humu watu walikuwa wanazisifia zina quality nzuri ya picha, siku moja nilitembelea banda moja la game nikakuta wamezieka, tv zipo kwa chini kidogo, nikisimama tu tayari ule ubora wa picha unapotea inataka uiangalie straight, inamaana haitumii ips technology.
hivi vitu ambavyo hata ukivigoogle zinakuja result za Africa tu muwe mnakaa mbali navyo, vingi ni watu wanaenda China wananunua vitu na kubrand majina yao, havijulikani hata vimetengenezwa kiwanda gani.
kama Huna budget ya kutosha Tafuta TCL ni mchina anayeaminika na bei zao zinafanana na hao kina Boss na Star X.