tech, Musoma tech, Moshi tech, Mtwara tech, Bwiru boys, Mazengo Alliance (tech).Ufundi umeme, Ufundi makenika, Ufundi ujenzi na usanifu wa majengo, Ufundi radio na televisheni (TV).Shule ya Ufundi Mazengo imebadilishwa na kuwa Chuo Kikuu cha St John.
Shule zingine zipo.
Ashira na Zanaki sekondariUshonaji, Ususi, Udobi na Upishi.Shule zipo


Shule za Upili za Ufundi Tanzania zimesahaurika sana. Changamoto ni nyingi sana. Mara ya mwisho nilitembelea Shule ya Upili ya Ufundi ya Iyunga mwaka 2018. Nilifanikiwa kuingia katika karakana zote zilizopo katika shule ile. Utafurahishwa na umaridadi wa mashine na vifaa vingine vilivyopangiliwa, ubora wa vifaa vilivyopo ni wajuu sana. Lakini kitu cha kukatisha tamaa ni kwamba; vifaa havifanyi kazi, chanagamoto ni muunganiko wa umeme baina ya vyanzo na vifaa. Kitu ambacho kinadhorotesha muamko kwa wanafunzi kuwekeza muda kwa ajili ya kujifunza masomo ya Ufundi.

Pia, nilibahatika kuongea na baadhi ya wanafunzi na walimu pale shuleni. Wanafunzi walidai kuwa hakuna wanachofundishwa kwa vitendo bali nadharia tu. Kwa mfano, mwanafunzi amesoma nadharia ya umeme miaka mine lakini hawezi hata kutengeneza sakiti ya umeme yenye taa moja na swichi moja kwa vitendo.

Pia, unakuta mwanafunzi amesoma ujenzi na usanifu wa majengo, anachokiweza kwa kiasi fulani ni nadharia tu na kuchora michoro iliyobuniwa lakini ukimwambia afyatue tofali lenye kukidhi vigezo hawezi hata kidogo. Je huyu kijana atakuja kujiajiri? Kijana huyu akirudi nyumbani atakuwa mbabaishaji tu atafanya vitu ambavyo havikamiliki na havitakamilika kamwe.

Walimu nao walinena, walidai kuwa hakuna vifaa kwa ajili ya kufundishia kwa kigezo cha kwamba vifaa vingi havina muunganiko wa umeme ili vitumike. Pia, hakuna program maalumu kwa ajili ya kuwaimarisha walimu kwani taaluma ya ufundi kila siku inabadilika. Pia uchache wao ni kikwazo, wastani wa walimu kwa wanafunzi haukubaliki. Kuna baadhi ya program za ufundi walimu hakuna kabisa, utakuta kikongwe miaka zaidi ya 75 anajitolea baada ya kustaafu anafundisha vijana angalaau awaokoe wapate kujua ABC za somo hilo.

Kiukweli inauma sana kwa wadau wa Elimu ya Ufundi. Nakumbuka nilivyomaliza kidato cha nne, Moshi Shule ya Ufundi, miaka saba iliyopita. Changamoto nilizopitia ni nyingi. Kwanza nilipofika nyumbani, Baba yangu aliniambia nibadilishe taa ya valandani, sikuweza hadi nilipoenda kwa rafiki yangu aliyesoma VETA akanisaidia vifaa na tukashirikiana naye kubadili taa ile. Kwa sababu nilisoma nadharia zaidi kuliko vitendo.

Ukweli ni kwamba licha yakuwa shule hizi ni kubwa kama zinavyofahamika, lakini ni bora usome VETA kama unalengo la kumfanya kijana wako awe fundi kweli au kama kijana anahitaji kuwa fundi wa kweli kwa sasa ajiunge VETA kuliko shule hizi. Hadhi ya shule hizi imekwisha imebaki kama shule nyingine za kata (za wazazi). Wazee wetu ndio waliosoma kweli Shule za Ufundi za Upili kwa ukamilifu kwani walijifunza zaidi kwa vitendo.

Kuna wakati najiuliza hivi Wizara ya Elimu na serikali inaliona hili? Nasikitika pia kuona shule hizi zinafundisha michepuo ya “Arts” kwa kuanzisha ufundishwaji wa somo la Historia katika shule hizi. Sikuelewa kigezo kipi kimepelekea Wizara ya Elimu kuanzisha program hii kwani shule hizi ziliandaliwa kwa ajili ya masomo ya Sayansi na Ufundi tu.

