One Plus 6 haikai na chaji halafu bado ni Android 8.1, kumbuka hii ni 2023. Kama ni laki nne kwa Bongo bora ujinunulie "Xiaomi Redmi 10" plain upate simu iliyobalance specifications kwa standard ya 2023. Display yake ni IPS LCD ingawa gsmarena amethibitisha kuwa bado ina mwanga wa kutosha na unaweza kuitumia juani. Pia ina kamera ambayo haina mpinzani kwa bei yake. AnTuTu score yake ni kama ya One Plus 6 na bado inakaa na chaji, unapata mpya full and sealed box

Wazee wa AliExpress kwa chini ya laki tatu na nusu unajipatia "Xiaomi Redmi Note 10 5G" ya 4GB RAM 128GB ROM na "Xiaomi Poco M5" ya 4GB/64GB na Xiaomi Redmi Note 11 ya 4GB/64GB kwa around 367,000/=. Hizi simu zinauzwa bei hii kwenye store kubwa zenye positive reviews nyingi, rating ya above 4.5 na order nyingi sana mfano store ya Goldway huko AliExpress
Kwa laki nne unajipatia Realme 8 safi kabisa huko AliExpress. Binafsi sishauri kununua simu used
Kama shida ni simu used kuna Sony Xperia XZ3 kwa around 300K ambayo Ina Android 9 au hata LG G8, otherwise nunua simu mpya ambayo ni bora yenye standard nzuri ya Sasa na inayotunza chaji.