Dhima kuu ya kuwepo shule za ufundi ni kuzalisha wanasayansi kama vile madaktari, wahandisi, marubani nk. Pia kuzalisha mafundi watakao jiajiri wenyewe hata kama hawakufanikiwa kuendelea na masomo ya juu zaidi. Walimu waliopita katika shule hizi kabla ya kwenda kusomea ualimu ni walimu wazuri sana wa sayansi na wanategemewa sana kutokana na uzoefu wao katika masomo hayo. Kwa ujumla, shule za Ufundi zina tija kubwa sana kwa taifa letu la Tanzania.

Shule za Ashira na Zanaki ni shule kongwe za wasichana zilizokuwa na mchepuo wa Ushonaji na Ususi (Needlework) pamoja Upishi (Cookery). Ukienda katika shule za Ashira na Zanaki kwa sasa utakuta madarasa na vifaa kwa umaridadi vimewekwa kama vile Cherehani za mezani, Cherehani za umeme, Majiko ya umeme tena makubwa na ya gesi. Inasikitisha sana kwamba vyote hivyo havitumiki kama ilivyolengwa, kwa mfano utakuta chumba chote cherehani zinazotumika ni mbili tu kati ya 25 na majiko matatu kati ya 20. Ukichunguza kwa makini zaidi utagundua pia cherehani zinazotumika ni zile za kawaida na sio zenye mfumo wa umeme hata majiko ni ya mkaa ndio yaliyo hai baada ya msamalia mwema kupita na kutoa msaada wa vifaa hivyo.

Tafsiri yake ni kwamba wanafunzi wanasoma zaidi kwa nadharia tu ili wajibu mitihani yao waende zao. Kitu ambacho kinaua dhana ya uanzishwaji wa shule hizi kwani hata shule ambayo haina vifaa inaweza kufundisha na kuwakaririsha wanafunzi nadharia bila vitendo kwa uwezo wao mkubwa, wakafaulu mitihani yao ya mwisho.

Swali hapa ni kwamba, Taifa hili halina umeme wa kutosha kuwasha vifaa hivi vitumike kwa ajili ya kufundishia vijana hawa? Au, walimu hawapo wakutosha na wenye uzoefu na masomo hayo? Je, hapo mwanzo walitoka wapi? Mwisho, tunategemea nini katika hili? Bila shaka tunazalisha vijana tegemezi katika Taifa, hawawezi kujiajiri wala hawana sifa za kuajirika.

Kwa mfano unakuta mwanafunzi amesoma mchepuo wa Upishi lakini hawezi kupika kwa ufasaha anapokuwa amerudi nyumbani hata wazazi wake wanamshangaa na kujihoji kwamba mtoto huyu amesoma mapishi au maneno.

Ningependa kutoa maoni ya namna gani ya kurudisha hadhi ya shule hizi kama ifuatavyo;

Napongeza kwa hatua iliyochukuliwa na Serikali na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia katika uboreshaji wa majengo na miundombinu ya shule kongwe zikiwemo na shule za Ufundi. Hilo natoa pongezi kwa mamlaka husika. Lakini nasisitiza sio tu waboreshe muonekano wa majengo kwa nje halafu ndani hamna cha maana. Mfano, karakana ni lazima zirudi katika uhalisia wake wa mwanzo, mifumo ya umeme irudishwe, mifumo ya maji taka na safi irudishwe, vifaa vilivyoharibika visivyorekebishika viondolewe na viwekwe vipya.

Napendekeza idadi ya walimu iongezeke, uwiano kati ya wanafunzi na walimu haukubaliki katika shule hizi. Walimu wazee (Vikongwe) wapunguzwe kwani uwezo wao umepungua. Walimu hawa wawe wenye sifa na uzoefu katika program za ufundi kwa vitendo. Pia walimu hawa, waandaliwe mkakati endelevu (Special Upgrading Program) katika kuongeza ujuzi na ujasiri (confidence) wa kufundisha masomo ya ufundi kwa vitendo kwani taaluma ya Ufundi inabadilika kila kukicha.

Serikali iandae utaratibu maalumu kuhakikisha upatikanaji na ugawaji wa rasilimali (Materials and Resources). Mamlaka zina wajibu wa kusimamia matumizi sahihi ya rasilimali hizo kwa ukaribu, itapunguza urasimu unaofanywa na baadhi ya watumishi wenye mamlaka katika hili. Ni kitu kisichofichika kuwa rasilimali zitokazo serikalini kwa kusudi la kufundishia na kujifunzia wanafunzi, hazitumiki kama zilivyokusudiwa. Mfano, wakuu wa vitengo vya program za Ufundi wakishirikiana na watu wao na Wakuu wa shule hizo hujimilikisha mali hizo na kuzipora kwa faida yao.

Wahusika wanaofanya uchaguzi wa wanafunzi wanaotegemewa kujiunga na Shule za Ufundi ni lazima wazingatie vigezo na sifa za kitaaluma. Mfano, ni lazima mwanafunzi anayejiunga katika shule hizi awe ana ufaulu wa juu wa masomo ya Hisabati na Sayansi. Ile tabia ya kujuana au upendeleo kutoka kwa Wakuu wa shule na Wakuu wa vitengo ukomeshwe.

Serikali ibuni mpango endelevu wa kutoa motisha kwa walimu na wanafunzi wanaofanya vizuri katika masomo ya Sayansi na Ufundi. Hii itatoa hamasa kwa walimu na wanafunzi wao kuwekeza mda, kufundisha na kujifunza zaidi Sayansi na Ufundi. Italeta ushindani baina yao matokeo yake tutapata vijana makini wenye uwezo wa kujiajiri na kupambana katika soko la ajira (Competitive Advantages).

Bila kupepesa macho, ninapendekeza Wizara husika iandae mkakati wa kuwatambua wanafunzi wanaomaliza kidato cha nne katika program zao za ufundi. Nikimaanisha wapewe vyeti maalumu kutokana na program za ufundi walizosomea. Utambulisho huu utawasaidia kutambulika na kuwajengea ujasiri na ushindani (Competence).
 
Leo nimeongea na Mkuu wa Moshi Ufundi anasema yote yako sahihi maboresho ni lazima yafanyike kuokoa shule hizi
 
20210610_145122.jpg
 
Katika ule mkeka wa ajira 13,000/= waliajiri engineers 16 kila shule ya ufundi lengo kuzifufua.. ila serikali imewavunja moyo vijana hao kwa kuwalipa mishahara sawa na ya ualimu
 
Ha haa! Nilisoma topic ya AC motors. Kitu pekee nilichoambulia ni Ameture! Nadhani tulikuwa tunafundishwa vitu vikubwa tofauti na uwezo wetu.

Kuhusu mwanafunzi kutoweza kutengeneza circuit ya taa moja huo ni uzembe wake. By the time naingia form two, tayari nilishakuwa nimepata uwezo wa kufanya wiring na practical yangu ya kwanza ilikuwa kwenda kutengeneza umeme kwenye nyumba ya headmaster nikimsaidia mwanafunzi wa form three.

Cku moja umeme ukaharibika Dinning nikaitwa kwenda kutengeneza, wee, nilibaki natetemeka kwa kuwa at the age of 17, bado nilikuwa kanjanja. Nafika pale nakutana na zile main switch za enzi za mkoloni. Nikajisemea sasa leo nauwawa na umeme au nadhalilika na ukanjanja wangu... Nikala kona.
 
Umedadavua vyema sana. Unayo kura yangu. Ngoja nikitumia computer natumaini nitaona pa kuweka kura
 
Ha haa! Nilisoma topic ya AC motors. Kitu pekee nilichoambulia ni Ameture pekee. Nadhani tulikuwa tunafundishwa vitu vikubwa tofauti na uwezo wetu.
Kuhusu mwanafunzi kutoweza kutengeneza circuit ya taa moja huo ni uzembe wake. By the time naingia form two, tayari nilishakuwa nimepata uwezo wa kufanya wiring na practical yangu ya kwanza ilikuwa kwenda kutengeneza umeme kwenye nyumba ya headmaster nikimsaidia mwanafunzi wa form three.
Cku moja umeme ukaharibika Dinning nikaitwa kwenda kutengeneza, wee, nilibaki natetemeka kwa kuwa at the age of 17, bado nilikuwa kanjanja. Nafika pale nakutana na zile main switch za enzi za mkoloni. Nikajisemea sasa leo nauwawa na umeme au nadhalilika na ukanjanja wangu... Nikala kona.
Sasa iyo wew ulifanya kipindi hichooo alaf ulikuta ndo waalimu wazalendo wanamaliza zama zao, nenda leo utafurah au nenda kaulize aliyepita 2012 to 2020 kama anaweza hata muulze Miniature Circuit Breaker kana anaijua hata mchoro wake hajui
 
Ha haa! Nilisoma topic ya AC motors. Kitu pekee nilichoambulia ni Ameture pekee. Nadhani tulikuwa tunafundishwa vitu vikubwa tofauti na uwezo wetu.
Kuhusu mwanafunzi kutoweza kutengeneza circuit ya taa moja huo ni uzembe wake. By the time naingia form two, tayari nilishakuwa nimepata uwezo wa kufanya wiring na practical yangu ya kwanza ilikuwa kwenda kutengeneza umeme kwenye nyumba ya headmaster nikimsaidia mwanafunzi wa form three.
Cku moja umeme ukaharibika Dinning nikaitwa kwenda kutengeneza, wee, nilibaki natetemeka kwa kuwa at the age of 17, bado nilikuwa kanjanja. Nafika pale nakutana na zile main switch za enzi za mkoloni. Nikajisemea sasa leo nauwawa na umeme au nadhalilika na ukanjanja wangu... Nikala kona.
Sasa iyo wew ulifanya kipindi hichooo alaf ulikuta ndo waalimu wazalendo wanamaliza zama zao, nenda leo utafurah au nenda kaulize aliyepita 2012 to 2020 kama anaweza hata muulze Miniature Circuit Breaker kana anaijua hata mchoro wake hajui
 
Ha haa! Nilisoma topic ya AC motors. Kitu pekee nilichoambulia ni Ameture pekee. Nadhani tulikuwa tunafundishwa vitu vikubwa tofauti na uwezo wetu.
Kuhusu mwanafunzi kutoweza kutengeneza circuit ya taa moja huo ni uzembe wake. By the time naingia form two, tayari nilishakuwa nimepata uwezo wa kufanya wiring na practical yangu ya kwanza ilikuwa kwenda kutengeneza umeme kwenye nyumba ya headmaster nikimsaidia mwanafunzi wa form three.
Cku moja umeme ukaharibika Dinning nikaitwa kwenda kutengeneza, wee, nilibaki natetemeka kwa kuwa at the age of 17, bado nilikuwa kanjanja. Nafika pale nakutana na zile main switch za enzi za mkoloni. Nikajisemea sasa leo nauwawa na umeme au nadhalilika na ukanjanja wangu... Nikala kona.
Dah nashukuru nilipita pale Alliance nikapata elimu ya unga
 
Zanaki sekondariUshonaji, Ususi, Udobi na Upishi.Shule zipo

Hamna kitu, hii sera ndio maana inafeli....
Yaani Zanaki Sec, shule kongwe ya kina Maria Sarungi ndio inakuwa na hizi kozi za kusutana na umbea
Wakati nasoma Zanaki Primary tulikuwa tunaenda kwenye hall yao ilikuwa na Grand Piano iko pale tunaichezea na wadada walikuwa wanafundishwa kuitwanga, basi kweli imekuwa...
Ualimu pasipo Elimu (UPE)
 
Labda wakiacha kununua landcruiser na kuanza kulipa kodi kama wengine, lakini nafikiri siku hizi wamekuja na hivi vyuo vya ufundi kila wilaya sijui kata, watu binafsi nao washiriki kuanzisha vyuo kuendeleza hizi elimu za ufundi
 
Hili andiko ndio bora kuliko yote niliyosoma KATIKA shindano hili. Limefuata hata za msingi za uandishi. Mfululizo mzuri Sana. Kifupi amebobea KATIKA uandishi #aidx hongeraa zaki. JF judges tazameni hili, mwandishi mzuri Sana. Pengine ni lulu.
 
Upo sahihi sana, nilipitia technical school O level, kwakweli ni majanga siyo poa kabisa yani.Department nyingi hazina walimu,mashine zimekufa na serikali haina mpango wa kuzifufua.Kwa ufupi hizi shule zipo zipo tu tofauti kusudio la uanzishwaji wake.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom